Tuesday, February 21, 2017

MONDULI YAUNGA MKONO KUPIGA VITA MADAWA YA KULEVYA


Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo akizungumza na watumishi katika wilaya ya Monduli ,alipofanya ziara ya kukagua maendeleo katika halmashauri hiyo,aliyeko pembeni yake ni mkuu wa wilaya Monduli Idd Kimanta.picha na Vero Ignatus Blog.
Mkuu wa mkoa akipokea kadi ya CHF wilaya ya Monduli kutoka kwa mkuu wa wilaya hiyo Idd Kimanta,ili kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko huo.Picha na Vero Ignatus Blog
Baadhi ya watumishi katika halmashauri ya wilaya ya momduli wakifuatilia yaliyokuwa yanaendelea kwa makini.Picha na Vero Ignatus Blog
Mkutano unaendele wadau pamoja na watumishi wa wa halmashauri hiyo wakifuatilia yale yanayoendelea.Picha na Vero Ignatus Blog




Na.Vero Ignatus, Monduli.


Halmashauri ya wilaya ya Monduli imeendelea kuungana na vyombo vya ulinzi na usalama na wananchi katika kupiga vita dhidi ya madawa ya kulevya .

Hayo yamebainika katika taarifa iliyosomwa mkurugenzi wa halmashauri hiyo Steven Ulaya kwa mkuu wa mkoa Mrisho Mashaka Gambo, alipofanya ziara ya kukagua maendeleo katika halmashauri hiyo ambapo taarifa hiyo imesema kuwa Mirungi imekuwa ikiingizwa kutoka nchi ya jirani ya Kenya kupitia mpaka wa Namanga.

Ripoti hiyo imeendelea kusema kuwa jeshi la polisi lilefanya operesheni maalum na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu madhara ya madawa hayo,ambapo takwimu za mwaka 2016 hadi januari 2017 kesi za bhangi 11 dhidi ya 8 mwaka 2015 na mirungi ni kesi 12 kwa mwaka 2016 dhidi ya 10

Aidha ripoti hiyo imeonyesha kuwa halmashauri inaendelea na zoezo la uhakiki wa watumishi hewa limewabaini 24 ambapo kiasi cha shilingi 54,798,300 kilihojiwa kwa watumishi hao,kiasi cha shilingi 32,988,963.19 kilirejeshwa hazina baada ya kuzuia mishahara ilitolewa na baadhi ya watumishi walirejesha fedha hizo walionufaika nazo ambapo makato ya mishahara kiasi cha shilingi 21,809,336.81 yaliyokuwa yanalipwa moja kwa moja na wizara ya fedha ikiwa ni kodi ya mishahara ya watumishi husika na makato ya mifuko ya pensheni tayari mfuko umeandikiwa barua za kurejesha fedha hizo .

Sambamba na hayo halmashauri hiyo ina jumla ya watumishi 1,867 sawa na asilimia 71.3 ya mahitaji halisi ya watumishi 2,615,ikiwana upungufu wa watumishi 723 katika mchanganuo ufuatao :Idara ya elimu ya msingi walimu 191,elimu ya sekondari (walimu wa sayansi 54)Mmaendeleoa jamii watumishi 18,Utawala (watendaji wa vijiji na kata 20)Kilimo (watumishi 25)Mifungo (watumishi(21)Afya watumishi 391.

Wilaya ina jumla ya watumishi 295 wa sekta ya Afya ambapo ni sawa na asilimia 43 tu ya mahitaji ya watumishi wote 686,upungufu mkubwa upo katika kada ya Tabibu,wauguzi,wateknolojia ,,mahabara,Dawa na Daktari wasaidizi.

Ripoti hiyo inaonyesha kuwa mapato ya halmashauri hiyo kwa mwaka 2016/2017 imekasimia kukusanya jumla ya shilingi 2,457,310,003 kutoka katika mapato ya ndani hadi kufikia januari 2017,halmashauri iliuwa imekusanya jumla ya shilingi 1,120,7147,542.32 sawa na 46% makisio ya mwaka mzima.

Ikumbukwe kuwa Wilaya ya Monduli miezi ya hivi karibuni ilipatwa na matukio 4 kuungua moto kwa badhi ya mabweni na shule za sekondari 1.Lowassa Sekondari tarehe 27/01/2016 na 31/7/2016,Nanja Sekondari tarehe 2/8/2016 na Ole Sokoine Sekondari tarehe 11/8/2016 ambapo matukio haya ya moto yalileta athari kubwa kwa jamii ikiwemo baadhi ya wanafunzi kurejeshwa majumbani kwa muda kwa mahitaji ya shule .

No comments: