Friday, October 30, 2015

KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA BAN KI MOON AIPONGEZA TANZANIA Salam

Salamu za pongezi kitaifa na kimataifa zaanza kutolewa kwa Rais mteule wa awamu ya tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Taifa la Tanzania.
Mapema leo baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kumaliza hafla ya kumkabidhi Rais mteule cheti chaushindi katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Jijini Dar es Salaam.Tanzania ilianza pokea salamu za pongezi toka kwa Katibu Mkuu wa umoja wa mataifa (UN) Ban Ki -Moon liyetuma salamu zake za pongezi.
Pia, aipongeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuratibu na kusimamia vyema zoezi zima la Uchaguzi, ukusanyaji matokeo ya Uchaguzi kutoka katika vituo mbalimbali, ujumlishaji matokeo kusanywa, pamoja na usomaji matokeo hayo uliokuwa wa wazi, huru na haki.
Hata hivyo katika nyongeza yake, aelezea "concern" yake juu ya zoezi la Uchaguzi Zanzibar.

Soma Hapa:

MAGUFULI AKABIDHIWA HATI YA USHINDI NAFASI YA URAIS

Rais mteule wa Tanzania John Pombe Magufuli akionesha cheti chake cha ushindi alichokabidhiwa muda huu katika ukumbi wa Diamond Jubilee



Na Anitha Jonas na Beatrice Lyimo- MAELEZO.
 
Watanzania wametakiwa kukubaliana na matokeo ya  Uchaguzi Mkuu  wa mwaka 2015, yaliyotangazwa na Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC) kwa kuwa  ni ya haki na hakuna aliyeibiwa kura.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Waangalizi wa Uchaguzi kutoka nchi za Jumuiya ya Madola nchini na ambaye Rais Mstaafu wa Nigeria, Goodlucky Jonathan kwenye halfa ya kumkabidhi hati Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM) iliyofanyika  leo kwenye ukumbi wa Diamond  Jubilee  jijini Dar es salaam.

“Uchaguzi ulikuwa wa haki na amani na hakuna yeyote aliyeibiwa haki yake kwani matokeo hayo yamedhibitishwa kuwa ya uhuru na haki kwa kufuata misingi ya sheria na taratibu zilizopo” alisema  Rais Mstaafu Jonathan.

Kwa upande wa mgombea urais kupitia chama cha ACT wazalendo Bibi. Anna Mghwira amesema kuwa chama chake kimemkubali matokeo ya uchaguzi uliompitisha Dkt. John Magufuli.

Vilevile ameongeza kuwa wagombea wote walizungumza kuhusu mabadiliko hivyo ana imani na mshindi wa nafasi hii atalisimamia ipasavyo.

“Watanzania wanahitaji mabadiliko hasa katika Katiba Mpya itakayotokana na maoni ya Watanzania, kuimarisha umoja wa kimataifa, kuinua uchumi wa nchi, kusimamia shughuli za Serikali pamoja na kuboresha usawa wa kijinsia kati ya mwanamke na mwanamume,” aliongeza Bibi Mghwira.

Mbali na hayo mgombea huyo wa urais kupitia chama cha ACT wazalendo amemkabidhi Rais Mteule Ilani ya chama hicho kama muongozo kwa yale yaliyopungua katika Ilani ya cha chake.

Aidha Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) Jaji Mstaafu Damian Lubuva amewapongeza wananchi kwa kuwa na mwamko mkubwa wa kupiga kura na kuliendesha zoezi hilo kwa amani.

Pia Jaji Mstaafu Lubuva alimkabidhi hati ya ushindi mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi.

HAFLA YA KUKABIDHI CHETI CHA MSHINDI WA URAIS 2015


 

Kutangazwa rasmi mshindi wa urais 2015 kutokaa ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar Es Salaam;   
 Washiriki wa mbio za urais wa vyama vya siasa pamoja na viongozi mbalimbali katika hafla za kutangazwa mshindi wa urais 2015;Hafla 
MKurugenzi wa NEC Ramadhan Kailima akitoa tathmini ya mchakato  wa uchaguzi mkuu mwaka  2015;https://youtu.be/Lg8d2m1YwgE 
STAR TV: Mwenyekiti wa NEC Jaji Damian Lubuva akitoa taarifa za matokeo ya uchaguzi 2015 katika hafla ya kutangazwa mshindi wa urais 2015; https://youtu.be/b-RaifbfLy0
 DR.John Pombe Magufuli  na Samia Suluhu  wa CCM wakipokea chati cha ushindi wa urais na makamu wa urais wa Tanzania 2015; https://youtu.be/i15KeuGkv3Y 
  Anna Mghwira -ACT-Wazalendo aeleza matarajio ya Watanzania kwa uongozi wa Dr.Magufuli ikiwemo katiba ya mpya, usawa, uchumi na kudumisha amani  ya nchi huku akimkabidhi ilani ya chama chake ;https://youtu.be/pJet8rttF8U
Viongozi mbalimbali wakishiriki kupiga picha za kumbukumbu wakati wa hafla ya kukabidhi washindi wa wagombea urais vyeti; https://youtu.be/nGT8lWgs504

RAMANI YA TANZANIA KUONYESHA MAENEO VYAMA VILIKOPATA KURA NYINGI



GLOBAL EDUCATION LINK (GEL) YAPELEKA WANAFUNZI 65 KUSOMA VYUO VIKUU NCHINI CHINA

 Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Global Education Link (GEL), Abdulmalik Mollel akiwa ameambatana na wafanyakazi wa kampuni hiyo kwa ajili ya kuwasindikiza wanafunzi wanaokwenda kusoma vyuo vikuu nchini China mapema jana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Global education link (GEL) Abdulmalik Mollel akiwaita majina wanafunzi wanaokwenda kusoma vyuo vikuu nchini China mapema jana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mfanyakazi wa Global link education (GEL) wakiwakagua wanafunzi viambatanisho vyao muhimu ikiwemo viza, vyeti, na passport.
 Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Global Education Link (GEL), Abdulmalik Mollel akibadilishana mawazo na wazazi mara baada ya kuwasili katika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Mwanafunzi akifurahia jambo na wazazi wake.
Wanafunzi wakiingia sehemu ya kwenda kukaguliwa tayari kwa safari.
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Global Education Link (GEL), Abdulmalik Mollel akiambatana na wanafunzi kuelekea sehemu ya ukaguzi.
Wanafunzi wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukamilisha zoezi muhimu

UN TANZANIA STATEMENT ON TANZANIA GENERAL ELECTIONS

IMG_5569UN Resident Coordinator, Alvaro Rodriguez.
Dar es Salaam, 29 October 2015: The United Nations is following very closely the Tanzanian general elections of 25 October and congratulates the president elect. We congratulate Tanzanians for exercising their democratic rights in a peaceful manner. We take note of the international observers statement (Commonwealth, AU, SADC and EU) of today that indicates they are pleased that the voting and counting took place in an environment of peace.
However, the observer missions as well as the US Embassy and UK High Commission have also shared their great concern with the statement issued by the Chairman of the Zanzibar Electoral Commission in which he nullified the Zanzibar elections.
We call on political leaders to promote an environment of peaceful dialogue to resolve their differences and to ensure a continued peaceful and democratic elections process. It is through this peaceful and democratic process that the social and economic development of the United Republic of Tanzania can be ensured.
SIGNED BY: ALVARO RODRIGUEZ
UN RESIDENT COORDINATOR

