Sunday, November 25, 2012

Jiwe la msingi Ilembo NHC Mpanda

 Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Mchechu akiwa sambamba na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck Ole Medeye wakikagua mojawapo ya nyumba za mradi wa nyumba za gharama nafuu za NHC Ilembo, Mpanda Katavi jana
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mkurugenzi wa Utawala na Uendeshaji wa Mikoa, Raymond Mndolwa huku Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Mchechu na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck Ole Medeye wakishuhudia kwenye uzinduzi wa nyumba za gharama nafuu za NHC Ilembo, Mpanda Katavi jana
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk mohammed Gharib Bilal, akizindua ujenzi wa nyumba za gharama nafuu NHC Ilembo huku Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Mchechu na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck Ole Medeye wakishuhudia kwenye uzinduzi wa nyumba za gharama nafuu za NHC Ilembo, Mpanda Katavi jana
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk mohammed Gharib Bilal, akizindua ujenzi wa nyumba za gharama nafuu NHC Ilembo huku Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Mchechu na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck Ole Medeye wakishuhudia kwenye uzinduzi wa nyumba za gharama nafuu za NHC Ilembo, Mpanda Katavi jana

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk mohammed Gharib Bilal, akipeana mkono na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck Ole Medeye  kwenye uzinduzi wa nyumba za gharama nafuu za NHC Ilembo, Mpanda Katavi jana. Picha zote za kwa hisani ya SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA

Saturday, November 24, 2012

DKT GHARIB BILAL AZINDUA UWANJA NDEGE WA MPANDA NA KONGAMANO LA TATHMINI YA UWEKEZAJI UKANDA WA ZIWA TANGANYIKA

 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. Gharib Bilal na Mkewe mama Aisha Bilal wakishuka kwebye ndege mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda mkoani Katavi kwa ajili ya uzinduzi wa mkoa mpya wa Katavi unaofanyika mjini mpanda kesho, Makamu wa Rais pia amezinddua uwanja wa ndege wa Mpanda na kuzindua Kongamano la Tathimini ya Mkutano wa Uwekezaji Ukanda wa Ziwa Tanganyika  uliofanyika Oktoba 17 mwaka jana na kushirikisha mikoa mitatu ya Rukwa, Kigoma a kufanyika mjini mpanda ambapo  sasyamekuwa makao makuu ya Mkoa wa Katavi.
 
Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal akisalimiana na Waziri Mkuu Mizengo Pinda mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda, kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rutengwe na katikati ni mama Tunu Pinda.
Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal kushoto akijadiliana jambo na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati wa Kongamano la kutathmini Mafanikio na Changamoto baada ya mkutano wa Uwekezaji wa Ukanda wa Ziwa Tanganyika Kigoma na Rukwa uliofanyika Oktoba 17 mwaka jana mjini Mpanda
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akizungumza katika uzinduzi wa Uwanja wa ndege wa Mpanda, kshoto ni Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal na kulia ni mama Zakia Bilal.
 
Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal akizungumza wakati wa uzinduzi wa  uwanja wa ndege wa Mpanda mkoani Katavi leo mchana.
 
Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi Mhandisi Omar Chambo akitoa taarifa ya ujenzi wa uwanja huo kwa Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal wakati wa uzinduzi mjini mpanda leo.
 
Naibu Waziri wa Uchukuzi Dkt. Charles Tizeba akimkaribisha Makamu wa Rais ili kuongea na wananchi wakati wa uzinduzi wa uwanja huo mjini Mpanda leo
 
Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa uwanja wa ndege wa Mpanda baada  ya kukamilika kwa ujenzi wa uwanja huo, kulia ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Mizengo Pinda na Naibu Waziri wa Uchukuzi Dkt. Charles Tizeba, kushoto ni Mama Zakia Bilal mke wa Makamu wa Rais.

 Kutoka kulia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck Ole Medeye, Dkt. Mary Nagu Waziri wa Uwekezaji na Uwezeshaji Ofisi ya Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda Mke wa Waziri Mkuu na Mama Zakia Gharib Bilal Mke wa Makamu wa Rais wakiwa katika uzinduzi huo 
Makamu wa Rais akisalimiana na Mary Nagu Waziri wa Uwekezaji na Uwekezaji mara baada ya kuwasili mjini Mpanda leo Katikati ni Mwenyekiti wa CCM Katavi Mselem na kutoka kulia ni Mbunge wa Mpanda mjini CHADEMA Mh.Said Arfi na Naibu Waziri wa Uchukuzi Dkt Charles Tizeba.
 
