Sunday, February 05, 2017

Dk.Shei awaandalia chakula Maaskari walioshiriki Gwaride la Maadhimisho ya Miaka 53 ya Mapinduzi


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akiwapungia mkono maaskari walioshiriki katika sherehe za Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar wakati alipowasili katika  hafla ya chakula maalum kwa Askari hao iliyofanyika leo katika viwanja vya Kambi ya KVZ Mtoni (kulia) Brigedia Jeneral Sharif Sheikh Othman ,Kamanda wa Brigedi ya Nyuki Zanzibar
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa na Viongozi mbali mbali wakisimama wakati Wimbo wa Taifa ukipigwa wakati wa hafla ya chakula maalum kwa maaskari walioshiriki katika sherehe za Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar mara baada ya kuwasili katika   hafla hiyo  iliyofanyika katika viwanja vya Kambi ya KVZ Mtoni
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akiteta jambo na  Kamanda wa Brigedia ya Nyuki Zanzibar Brigedia Jeneral Sharif Sheikh Othman  wakati wa hafla ya chakula maalum kwa maaskari walioshiriki katika sherehe za Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar mara baada ya kuwasili katika   hafla hiyo  iliyofanyika katika viwanja vya Kambi ya KVZ Mtoni
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi, (wa pili kushoto) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Haji Omar Kheir,(kushoto) Spika wa Baraza la Wawakilishi  Zubeir Ali Maulid na  Kamanda wa Brigedia ya Nyuki Zanzibar Brigedia Jeneral Sharif Sheikh Othman (wa pili kulia)  wakiwa katika   hafla ya chakula maalum kwa maaskari walioshiriki katika sherehe za Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,hafla hiyo  iliyofanyika leo katika viwanja vya Kambi ya KVZ Mtoni
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akichukua chakula wakati wa hafla ya chakula maalum iliyoandaliwa kwa maaskari walioshiriki katika sherehe za Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,iliyofanyika katika viwanja vya Kambi ya KVZ Mtoni Zanzibar
 Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi, (wa pili kushoto) na   Kamanda wa Brigedia ya Nyuki Zanzibar Brigedia Jeneral Sharif Sheikh Othman (wa pili kulia)  wakichukua chakula katika   hafla maalum kwa maaskari walioshiriki katika sherehe za Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, hafla hiyo  iliyofanyika katika viwanja vya Kambi ya KVZ Mtoni
 Maaskari wa vikozi vya ulinzi walioshiriki sherehe za Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,wakichukua chakula cha mchana kilichotayarishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika viwanja vya  Kambi ya KVZ Mtoni Zanzibar
 Maaskari wa vikozi vya ulinzi walioshiriki sherehe za Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,wakichukua chakula cha mchana kilichotayarishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika viwanja vya  Kambi ya KVZ Mtoni Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akiagana na Brigedia Jeneral Sharif Sheikh Othman,Kamanda wa Brigedi ya Nyuki Zanzibar baada ya hafla ya Chakula  maalum aliyoiandaa kwa maaskari walioshiriki katika sherehe za Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,Sherehe iliyofanyika katika kambi ya KVZ Mtoni Mkoa wa Magharibi Unguja. Picha na Ikulu. 





STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE

Zanzibar                                                         4.2.2017
RAIS wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein leo ameungana na Wakuu wa vikosi vya Ulinzi na Usalama wa SMT na SMZ pamoja na Maafisa na Askari katika hafla maalum ya chakala alichowaandalia kutokana na ushiriki wao katika gwaride la kutimia miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Januari 12, 1964. 
Hafla hiyo ilifanyika huko katika viwanja vya Makao Makuu ya KVZ  Mtoni mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, Haji Omar Kheir, na Vikosi wa na viongozi wengine. 
Akitoa neno la shukurani mara baada ya chakula hicho kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Issa Haji  Ussi Gavu alitoa pongezi na shukurani kwa wapiganaji hao kwa ushiriki wao mzuri katika sherehe za kutimiza miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. 
Katika maelezo yake, Waziri Gavu alisema kuwa Mapinduzi ndio yaliyowapa  uhuru wa kujitawala na kuendesha mambo yao wananchi wote wa Zanzibar, hivyo yataendelea kuenziwa, kutunzwa na kuthaminiwa kwa nguvu zote. 
Waziri Gavu aliendelea kutoa neno la shukurani kwa kueleza namna vikosi hivyo vilivyopamba sherehe hizo za miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa gwaride mwanana sambamba na nidhamu ya hali ya juu na kusisitiza kuwa mafanikio hayo yatakuwa ni muendelezo kwa sherehe za miaka ijayo. 
Aidha, Waziri Gavu alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendela kusimamia umoja, mshikamano pamoja na amani na utulivu kwa wananchi wote wa Zanzibar kwani ndio rasilimali pekee inayoweza kusukuma mbele maendeleo ya Zanzibar. 
Mapema Brigedia Jenerali Sharif Sheikh Othman alitoa neno la shukurani kwa niaba ya wapiganaji wote kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Barza la Mapinduzi na kuipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa jinsi inavyowajali na kuwathamini walinzi wake kwa kuwaandalia chakula hicho kutokana na ushiriki wao wa sherehe za kutimiza miaka 53 ya Mapinduzi ya Matukufu ya Zanzibar. 
Alisema kuwa mkusanyiko huo ni muhimu sana kwani unatoa fursa ya askari na wapiganaji wote kupata kubadilishana mawazo sambamba na kutathmini gwaride lililopita na kujipanga vyema kwa gwaride lijalo la mwaka 2018 la kutimiza miaka 54 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar jambo ambalo ni muhimu hasa kwa vikosi hivyo. 
Brigedia Generali Othman ambaye piandie Msimamizi Mkuu wa Gwaride hilo lililopita alieleza kuwa vikosi vya Ulinzi na Usalama vya SMT na SMZ vitaendelea kushirikiana zaidi na Serikali ikiwa ni pamoja na kushauriana na kusisitiza kuwa mda wote wako tayari kupokea maelekezo ikiwa ni pamoja na kufanya tahmini ya gwaride la sherehe za kutimiza miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar zijazo.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 
 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

No comments: