Friday, September 15, 2017

TANZANIA IKO TAYARI KUWA MWENYEJI WA TAMASHA LA JAMAFEST 2019-DKT. HARRISON MWAKYEMBE

Naibu Waziri Mkuu ambaye ni Waziri wa Wizara ya Mambo ya Afrika Mashariki ya Uganda Mhe. Ali Kirunda Kivejinja akimkaribisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Harisson Mwakyembe kabla ya kumkabidhi Bendera ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya kuashiria kuwa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa ni zamu yake kukabidhiwa dhamana ya kuandaa Tamasha la Nne (4) la Utamaduni na Sanaa la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST) litakalofanyika mwaka 2019.
Naibu Waziri Mkuu ambaye ni Waziri wa Wizara ya Mambo ya Afrika Mashariki ya Uganda Mhe. Ali Kirunda Kivejinja akabidhi Bendera ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Tanzania Mhe. Dkt. Harisson Mwakyembe ikiashiria kuwa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ni zamu yake kukabidhiwa dhamana ya kuandaa Tamasha la Nne (4) la Utamaduni na Sanaa la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST) litakalofanyika mwaka 2019 jana usiku hafla hyo ilifanyika katika Jumba la Sanaa la Taifa jijini Kampala Nchini Uganda.
Kaimu Balozi ambaye pia Naibu Balozi wa Tanzania Nchini Uganda Balozi Elibariki Nderimo Maleko aliyevaa shati la kitenge akiwaongoza Washiriki wa Tanzania katika Tamasha la Utamaduni na Sanaa la Afrika Mashariki pamoja na Watanzania wanaishi Uganda kusherehekea kupokea bendera ya Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya kukabidhiwa kutoka kwa Nchi ya Uganda


Na Benedict Liwenga-WHUSM, Kampala-Uganda.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kwamba, Tanzania iko tayari kuwa wenyeji wa Tamasha la Utamaduni na Sanaa Afrika Mashariki maarufu kama JAMAFEST kwa mwaka 2019.

Kauli hiyo ameitoa jana Mjini Kampala nchini Uganda wakati wa Ufungaji wa Tamasha hilo kwa mwaka 2017 ambapo wenyeji kwa mwaka huu walikuwa ni nchi ya Uganda.

Mhe. Mwakyembe amezipongeza nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ambazo zimehudhuria tamasha hilo kwa ushirikiano wa hali ya juu katika kubadilishana uzoefu na ujuzi juu ya masuala mbalimbali yanayohusu utamaduni na sanaa kwakuwa yameongeza mahusiano mapya ya karibu baina ya nchi hizo.

Waziri Mwakyembe aliezea kufurahishwa kwake kwa kujionea ngoma mbalimbali za kitamaduni toka kwa nchi wanachama ambazo zinaakisi uhalisia wa utamaduni wa nchi hizo, pia amefurahishwa na kwa kujionea bidhaa mbalimbali adimu toka kwa nchi hizo jambo ambalo amesisitiza kwamba nchi wanachama hazinabudi kuendelea kushirikiana katika kuzilinda tamaduni hizo na kuendelea kujifunza ujuzi mbalimbali wa kazi za sanaa.

“Nilipotembelea Maonyesho ya Tamasha hili pale katika viwanja vya Kololo nilifurahi sana kujionea ngoma za kitamaduni toka kwa vikundi mbalimbali vya nchi wanachama wa Jumuiya yetu ya Afrika Mashariki, hakika inapendeza sana, kwakweli tuzidi kuzilinda tamaduni zetu na kushirikiana kwa karibu zaidi”, alisema Mhe. Mwakyembe.

Akiongea kuhusu suala la Tanzania kukubali kuwa wenyeji wa Tamasha lijalo litakalofanyika mwaka 2019, Dkt. Mwakyembe alisema kwamba, Tanzania iko tayari kuwa wenyeji katika tamasha hilo lijalo na amezitaka nchi wanachama kujitahidi kushiriki pasipo kukosa wakiwa na bidhaa zao za kutosha huku akiwaahidi kuwa pindi wajapo Tanzania watafurahia mambo mengi na kujionea namna Watanzania wanavyo chapa kazi kutokana na kaulimbiu ya ‘HAPA KAZI TU’ iliyoasisiwa na Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

“Kwakuwa mwaka 2019 ni mzunguko wa Tamasha kama hili niwaambie kwamba, Tanzania iko tayari kuwa mwenyeji wa Tamasha hili na nawakaribisheni kwa dhati kabisa mje kujionea nchi yetu na namna tunavyofanya kazi kwa bidii, lakini pia mje na bidhaa nyingi zaidi kwa ajili ya kuwaonyesha Watanzania”, alisema Dkt. Mwakyembe.

Tamasha la JAMAFEST lilianzishwa mwaka 2013 nchini Rwanda na baadhi ya Viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo kwa mwaka huu tamasha hilo linafanyika mjini Kampala nchini Uganda ambapo kwa mwaka 2019 linatarajiwa kufanyika nchini Tanzania.

KUKAMATA NA KUCHOMA NYAVU HAITOSHI, TUWACHOME WAHALIFU- RC RUKWA

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mtaaafu Zelote Stephen (Kulia)akitoa maelekezo namna ya kuziteketeza nyavu haramu (hazimo kwenye picha) mbele ya maafisa aliongozana nao kushiriki uteketezaji wa zana hizo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mtaaafu Zelote Stephen (Katikati Mwenye suti ya ugoro) akiwasha moto tayari kwaajili ya kuzitekezeteza zana  haramu, kulia ni Juma Makongoro Afisa Mfawidhi Idara ya Uvuvi kanda ya Rukwa kushoto ni diwani wa kata ya kirando Kessy Sood


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mtaaafu Zelote Stephen kwa pamoja na  Mfawidhi Idara ya Uvuvi kanda ya Rukwa Juma makongoro pamoja na Diwani wa Kata ya Kirando Mh. Kessy Sood wakiteketeza zana haramu.
Nyavu zenye thamani ya shilingi milioni 57.6 zikiteketea kwa moto mbele ya wananchi, katika mwalo wa kijiji cha kirando, Ziwa Tanganyika, Wilayani Nkasi Mkoani Rukwa.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafi Zelote Stephen ameionya idara ya uvuvi iliyo chini ya wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi nchini kuhakikisha wanawachukulia hatua wale wote wanaokamatwa na zana haramu za uvuvi na kutangaza hukumu zao na si kuishia kwenye kuchoma zana zao tu.

Ameyasema hayo wakati akijiandaa kushiriki zoezi la kuteketeza zana haramu zilizokamatwa kupitia doria katika vijiji vya Kabwe, Isaba, Chongokatete, mandakerenge, kolwe, lupata na kisenga katika wilaya ya Nkasi Mkoani humo. zoezi lililofanyika katika mwalo wa kijiji cha Kirando. 

“Kukamata na kuchoma haitoshi, kwasababu hii inaungua tu, nataka tuwachome wahalifu kwa kutumia sheria, nimechoma sana nyavu hizi na huu mtindo bado unaendelea, hii haina tija, kila tukichoma madhara yanatokea, mazingira yanaharibika, sasa tuseme basi, ningependa kusikia mhalifu kakamatwa kapelekwa mahakamani na kupewa adhabu,” Amesema

Katika kuhakikisha wahalifu hao wanapatika Mh. Zelote amewaasa watumishi wa idara hiyo kuachana na kupokea rushwa, jambo ambalo linaonekana kukwamisha juhudi za serikali katika kulinda rasilimali zake kwaajili ya faida ya kizazi hiki na kijacho.

Amesisitiza kuwa wananchi bado wanahitaji kuendelea kupatiwa elimu juu ya umuhimu wa rasilimali hizo na wajulishwe kuwa rasilimali hizo ni za watanzania wote na hatimae kuacha tabia kuvua samaki hao kwa zana zisizokubalika na sheria za serikali.

Mh. Zelote aliishauri idara hiyo kuwa panapokuwa na zoezi hilo linalofanyika mbele ya wananchi wahakikishe kunakuwa na nyavu halali zinazokidhi viwango vya serikali na kuwaelimisha wananchi tofauti iliyopo ili wasiojua nao wapate kufahamu matakwa ya serikali katika kuhifadhi mazingira.

Kutokana na doria hiyo iliyofanywa na kikosi cha usimamizi wa rasilimali za uvuvi Kijiji cha Kipili kwa kushirikiana na polisi pakmoja na kikosi cha jeshi la wanamaji wote wa kipili kuanzia Juni hadi September 2017 waliweza kukamatanyavu zisizokidhi viwango vya serikali zenye thamani ya shilingi milioni 57.6.

Miongoni mwa nyavu zilizokamatwa ni nyavu 32 za Makira (gilinets) zenye thamani ya shilingi milioni 38.4, nyavu za dagaa zenye macho chini ya 8mm zenye thamani ya shilingi milioni 16.5 na makokoro ya vyandarua yenye thamani ya shilingi milioni 2.7.

Awali akisoma taarifa hiyo fupi ya uteketezaji wa zana haramu za uvuvi kwa mgeni rasmi Afisa mfawidhi idara ya uvuvi kanda ya Rukwa Juma Makongoro alitaja kuwa kuna manufaa mengi yanayopatikana kutokana na rasilimali hiyo ikiwa ni pamoja na watu kujipatia ajira, kitoweo, fedha za kigeni na kuingizia serikali kodi ambayo hutumika kutekeleza miradi ya maendeleo.

BANK OF AFRICA – TANZANIA yazindua program mpya ya kibenki ya “SWAHIBA MOBILE APP”

Sehemu ya wageni waalikwa wakiwa kwenye meza kuu.

Mkurugenzi Mtendaji wa BANK OF AFRICA – TANZANIA, Mr. Ammishaddai Owusu-Amoah akizindua rasmi program ya SWAHIBA Mobile App. Kulia kwake ni mkuu wa kitengo cha rasilimali watu wa benki hiyo Ms. Mercy Msuya na Meneja Masoko, utafiti na maendeleo wa benki hiyo ndg. Muganyizi Bisheko.

Mr. Emmanuel Mshindo, Mkuu wakitengo cha Huduma mbadala za kibenki akitoa maelezo juu ya huduma mbalimbali zipatikanazo katika program ya SWAHIBA Mobile, wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma hiyo mapema hii leo.

Mkurugenzi Mkuu wa MaxCom Africa, watoaji wa huduma za Max Malipo pichani ndugu Jameson Kasati, ameipongeza BANK OF AFRICA kwa hatua za makusudi za kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma zake za kibenki. Aidha aliongeza Zaidi kua mtazamo wa BANK OF AFRICA wa kutumia mabadiliko ya kiteknolojia na kidigitali katika kusogeza huduma zake karibu Zaidi kwa watanzania unashabihiana na wa MaxCom.

Naibu Mkurugenzi wa BANK OF AFRICA Bw. Wasia Mushi, akiongea na wageni waalikwa (hawapo pichani) katika hafla ya uzinduzi wa program ya SWAHIBA Mobile mapema hii leo.

Sehemu ya wageni waalikwa, uongozi na wafanyakazi wa BANK OF AFRICA wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya hafla ya uzinduzi rasmi wa Programu ya SWAHIBA Mobile.

BANK OF AFRICA – TANZANIA imezindua programu yake mpya ya kibenki inayoitwa "SWAHIBA Mobile" kwenye soko la Tanzania. Huduma hii inakuja kama muendelezo wa programu ya B- Mobile, inayoruhusu watumiaji kufurahia huduma kamili za kibenki kupitia aina yoyote ya simu za mkononi, wakati wowote.

SWAHIBA Mobile App inawapa wateja urahisi wa kutumia huduma za kibenki katika simu kwani inakuja na muonekano mzuri Zaidi na sifa nyingi mpya zinanzowarahisishia wateja kufuatilia akaunti zao za binafsi na za kibiashara kwa wakati mmoja.

Huduma zipatikanazo kwenye programu hii ni: huduma za kuhamisha fedha, huduma za hundi, maombi ya mkopo wa papo hapo, malipo ya bili mbalimbali, huduma za utoaji fedha kwenye ATM bila kadi, kuongeza muda wa maongezi, usajili binafsi wa mobile banking na huduma za e-chama pamoja na nyingine nyingi.

Zaidi ya hayo, SWAHIBA Mobile APP inaweza kutumiwa na Mtanzania yoyote hata ambae si mteja wa BANK OF AFRICA. Hii ni kupitia huduma mbalimbali zinazopatikana kabla ya kuingia kwenye program yaani “without Log in services”. huduma hizi ni kama vile maelezo kuhusu Huduma mbalimbali zitolewazo na BANK OF AFRICA, Maombi ya Mikopo, maelekezo kuhusu yalipo Matawi ya BANK OF AFRICA na ATMs, pamoja na viwango vya ubadilishaji fedha za kigeni.

Mr. Ammishaddai Owusu-Amoah, Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa BANK OF AFRICA - TANZANIA alisema Benki yake inajivunia kuanzisha programu hii mpya ya benki kiganjani katika wakati huu muhimu ambapo benki hiyo inaadhimisha miaka 10 ya biashara katika nchi ya Tanzania. "Uzinduzi wa SWAHIBA Mobile App ni namna ya kipekee ya kuwasilisha shukrani zetu kwa wateja, jamii, washirika, wamiliki na wadau wote, walio tupa ushirikiano wa kutosha katika kipindi cha miaka 10 ya kazi nchini ".

"Huduma hii pia inakuja kutia msistizo wa ahadi yetu ya kuweka mapendekezo ya wateja wetu kwanza na kuwaongezea uzoefu wa kidigitli Zaidi katika ukuwaji wa sayansi na technologia. Mkurugenzi aliendelea kueleza “Pia inathibitisha uamuzi wa benki wa kujenga uwepo wake wa kidigitali na kukidhi mahitaji ya haraka ya wateja wetu "

Bwana Emmanuel ameeleza: " katika dunia ya sasa kuna ongezeko kubwa sana la matumizi ya technologia pamoja na matumizi ya “Simu za kisasa na Tablets” tumeunda huduma hii katika ubunifu na uwezo wa hali ya juu sana na ambao mtanzania yoyote anaweza kutumia. Program hii inamuongezea mteja uzoefu wa kubenki kidigitali Zaidi huku akifurahia huduma maridhawa kwa uharaka zadid bila kujali kuhusu foleni benki au kufungwa kwa tawi.

Mbali na ongezeko la huduma SWAHIBA Mobile App inamfumo bora wa ulinzi wa fedha. “ Ulinzi wa fedha za wateja wetu ni kitu cha kwanza kabisa ambacho benki inaangalia kwenye programu hii benki imeingiza vipengele vya usalama wa hali ya juu kama vile vinavyopatikana kwenye benki ya mtandao (B WEB SMART) "alieleza Mr. Mshindo.

“Program yetu hii ni rahisi sana kutumia ikiwa imeundwa kwa kumzingatia mteja ili kumwezesha kuona machaguo mbalimbali punde tuu anapifungua program hii na hili limefanyika ili kupunguza mlolongo mrefu katika uchaguzi wa huduma ambayo mteja atakua anahitaji” alisema Mshindo, kwa sasa SWAHIBA MOBILE App, inaweza kupakuliwa kupitia “ Play store” kwa watumiaji wa Android na Apple iOS kwa watumiaji wa Iphone.

