Wednesday, November 03, 2010

Nyalandu aibuka na ushindi mnono



MBUNGE wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu ameweza tena kurejea madarakani baada ya kuibuka na jumla ya kura 46,869 ikiwa ni asilimia 91 ya kura zote.

Nyalandu ambaye amekuwa mgombea ubunge wakwanza nchini kutumia helkopta katika kampeni aliwabwaga wapinzani wake Msaghaa Kimia kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) alipata kura 3,544 wakati Sizimwe Kanyota wa Chama cha Wananchi (CUF) aliyepata kura 550.

Akitangaza matokeo hayo usiku wa jana, Msimamizi wa uchaguzi katika jimbo hilo, Iliminata Mwenda alisema jumla ya wapigakura waliojiandikisha walikuwa 90,045 wakati waliopiga kura ni 46,869 katika jimbo hilo.

Akizungumza baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo, Nyalandu alisema kuwa wananchi wa Singida Kaskazini wamempa heshima kubwa kwa kuonyesha kumwamini na kuwa yuko tayari kuendeleza mambo aliyoyafanya kipindi kilichopita na kutimiza ahadi zake alizotoa wakati wa kampeni.

No comments:

RUZUKU YA SH.MILIONI 250 YATOLEWA KWA WABUNIFU WA MATUMIZI BORA YA NISHATI

📌 Kamishna wa Umeme asema Serikali itaendelea kuwawezesha vijana wabunifu katika teknolojia ya matumizi bora ya nishati 📌 Wabunifu wa kike...