Tuesday, September 04, 2007

Wabongo si mchezo





Hebu cheki shughuli iliyofanywa na washabiki wa mechi ya juzi. Siyo kwamba haujaisha umebomolewa uwanja wetu.


KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida ikiwa ndio siku ya kwanza tu kutumika kwa Uwanja Mkuu wa Taifa wa Tanzania (uwanja mpya) uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu, mashabiki wameng'oa viti pamoja na baadhi ya koki za mabomba ya maji chooni.
Mechi ya kwanza kwenye uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 60,000 waliokaa vitini ilichezwa Jumamosi iliyopita baina ya Taifa Stars na Uganda na ilihudhuriwa na watazamaji wanaozidi 50,000 ambato ni kubwa kutokanana mechi kuwa ya kirafiki.
Baada ya mechi hiyo imegundulika kuwa baadhi ya viti vya rangi ya bluu vimeng'olewa na baadhi ya koki za mabomba chooni pia ziling'olewa.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Msimamizi Mkuu na Mtaalamu wa Ujenzi katika uwanja huo, Alloyce Mushi alisema jana walitarajia kufanya tathimini na kesho watakamilisha ukarabati huo ambao umeshaanza.
Mafundi waliongea uwanjani hapo, walidai vitu vingi vimeharibika kutokana na wingi wa mashabiki kutokujua jinsi ya kutumia vifaa vilivyopo ndani ya uwanja huo ikiwa ni pamoja na kupanda juu ya viti wakati wa kushangilia.
Baadhi ya mafundi hao walisema viti vya kukunja na kufungua ndiyo vina uimara zaidi kuliko vile ambavyo vimefungwa juu ya bomba moja.
Viti vilivyong'oka ni vya upande wa Mashariki na Magharibi ya uwanja huo baadhi vikiwa ni karibu na jukwaa la VIP.
Uwanja huo ambao bado haujafunguliwa rasmi utatumika tena katika mechi ya kuwania kufuzu kucheza fainali za Mataifa ya Afrika Jumamosi baina ya Taifa Stars na Msumbiji.

1 comment:

Anonymous said...

JAMANI KUNA MSEMO KUWA KANIKI WEUSI NI RANGI YAKE USIMLAUMU DOBI ! HIVYO VITI VIMEVUNJIKA TOKANA NA KUKOSA UIMARA KTK HIYO STEPPED CONCRETE AMBAYO NATUMAI ILIPIGWA PLASTER YENYE UNENE MKUBWA SANA NA KUIACHA CONCRETE KUWA MBALI NA KUNA EXPANSION BOLT AMBAZO NDIO HUFUNGWA KUSHIKILIA HIZO SEAT SASA KAMA SIZE YA BOLT ITAKUWA AIJAIINGIA SAWASAWA KWENYE CONCRETE UNATEGEMEA NINI ? AIWEZI KUSTAAHAMILI UZITO WA MTU HAPO ITAKUWA IMESHIKA KWENYE PLASTER NA HILO NINI TATIZO LA WAJENZI WA UWANJA HIYO NI SUBSTANDARD BWANA ! NA LAZIMA TUFAHAMU KUWA HIVYO VII VIMEBUNIWA VIWEZE KUBEBA UZITO MKUBWA WA WANADAMU NA MISUKOSUKO YOTE YA USHANGILIAJI SASA LEO TU KTK MECHI MOJA VINAVUNJIKA BASI NI BALAA INABIDI KUFANYIKE UKAGUZI WA KUTOSHA JUU YA VIFAA TUTAKAVYOFUNGIWA NA WAJENZI WA UWANJA.WATU KUVUNJA VITI BASI LAZIMA WANGEINGIA NA ZANA NZITO NA SI KWA KUKALIA TU .

"Usimlaumu dobi kaniki weusi ni rangi yake"

Mzushi