Monday, August 24, 2026

TRC KUONGEZA SAFARI ZA SGR DAR ES SALAAM–DODOMA 🚆🇹🇿

 


Habari njema kwa wasafiri! Shirika la Reli Tanzania (TRC) limetangaza kuongeza safari za treni ya SGR kati ya Dar es Salaam na Dodoma kuanzia Septemba 1, 2026.

Kuongezeka kwa safari kunatarajiwa kutoa nafasi zaidi kwa abiria, kuongeza urahisi wa usafiri na kuimarisha zaidi muunganiko kati ya Dar es Salaam na Dodoma.

Hatua hii ni mwendelezo wa matumizi ya miundombinu ya kisasa ya reli katika kurahisisha usafiri wa wananchi na kuchochea shughuli za kiuchumi.

🚆 Safari zaidi. Urahisi zaidi. Muunganiko zaidi.

#TRC #SGR #DarEsSalaam #Dodoma #Usafiri #Miundombinu #Maendeleo #Tanzania

No comments:

SERIKALI YATAKA MAKAZI YAENDANE NA KASI YA UKUAJI WA MIJI

  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Leonard Akwilapo,akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Makazi Duniani 2026 yal...