Wednesday, March 12, 2025

WAZIRI SILAA AWASILI ARUSHA KWA ZIARA YA SIKU MBILI, AAZIMIA KUIMARISHA TEKNOHAMA KWA VIJANA






Na Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Jerry William Silaa (Mb.), amewasili katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha leo, tarehe 12 Machi 2025, kabla ya kuanza ziara ya siku mbili mkoani humo.

Mara baada ya kuwasili, Waziri Silaa alipokelewa na mwenyeji wake, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Paul Makonda, ambaye alimkaribisha rasmi na kumpongeza kwa juhudi kubwa anazozifanya katika kuimarisha sekta ya mawasiliano nchini, hususan katika uwekaji wa minara ya mawasiliano.

Katika ziara yake, Mhe. Silaa atatembelea na kufanya mazungumzo na vijana wanaojihusisha na bunifu changa za TEHAMA (Startups), akilenga kuwahamasisha na kuwaunga mkono katika kukuza na kuboresha ubunifu wao kwa maendeleo ya kidijitali nchini.

Mhe. Makonda ameahidi ushirikiano wa dhati kati ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha na Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, akibainisha kuwa kuimarishwa kwa miundombinu ya mawasiliano kutasaidia kupunguza migogoro na changamoto mbalimbali zinazokabili mkoa huo.

Ziara hii inalenga kuchochea maendeleo ya TEHAMA, kuhakikisha vijana wanapata fursa stahiki za kujifunza, kuendeleza miradi yao, na kuchangia uchumi wa kidijitali kwa manufaa ya taifa zima.


#Arusha 🏔️ #Startups 🚀 #SmartTanzania 📡

No comments:

TANZANIA AND BURKINA FASO IN TALKS TO ESTABLISH CARDIAC FACILITY MODELED AFTER JAKAYA KIKWETE CARDIAC INSTITUTE

  On April 17, 2025, in Ouagadougou, the Executive Director of Muhimbili National Hospital, Prof. Mohamed Janabi @ProfJanabi, along with the...