Monday, August 03, 2026

WAZIRI KIJAJI AKUNA NAZI NANENANE 2026



Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, ametembelea Banda la Makumbusho ya Taifa la Tanzania katika Maonesho ya Nanenane 2026 jijini Dodoma na kushiriki shughuli ya jadi ya kukuna nazi—ishara ya kuenzi, kuhifadhi na kutangaza urithi wa utamaduni wa Mtanzania.

Mhe. Dkt. Kijaji ameeleza kuwa Maonesho ya Nanenane ni jukwaa muhimu la kutangaza vivutio vya utalii, kuimarisha ushirikiano na wadau na kuunga mkono jitihada za Serikali za kufikia lengo la kuvutia watalii milioni nane ifikapo mwaka 2030.

#Nanenane2026 #MakumbushoYaTaifa #UrithiWetu #UtaliiTanzania

No comments:

NIRC YAFUNGUA SURA MPYA YA KILIMO: MIRADI 30, PAMPU 2,000 NA AJIRA 4,000

  Na Mwandishi Wetu, Dodoma Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) inatarajia kuanza utekelezaji wa miradi mipya zaidi ya 30 ...