Makamu wa Rais Dkt Gharib Bilal akivishwa skafu na vijana wa chipukizi mjini Mpanda mara baada ya kuwasili mkoani Katavi leo.
 
Makamu wa Rais akisalimiana akipungia mkono wananchi waliofika kumlaki kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda mkoani Katavi leo, kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Katavi Dkt Rajab Rutengwe na kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa Bw. Mselem.
 
Makamu wa Rais Dkt Gharib Bilal na Mkewe Mama Zakia  Bilal wakiangalia ngoma katika uwanja wa ndege wa  Mpanda
 
Mama Tunu Pinda akishiki kuchza ngoma za asili za mkoa wa Katavi kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda wakati wa mapokezi ya Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal.
 
Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba Bw. Nehemia Kyando Mchechu
 
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akifurahia jambo na Mzee Paul Kimiti Waziri Mkuu wa Zamani na Mbunge wa jimbo la Sumbawanga miaka iliyopita kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda
 
Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kibondo Mh. Venance Mwamoto wakati wa mapokezi hayo, kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Rajab Rutengwe.
 
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akimpa ishara ya Dole Mbunge wa Mpanda mjini CHADEMA Mh. Said Arfi, wakati wa mazungumzo yao kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda katika mapokezi ya Makamu Wa  Rais Dkt. Gharib Bilal, Kauli mbiu ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Rajab Rutegwe katika maendeleo mkoani Katavi inasema “SIASA NI MAENDELEO”
 
kutoka kulia ni Mkuu wa mkoa wa Rukwa Injini Stella Manyanya, Mkuu wa mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rutengwe, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Issa Machibya na mwenyekiti wa CCM Mpanda Hamida Mbogo wakizungumza mawili matatu wakati wa mapokezi ya makamu wa Rais mjini Mpanda leo,

Shirika la Nyumba lazindua Ujenzi nyumba za gharama nafuu Katavi

 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja Mawasiliano wa Shirika la Nyumba la Taifa, Yahya Charahani kwenye maonyesho yanayoshirikisha taasisi, asasi na vitengo mbalimbali vya umma na watu binafsi mjini Mpanda jana. Maonyesho hayo ya wiki moja ni sehemu ya uzinduzi rasmi wa mkoa wa Katavi unaofanyika rasmi kesho.
 Ujenzi wa Majengo ya nyumba za gharama nafuu za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Ilembo Mpanda mkoani Katavi yakiwa katika hatua za awali za ujenzi wake ambao baada ya kukamilika zitajengwa nyumba 94 za kuishi kwaajili ya watu wa kipato cha chini.
 Ujenzi wa Majengo ya nyumba za gharama nafuu za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Ilembo Mpanda mkoani Katavi yakiwa katika hatua za awali za ujenzi wake ambao baada ya kukamilika zitajengwa nyumba 94 za kuishi kwaajili ya watu wa kipato cha chini.
Mkurugenzi wa Utawala na Uendeshaji wa Mikoa wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Raymond Mndolwa akieleza jambo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemiah Kyando Mchechu kwenye Ujenzi wa Majengo ya nyumba za gharama nafuu za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Ilembo Mpanda mkoani Katavi yakiwa katika hatua za awali za ujenzi wake ambao baada ya kukamilika zitajengwa nyumba 94 za kuishi kwaajili ya watu wa kipato cha chini.
Meneja wa NHC Mbeya ambaye pia ni Mhandisi Msimamizi wa Mradi wa Ujenzi wa Majengo ya nyumba za gharama nafuu za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Ilembo Mpanda mkoani Katavi, Malissa (kushoto) akizungumza na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya NHC, Geofrey Msella wakati huku Mkurugenzi Mkuu Nehemia Kyando Mchechu (katikati) akisikiliza .