Thursday, September 14, 2017

DKT.MWAKYEMBE AMEWAPONGEZA WAJASIRIAMALI WA TANZANIA KWA KUSHIRIKI TAMASHA LA JAMAFEST KAMPALA, UGANDA


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Utamaduni, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akiangalia ngoma ya kiutamaduni iliyokuwa ikipigwa na Kikundi cha Sanaa na Utamaduni Tanzania (TaSUBA) katika banda lao wakati wa Tamasha la Utamaduni na Sanaa Afrika Mashariki (JAMAFEST) linalofanyika mjini Kampala, Uganda 13 Septemba, 2017.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Utamaduni, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akimsikiliza mjasiriamali wa Tanzania kuhusu baadhi ya bidhaa zilizopo katika banda lao wakati wa Tamasha la Utamaduni na Sanaa Afrika Mashariki (JAMAFEST) linalofanyika mjini Kampala, Uganda 13 Septemba, 2017.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Utamaduni, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akipokea zawadi ya shati toka kwa mjasiriamali wa Tanzania mara alipotembelea banda lao wakati wa Tamasha la Utamaduni na Sanaa Afrika Mashariki (JAMAFEST) linalofanyika mjini Kampala, Uganda 13 Septemba, 2017.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Utamaduni, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (mwenye tai nyekundu) akiangalia moja ya ubunifu wa picha iliyochongwa na mjasiriamali wa Tanzania wakati wa Tamasha la Utamaduni na Sanaa Afrika Mashariki (JAMAFEST) linalofanyika mjini Kampala, Uganda 13 Septemba, 2017.PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amewapongeza Wajasiriamali wa Tanzania kwa ushiriki wao katika Tamasha la Utamaduni na Sanaa Afrika Mashariki maarufu kama JAMAFEST.

Dkt. Mwakyembe ametoa pongezi hizo leo mjini Kampala nchini Uganda katika viwanja vya Mashujaa Kololo alipotembelea kujionea namna tamasha hilo lilivyopokelewa na wadau wake walioiwakilisha Tanzania wakiwemo wajasiriamali toka vikundi mbalimbali, vikundi vya ngoma, vikundi vya sanaa ya maigizo pamoja na baadhi ya wasanii.

Katika tamasha hilo, Dkt. Mwakyembe pia alipata fursa ya kutembelea baadhi ya mabanda ya wajasiriamali hao pamoja na kuongea nao huku akijionea bidhaa mbalimbali zinazouzwa na nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki jambo ambalo limemfurahisha sana hususani kwa upande wa watu kutoka Tanzania kwakuwa wamejaza mabanda yao kwa bidhaa kadha wa kadha.
“Tamasha hili linaonyesha utajiri mkubwa wa sanaa, utamaduni pamoja na bidhaa tulizonazo kama nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, na hapa tumekutana kwasababu tunabadilishana mawazo na kuonyeshana bidhaa mbalimbali za nchi zetu”, alisema Dkt. Mwakyembe.
Aidha, katika ziara hiyo, Dkt. Mwakyembe amewatoa wasiwasi wajasiriamali hao kuhusu suala la upatikanaji wa masoko huku akiwaahidi kuwatafutia fursa ya kuwapeleka wajasiriamali hao pamoja na bidhaa zao Bungeni mjini Dodoma ili ziweze kupata soko kwa urahisi kupitia wabunge.
“Niwatoe wasiwasi wajasiriamali wote wa Tanzania mliohudhuria hapa, nitahakikisha kuwa pindi tunaporudi nyumbani nitatafuta wasaa wa kulishawishi Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili nyie mpate nafasi ya kuleta bidhaa zenu katika viwanja vya Bunge ili basi Wabunge wapate kujua haswa vitu vizuri mlivyonavyo nah ii itawasaidia kuviuza kwa urahisi zaidi na kujipatia vipato vyenu”, aliongeza Dkt. Mwakyembe.

Sambamba na hilo, Dkt, Mwakyembe amewahakikishia wajasiriamali hao kuhusu suala la kujitangaza kupitia vyombo vya habari akisema kwamba, atajitahidi kutoa ushawishi kwa vyombo vya habari nchini ili viweze kuwapatia muda wa kuwatangaza wajasiriamali hao ili wapate kujulikana ikiwemo shughuli wazifanyazo.
“Nitahakikisha kuwa siku mnapopewa nafasi ya kuja viwanja vya Bunge basi mnapata muda wa kutosha katika vyombo vya habari ili mpate kujulikana, hivyo kila mmoja wenu naamini atapewa nafasi ya kufanya mahojiano kwa kujieleza shughuli azifanyazo na mahali anapopatikana na hii itawasaidia kupata masoko zaidi toka kwa watu mbalimbali”, alisema Dkt. Mwakyembe.

Kwa upande wao wajasiriamali hao wameshukuru Waziri Mwakyembe kwa juhudi alizowafanyia hususani za kuhakikisha kwamba wanahudhuria kwa kiwango kikubwa katika tamasha hilo, lakini pia ahadi aliyowapa ya kuwapeleka Bungeni ili wakatangaze bidhaa zao na kuwatangaza katika vyombo vya habari nchini.
Tamasha la JAMAFEST lilianzishwa mwaka 2013 nchini Rwanda na baadhi ya Viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo kwa mwaka huu tamasha hilo linafanyika mjini Kampala nchini Uganda ambapo pia tamasha hili linatarajiwa kufanyika tena katika moja ya nchi mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) mwaka 2019.

Msisubiri Muda wa Kuchukua Leseni Kuisha - Dkt. Abbasi

 Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akielezea jambo wakati wa zoezi la kukabidhi Leseni za machapisho kwa Kampuni ya The Guardian Ltd leo Jijini Dar es Salaam ikiwa ni muendelezo wa utekelezaji wa matakwa ya sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 kifungu kidogo namba 5(e). Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi anayeshugulikia Usajili Patrick Kipangula na kulia ni Mhariri Mkuu wa The Guardian Ltd Jesse Kwayu. Kampuni hiyo inamiliki magazeti ya Nipashe, Nipashe Jumapili, Sema Usikike,The Guardian, The Guardian On Sunday, Kulikoni, Lete Raha, This Day, Alasiri na Taifa Letu.
  Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akimkabidhi Leseni za machapisho Mhariri Mkuu wa Kampuni ya The Guardian Ltd Jesse Kwayu (kulia) ikiwa ni muendelezo wa utekelezaji wa matakwa ya Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016 kifungu kidogo namba 5(e).Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi anayeshugulikia Usajili Patrick Kipangula. Kampuni hiyo inamiliki magazeti ya Nipashe, Nipashe Jumapili, Sema Usikike,The Guardian, The Guardian On Sunday, Kulikoni, Lete Raha, This Day, Alasiri na Taifa Letu.
  Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akimkabidhi Leseni za machapisho Meneja wa Sheria na Uhusiano  wa Kampuni ya The Guardian Ltd Bw. Emmanuel Matondo(kulia) ikiwa ni muendelezo wa utekelezaji wa matakwa ya Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016 kifungu kidogo namba 5(e). Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi anayeshugulikia Usajili Patrick Kipangula. Kampuni hiyo inamiliki magazeti ya Nipashe, Nipashe Jumapili, Sema Usikike,The Guardian, The Guardian On Sunday, Kulikoni, Lete Raha, This Day, Alasiri na Taifa Letu.
  Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi na Meneja wa Sheria na Uhusiano  wa Kampuni ya The Guardian Ltd Bw. Emmanuel Matondo (kulia) wakionyesha  Leseni ya machapisho aliyotolewa kwaa ajili ya gazeti la Nipashe mara baada ya kukabidhiwa leo Jijini Dar es Salaam.Utoaji wa Leseni unafuatia muitikio wa wamiliki wa machapisho kuzingatia matakwa ya Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 kifunga namba 5(e). Kampuni hiyo inamiliki magazeti ya Nipashe, Nipashe Jumapili, Sema Usikike,The Guardian, The Guardian On Sunday, Kulikoni, Lete Raha, This Day, Alasiri na Taifa Letu.
 Mhariri Mkuu wa Kampuni ya The Guardian Ltd Bw. Jesse Kwayu na Meneja Sheria na Uhusiano wa kampuni hiyo Bw. Emmanuel Matondo wakiwa wameshika Leseni 10 za machapisho yanayomilikiwa na The Guarid baada ya kukabidhi wa Leseni kumi za machapisho yanayomilikiwa na Kampuni hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Kampuni hiyo inamiliki magazeti ya Nipashe, Nipashe Jumapili, Sema Usikike,The Guardian, The Guardian On Sunday, Kulikoni, Lete Raha, This Day, Alasiri na Taifa Letu.

