Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda.
Na Emmanuel Masaka,Globu ya jamii
JOPO
la wataalam kutoka ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, maofisa Ustawi wa
Jamii, Wanasheria pamoja na askari Polisi wa dawati la Jinsia
wamemuhakikishia Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda
wamejidhatiti vyema kuwasikiliza akinamama ambao wametelekezwa na
hawapati fedha za matunzo ya watoto kutoka waume zao.
Ofisi
ya Mkuu wa Dar es Salaam ilitangaza kutoa msaada wa kisheria kwa
kuwasikiliza wanawake hao na kwamba watatoa msaada huo kwa siku tano
kuanzia Aprili kuanza April 9 mwaka huu.
Akizungumza
na wataalamu hao leo, Makonda amesema tatizo la wamama waliotelekezwa
ni kubwa na limekuwa likisababisha kinamama na watoto kuishi maisha ya
tabu na kusababisha ongezeko la watoto wa mitaani na vizazi vya watoto
wenye chuki na baba zao.
Makonda
amesema lengo la mchakato huo si ugomvi bali ni kumwezesha mtoto
kupata mahitaji ili aweze kuitumia vyema fursa ya elimu bure chini ya
Serikali ya awamu ya tano.
Pia amesema amewahimiza wataalamu hao kuhakikisha wanawasikiliza kinamama kwa umakini na kusimamia haki pasipo upendeleo.
Pamoja
na hayo Makonda amesema wapo kinababa ambao wameanza kutoa fedha ya
matunzo ya mtoto baana ya kusikia tangazo ambapo amewaomba kinamama
kufika Aprili 9 mwaka huu kwa ajili ya na watalaamu ili waingie kwenye
mfumo rasmi wa kimaandishi.
"Ifike hatua mwanaume ukimpa mwanamke ujauzito bila mpangilio aogope kama ilivyo kwenye ubakaji,"amesema Makonda.
Comments