Thursday, October 29, 2015

SAFU MPYA YA MAKATIBU NA NAIBU MAKATIBU WAKUU NISHATI NA MADINI YAKABIDHIWA OFISI

ch1

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi (kulia), akibadilishana Nyaraka za Makabidhiano na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omari Chambo (Kushoto). Maswi ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara.
ch2
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omari Chambo (Kushoto), akisaini Nyaraka za Makabidhiano sambamba na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Manyara.
ch6

ch5
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Paul Masanja (kulia) akipokea shada la maua kutoka kwa Cecilia Mrope Afisa kutoka Wizara ya Nishati na Madini.
ch4
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omari Chambo, akiongea jambo na Wajumbe wa Menejimnenti wa Wizara baada ya kuwasili wizarani hapo. Katibu Mkuu alitumia kikaohicho kuwaeleza wajumbe masuala muhimu ambayo atayasimamia kikamilifu katika sekta za Nishati na Madini.
ch3



Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi akimpongeza, aliyekuwa Kamishna wa Madini Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi
…………………………………………………………………………….
  • Makatibu wapya wataja vipaumbele
  • Kuzingatia 4Us, Uendelezaji Wachimbaji Wadogo
Teresia Mhagama na Asteria Muhozya
Katibu Mkuu mpya na Naibu Katibu Mkuu  walioteuliwa kuiongoza Wizara ya Nishati na Madini wameanza majukumu yao na kusisitiza watumishi wa Wizara na Taasisi zake kuzingatia Uadilifu, Ubunifu, Uwajibikaji, na Uwazi katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Wakizungumza  na wajumbe  wa menejimenti ya Wizara ya Nishati na Madini, viongozi hao walisisitiza  baadhi ya masuala yatakuwa  kipaumbele  kuwa ni uwepo wa umeme wa uhakika na bei nafuu ili wananchi watumie nishati hiyo kujiletea maendeleo na kukuza uchumi wa nchi.
Vipaumbele vingine ni kuongeza mchango wa sekta madini katika pato la Taifa, uwepo wa kiwanda cha kusindika gesi asilia, na suala la uwezeshaji wazawa(Local Content) katika sekta za Nishati na Madini.
Vilevile, vipaumbele vingine ni kuhakikisha kuwa wachimbaji wadogo wanasaidiwa katika masuala ya fedha na utaalam na kuboresha mazingira na maslahi ya wafanyakazi.
Katibu Mkuu, Mhandisi Omari Chambo, pamoja na kumshukuru aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi kwa kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa, alitoa wito wa ushirikiano kati ya uongozi huo mpya na wafanyakazi.
Naye, Naibu Katibu Mkuu, Mhandisi Paul Masanja pamoja na kuainisha vipaumbele mbalimbali  vya utekelezaji amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete kwa kumteua kushika nafasi hiyo   na kueleza kuwa, imetokana na kuridhika na utendaji wake wa kazi wakati aliposhika nyadhifa mbalimbali ikiwemo kuwa Kamishna wa Madini nchini.
Alitoa wito kwa wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Madini kutoa ushirikiano kwa uongozi huo ili kwa pamoja waweze kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazojitokeza katka uendelezaji wa sekta za Nishati na Madini.
Kabla ya kukabidhi nyaraka za makabidhiano, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Nishati na Madini, Eliakim Maswi  ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara, aliwashukuru watumishi wa Wizara ya Nishati na Madini kwa ushirikiano waliompa wakati wa kipindi cha uongozi wake na kuwaasa kufanya kazi kwa bidii na kutoa ushirikiano kwa uongozi mpya.
Vilevile, aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Mhandisi Ngosi Mwihava ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, aliwaasa Watumishi kuendelea kufanya kazi kwa kushirikiana, kuzingatia taratibu, sheria na kanuni, kuzingatia muda na kuimarisha mawasiliano.
Kabla ya kushika nyadhifa hizi Katibu Mkuu, Mhandisi Omari Chambo alikuwa Katibu Tawala mkoa wa Manyara na Naibu Katibu Mkuu, Mhandisi Paul Masanja alikuwa Kamishna wa Madini nchini.

WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU AMPONGEZA NDEJEMBI, AMSIFIA KWA UADILIFU NA UCHAPAKAZI

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba , amempongeza Mhe. Deogratius John Ndejembi kwa kuaminiwa ...