RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni  Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jakaya Mrisho Kikwete amewapandisha vyeo Maafisa wa jeshi la Polisi  katika ngazi za Manaibu Kamishna na Makamishna Wasaidizi Waandamizi.
   
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamishna Msaidizi wa Polisi, Essaka Mugassa, rais amewapandisha vyeo Makamishna Wasaidizi Waandamizi   Peter Kivuyo wa Makao Makuu ya Upelelezi Dar es salaam, Nestory Mpembela  ambaye ni Mkuu wa
Idara ya Mawasiliano Makao Makuu   na Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma Omary Rashid Mganga   kuwa Manaibu Kamishna.
   
Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama amewapandisha vyeo Makamishna Wasaidizi kumi na nane kuwa Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Jeshi la Polisi Ambao ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara , Luther Mbutu; Kamanda wa Polisi mkoa wa Kaskazini Unguja , Mselemu Masud Mtulia; Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Zelothe Stephen; na Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya Seleman  Hussein Kova.
   
Wengine ni Antony Joel Mwami ambaye ni Mkuu wa  Kikosi cha  Polisi Anga; Neven
Isaack Mashayo Mkuu wa Chuo cha Polisi Zanzibar; Juma Omary Kondia ambaye ni mkuu
wa mawasiliano Kanda Maalum ya Dar es Salaam; pamoja na Bw Kenneth Kasseke na
Faraji Kayuga wa Makao Makuu ya Polisi Zanzibar
   
 Waliopanda vyeo na kuwa Makamishna Wasaidizi Waandamizi wengine ni Mkuu wa
Mawasiliano Msaidizi Makao Makuu Abdul Issa Nina; Mkuu wa kitengo cha Maendeleo
cha Jeshi la Polisi Zuhura Munisi, Boniface Kanyunya Mpaze na John Kimario wa
Makao Makuu ya upelelezi Dsm.
   
Wengine ni kutoka Makao Makuu ya Polisi Dsm ambao ni Alexander Calist Mushi, Bw.
Rashid Ally Omar, Bw, Aswegen Wilson Magambo Bw Issaya Juma Mngulu na Mkuu wa
kikosi cha Bendi Makao Makuu, Mbazi  Yohana Mchomvu. Mheshimiwa Rais amewapandisha vyeo maafisa hawa wa Jeshi la Polisi   kuanzia Agosti  31, 2007
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
RAIS DKT. SAMIA AKUTANA NA UJUMBE WA JUKWAA LA MABUNGE LA NCHI ZA MAZIWA MAKUU (FP-ICGLR) IKULU NDOGO TUNGUU, ZANZIBAR
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Kiongozi wa Jukwaa la Mabunge la...
 
- 
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu na timu ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwa katika ...
- 
Mwanamuziki toka Jamhuri ya KIdemokrasia ya Kongo, Mbilia Bel akitumbuiza katika viwanja vya bunge mjini Dodoma jana. Picha na Jube Tranquil...
- 
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2014 EXAMINATION RESULTS ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA ...
 
No comments:
Post a Comment