Sunday, November 07, 2010

Rais Kikwete aapishwa aanza ngwe




RAIS Jakaya Kikwete jana aliapishwa kuiongoza Tanzania kwa kingine cha miaka mitano ijayo na kutoa wito kwa vyama vya upinzani kushirikiana na serikali yake katika kuimarisha demokrasia na kudumisha amani nchini.
Akitoa hotuba yake ya kwanza baada ya kuapishwa na Jaji Mkuu Augustino Ramadhan katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam jana, Rais Kikwete ambaye alipata ushindi wa asilimia 61.17 ambayo ni chini zaidi ya ushindi aliopata mwaka 2005, alisema wapinzani waliifanya CCM kujituma zaidi na mahali pengine kulazimika kufanya kazi ya ziada wakati wa kusaka ushindi.
"Siwezi kuacha kuwatambua wagombea wenzangu sita tuliowania nafasi ya uongozi wa juu kabisa wa nchi yetu, nawashukuru kwa kutuchangamsha wakati wa kampeni, mmetufanya tujitume zaidi na mahali pengine tufanye kazi ya ziada.

2 comments:

emu-three said...

Sasa mpaka umeshawekwa, wale waliokuwa wanataka kumbusu mkono, ku...' hakuna tena, ukitaka rungu la dola likushukie, ujaribu kumkaribia sasa.
Sawa yote hayo ndio wanaita `protokali' cha muhimu ni kutekeleza ahadi, lieni na ahadi kila mkikutana na viongozi hawa waliochaguliwa, wimbo' `tekelezeni ahadi mlizoahidi..'

zitto-kiaratu said...

hata sielewi haja ya vyama upinzani, kama alikuwa anajua ataiba kura za wananchi, hii picha inavunja mbavu.