Wednesday, December 01, 2010

Kumbe mgomo wa Ustawi wa jamii ni kanyaboya


SERIKALI ya wanafunzi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii imesitisha mgomo wao mara tu baada ya raisi wa chuo hicho kuitwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda ofisini kwake na kumuahidi kushughulikia matatizo ya chuo hicho ndani ya wiki moja.

Hata hivyo habari tulizozipata kutoka katika chanzo chetu cha habari zinaeleza kuwa tatizo la chuo hicho linasabababishwa na mpasuko uliopo ndani ya uongozi wa chuo kwa kudai kuwa na makundi mawili mbayo yanavutana ili kuharibiana sifa.

“Hapa chanzo cha tatizo ni Baraza la Usajili wa vyuo vya Ufundi ya kati(NACTE) ambayo ilileta muongozo na sifa zinazotakiwa kwa baadhi ya watu wanaotakiwa kuwa ndani ya uongozi wa chuo,” kilisema chanzo hicho.
Kilisema kuna watu ambao wapo katika nafasi nyeti za uongozi wa chuo na hawana sifa zilizotajwa na NACTE ivyo basi wameamua kutumia wanafunzi ili waweze kukamilisha lengo lao.
“Wanafunzi wanatumiwa kama chambo tu lakini wao hawajui chuki imejengwa na watu kutoka juu na mtu huwezi kulazimisha kukaa mahali wakati huna sifa za kuwa na cheo kuwa na mdaraka serikalini sio sababu ya kuweka mizigo katika sekta muhimu kama hizi,” kilisema chanzo hicho.
Hata ivyo raisi wa serikali ya wanafunzi ya chuo hicho jana aliitwa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii ili kuweza kupata ufumbuzi wa tatizo lao.

No comments: