Monday, February 27, 2017

BODI YA SHIRIKA LA POSTA YAWAPIGA CHINI VIONGOZI 2 WAANDAMIZI NA KUWASIMAMISHA 2

1
Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Fortunatus Kapinga, akizungumza wakati akimkaribisha Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika hilo, Dk. Haruni Kondo (katikati), kuzungumza na waandishi wa habari, Makao Makuu ya shirika, Dar es Salaam jana. Kulia ni Kaimu Katibu wa shirika hilo, Zuhura Pinde.
2
Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Fortunatus Kapinga, akizungumza wakati akimkaribisha Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika hilo, Dk. Haruni Kondo (katikati), kuzungumza na waandishi wa habari, Makao Makuu ya shirika, Dar es Salaam jana. Kulia ni Kaimu Katibu wa shirika hilo, Zuhura Pinde.
3
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania. Dk. Haruni Kondo, akizungumza na waandishi wa habari, waki wa mkutano huo. Kushoto ni Postamasta Mkuu, Fortunatus Kapinga.
4
Mmoja wa wafanyakazi walioteuliwa na Bodi ya Shirika hilo kukaimu moja ya nafasi zilizowazi ya Meneja Mkuu Menejimenti ya Rasilimali za Shirika, Macrice Mbodo (kuli), akiwa katika mkutano huo. Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Usalama ya shirika hilo, George Mwamgabe. 
5
Baadhi ya viongozi wa Shirika la Posta Tanzania wakiwa katika mkutano huo.
67
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kazini wakichukua taarifa hiyo, iliyokuwa ikitolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania, Dk. Haruni Kondo. 
 (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI MKUTANO ULIFANYIKA KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO WA POSTA HOUSE
TAREHE 25 FEBRUARI, 2017
Kwa kuzingatia maendeleo ya mageuzi makubwa yanayojitokeza katika sekta ya mawasiliano, Shirika la Posta Tanzania kama mtoa huduma kwa umma (Public Postal Operator), linawajibika kuhakikisha kuwa huduma za kisasa zinazozingatia vigezo vya ubora, usalama, uadilifu katika utendaji na uwajibikaji zinawafikia watu wengi zaidi katika maeneo yote ya nchi.
Kwa hivi sasa Bodi ya Wakurugenzi pamoja na Menejimenti imechukua hatua katika maeneo yafuatayo:-
1)   KUPAMBANA NA UHALIFU WA MADAWA YA KULEVYA.
Shirika la Posta Tanzania limechukua hatua kadhaa ili kuhakikisha linashiriki na kuchangia kikamilifu jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano za kupambana na uhalifu, ikiwa ni pamoja na usafirishaji, uuzaji na utumiaji wa madawa ya kulevya, usafirishaji na utakatishaji wa fedha haramu, ugaidi, udanganyifu katika utambulisho pamoja na uhalifu mwingine wa kimtandao wa Kitaifa na Kimataifa.
Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika imedhamiria kuongeza msukumo na kasi ya usimamizi ili kupambana na uhalifu huu ambao una madhara makubwa kwa jamii.
Post a Comment