Jiwe la Msingi la nyumba za gharama nafuu za NHC Ilembo, Mpanda mkoani Katavi. (PICHA ZOTE ZA NHC)

Friday, November 23, 2012

MBEKI MGENI RASMI MAJADILIANO YA UONGOZI AFRIKA DAR ES SALAAM

 Rais Mstaafu wa awamu ya pili ya utawala huru wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki (kulia) akifafania jambo wakati wa Majadiliano ya duara kuzungumzia uongozi barani Afrika na changamoto za maendeleo uliofanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa Mdahalo huo ulioandaliwa na Taasisi ya UONGOZI Tanzania, Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa David Msuya. Mbeki alikuwa Mgeni Rasmi katika mdahalo huo.
 Mwenyekiti wa Majadiliano ya duara kuzungumzia uongozi barani Afrika na changamoto za maendeleo, ulioandaliwa na Taasisi ya UONGOZI Tanzania, Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa David Msuya akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mdahalo huo jijini Dar es Salaam.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya UONGOZI, Prof. Joseph Semboja, akizungumza katika mdahalo huo.
 Rais Mstaafu wa awamu ya pili ya utawala huru wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki (kulia) akikiwa mwenye tabasamu wakati Mwenyekiti wa Majadiliano ya duara kuzungumzia uongozi barani Afrika na changamoto za maendeleo ulioandaliwa na Taasisi ya UONGOZI Tanzania, Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa David Msuya akitoa ufafanuzi wa majadiliano.
 waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa David Msuya na Mwenyekiti wa Mdahalo wa Uongozi Afrika, pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya UONGOZI, Prof. Joseph Semboja (katikati) wakimsikiliza Balozi wa kwanza wa Tanzania nchini Afrika Kusini Ami Mpungwe ambaye kwa sasa ni mfanyabiashara na Mwenyekiti wa Tanzanite One muda mfupi kabla ya kuwasili kwa Mgemi rasmi wa Majadiliano ya duara kuzungumzia uongozi barani Afrika na changamoto za maendeleo. 
Mawaziri Wakuu Wastaafu wa Tanzania, Cleo David Msuya (kulia)  na Salim Ahmed Salim wakijadiliana jambo muda mfupi kabla ya kuanza Majadiliano ya duara kuzungumzia uongozi barani Afrika na changamoto za maendeleo.
 
 Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki, (Kulia), akimtania Waziri Mkuu Mstaafu na mwenyekiti wa Tume ya mabadiliko ya katiba ya Tanzania, Joseph Warioba, wakati marafiki hao walipokutana kwenye majadiliano ya duara kuzungumzia uongozi barani Afrika. 
 Waalikwa mbalimbali wakiwa katika chumba cha majadiliano.
 Naibu waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba, akichangia mada katika majadiliano hayo ya Duara. Makamba alizungumzia sana kuhusu masulala ya uchumi.
 Mmoja wa waalikwa akichangia mada
 Mwenyekiti wa Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI) Bw. Felix Mosha akizungumza.
 Meza kuu ikifuatilia kwa ukaribu majadiliano hayo. kutoka kushoto ni Rais Mstaafu wa afrika Kusini, Thabo Mbeki, Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya UONGOZI, Prof. Joseph Semboja na Mdhamini wa taasisi ya Thabo Mbeki, Gloria.
Arnod Kileo nae akichangia mada, kulia ni Prof. Toli Mbwete, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania, ni ofisa kutoka Bank M.
Mwenyekiti wa Majadiliano ya duara kuzungumzia uongozi barani Afrika na changamoto za maendeleo ulioandaliwa na Taasisi ya UONGOZI Tanzania, Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa David Msuya akitoa ufafanuzi wa majadiliano.Kulia ni Mgeni Rasmi, Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki.
 Waziri wa mambo ya Nje, Bernard Membe (kulia), waziri Makuu Mstaafu, Cleopa Msuya na Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki wakifuatilia Majadiliano ya duara kuzungumzia uongozi barani Afrikajijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya waalikwa wakiwemo wahariri wa vyombo vya habari walihudhuria majadiliano hayo. kushoto ni Gabi Mgaya kutoka Daily News.
 Mwongozaji wa Majadiano hayo, Sauda Simba Kilumanga akisema jambo muda mfupi kabla ya kufunga.
Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki akizungumza jambo na Waziri Mkuu Mstaafu, na Mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Sinde Warioba huku Katikati waziri wa Mambo ya nje na Ushirikaino wa Kimataifa, Bernard Membe akichangia wakati viongozi hao wakitoka katika Majadiliano ya duara kuzungumzia uongozi barani Afrikayaliyoandaliwa na Taasisi ya UONGOZI jijini Dar es Salaam.

WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU ASAFIRI KWA SGR KUELEKEA DODOMA

  Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Septemba 30, 2026 amesafiri kwa treni ya Reli ya Kisasa (SGR) kutoka Dar es Salaam kuelekea Dodoma. ...