Picha na: Idara ya Habari - MAELEZO

Tuesday, September 12, 2017

TRA YATOA SOMO LA KODI KWA WASHEREHESHAJI

Mkurugenzi wa huduma na Elimu kwa mlipa kodi wa Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), Richard Kayombo akikata keki kuashiria uzinduzi wa Chama cha washereheshaji (WSB) 'Wakali wa sherehe Bongo' jijini Dar es Salaam leo. Kutoka (kushoto) ni Moafisa wakuu wa Elimu kwa mlipa Kodi, Rose Mahendeka na Julius Mjenga, Mwenyekiti wa WSB, Lameck Matemba na Katibu wa chama hicho, Reuben Ndimbo.
Mwenyekiti wa WSB, Lameck Matemba akiongea wakati wa uzinduzi huo. 
Afisa Mkuu wa Elimu kwa mlipa Kodi, Julius Mjenga akitoa mada kwa wana WSB. 
Mkurugenzi wa huduma na Elimu kwa mlipa kodi wa Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), Richard Kayombo akimpa za wadi ya diary Mwenyekiti wa WSB, Lameck Matemba 
Mkurugenzi wa huduma na Elimu kwa mlipa kodi wa Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), Richard Kayombo akiwa katika picha ya pamoja na wana WSB na wageni wao. 
Mkurugenzi wa huduma na Elimu kwa mlipa kodi wa Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), Richard Kayombo akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa WSB.
Mkurugenzi wa huduma na Elimu kwa mlipa kodi wa Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), Richard Kayombo
Mkurugenzi wa huduma na Elimu kwa mlipa kodi wa Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), Richard Kayombo akitoa elimu kwa wanachama wa WSB. 

DC MAHONGO AFUNGUA MKUTANO MKUU WA APC KARATU


Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Theresia Mahongo wa pili kutoka kushoto akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa APC Claud Gwandu wa kwanza kushoto, Makamu Mwenyekiti Charles Ngereza wa tatu kutoka kushoto na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Karatu Bw. Mourice wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa APC 2017 uliofanyika ukumbi wa KKK Karatu.(Picha na PamelaMollel Arusha).
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa APC wakisikiliza kwa makini hotuba iliyokuwa ikitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Karatu Theresia Mahongo(hayuko pichani), 
Mkuu wa Wilaya ya Karatu Theresia Mahongo akielekea kupiga picha ya pamoja na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kufungua mkutano mkuu wa APC 2017 katika ukumbi wa KKKT Lutherani Karatu 
Mjumbe wa mkutano mkuu wa APC, Nerbert Mramba katikati akichangia mada kwenye mkutano Mkuu wa APC 2017 katika ukumbi wa KKKT Lutheran.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa APC waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbalimbali nchini wakiwa katika picha ya pamoja katika lango la kuingilia hifadhi ya Taifa Tarangire
Viongozi wa APC kutoka kushoto Pamela Mollel (Mwekahazina), Claud Gwandu (Mwenyekiti), na Charles Ngereza (Makamu Mwenyekiti) wakisikiliza wajumbe wa mkutano mkuu wa APC uliokuwa ukiendelea katika ukumbi wa KKKT Karatu.

WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU AMPONGEZA NDEJEMBI, AMSIFIA KWA UADILIFU NA UCHAPAKAZI

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba , amempongeza Mhe. Deogratius John Ndejembi kwa kuaminiwa ...