Wednesday, March 21, 2018

KAMISHNA UHAMIAJI, DKT MWIGULU WAMSHUKURU RAIS KWA KUTOA FEDHA BILILIONI 10/- KWA AJILI YA KUJENGWA OFISI ZA IDARA YA UHAMIAJI DODOMA

"Sisi Idara ya Uhamiaji tunajukumu la kufuata taratibu zote kwa haraka iwezekanavyo ili jengo hili ndani ya mwaka wa fedha ujao liwe limekamilika kwsababu tayari fedha zipo,"amesema Dk.Makakala.

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk.Mwigulu Nchemba aambaye naye ametembelea eneo hilo la Mtaa wa NCC lililopo Manispaa ya Dodoma Mjini, ambako ndiko patajengwa ofisi hizo ambapo naye amemshukuru Rais kwa kutoa fedha hizo.

Dk. Mwigulu amemshukuru Rais, kwa kuwapa fedha hizo kwa ajili ya ujenzi makao makuu ya Uhamiaji na tayari kwa sasa eneo kubwa lenye mita za mraba 9,777 limepatikana kwa ajili ya kujenga jengo kubwa na la kisasa kwa Idara hiyo.
"Tunashumkuru Rais Magufuli kwa kutoa fedha ambazo zitatumika kwenye ujenzi wa ofisi za Idara ya Uhamiaji ambazo zitakuwa za kisasa.Eneo ambalo tumepata ni kubwa na litatosha kujengwa ofisi hizo,"amesema Dk.Mwigulu.

Amefafanua ni eneo ambalo lipo karibu na ofisi nyingine muhimu ikiwamo ya Ofisi ya vitambulisho vya Taifa, Zimamoto na ofisi nyingine za Serikali ambapo zitasaidia mtu anapofika eneo hilo kupata huduma kadri anavyohitaji.

Dk.Migulu ametoa rai kwa idara ya Uhamiaji kuendelea kuchapa kazi kwa bidii kwani kuchapa kazi kwao ndio kumefanya wao kupata fedha hizo za ujenzi kwa haraka na fedha za kununua nyumba za makazi ya askari Dodoma.
"Iwapo fedha ambazo Rais amezitoa wangefuata utaratibu wa bajeti basi ingechukua muda mrefu kuzipata lakini uchapakazi wao umemfanya Rais kutoa fedha hizo,"amesema Dk.Mwigulu.


Na Ripota Wetu, Blogu ya jamii

KAMISHNA wa Uhamajia nchini, Dk.Anna Makakala na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk.Mwigulu Nchemva wamemshukuru Rais Dk.John Magufuli kwa kuwapa fedha Sh.bilioni 10 kwa ajili ya kufanikisha ujenzi wa ofisi za Idara ya Uhamiaji mkoani Dodoma.

Kwa upande wake Dk.Makakala ametoa shukrani hizo kutokana na uamuzi wa Rais kutoa fedha hizo Sh.bilioni 10 kwa ajili ya ujenzi huo ambapo ameagiza zijengwe ofisi za idara hiyo ambazo zitakuwa za kisasa.Dk.Makakala amefafanua tayari wameshapata eneo kubwa kwa ajili ya kujenga ofisi zao.
Post a Comment