Thursday, March 15, 2018

SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA KUKARABATI MAJENGO UWANJA WA NDEGE DODOMA

Kaimu Mkuu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Bw. Richard Mayongela na  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Maagi wakibadilishana hati za makubaliano baada ya kutiliana saini makubaliano ya ukarabati wa majengo ya Uwanja wa Ndege wa Dodoma utakaogharimu kiasi cha shilingi milioni 623.

Picha ya pamoja ya viongozi mbalimbali walioongozwa na Mgeni rasmi katika hafla hiyo fupi alikuwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia masuala ya Ujenzi Injinia Joseph Nyamhanga, Mbunge wa Dodoma Mjini na Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Benilith Mahenge. Picha hiyo imepigwa baada ya utiaji saini.

 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Maagi akizungumza katika hafla hiyo fupi baada ya kutiliana saini makubaliano ya ukarabati wa uwanja huo wa ndege wa Dodoma

Shirika la Nyumba la Taifa limetiliana saini ukarabati wa majengo ya Uwanja wa Ndege wa Dodoma leo hii katika eneo la uwanja huo wa ndege wa Dodoma.
Hafla ya utiaji saini imefanyika leo kati wa Mamlaka ya Viwanja vya ndege nchini (TAAA) na Shirika la Nyumba la Taifa huku TAAA ikiwakilishwa na Kaimu Mkuu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Bw. Richard Mayongela na NHC Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Felix Maagi.
Ukarabati wa Majengo ya uwanja huo utagharimu kiasi cha shilingi 623milioni na unatarajiwa kuanza rasmi Aprili, 2018 na kukamilika baada ya miezi mitatu.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo fupi alikuwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye akiongozana na Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia masuala ya Ujenzi Injinia Joseph Nyamhanga, Mbunge wa Dodoma Mjini na Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Benilith Mahenge.
Post a Comment