VICTOR MASANGU, BAGAMOYO
Zaidi ya wananchi elfu 14 kutoka kata nane zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani kutoka katika makundi mbali mbali waliokuwa wanakabiliwa na changamoto mbali mbali katika masuala ya ndoa, mirathi, migogoro ya ardhi, pamoja na ukatili wa kijinsia wamepata mkombozi baada ya kupatiwa msaada wa kisheria bure wa Mama Samia kwa lengo la kuweza kutambua haki zao za msingi.
Hayo yamebainishwa na Wakiri George Molel ambaye ni mratibu wa huduma ya kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia katika Halmashauri ya Bagamoyo ambapo amesema kwamba lengo kubwa la msaada huo wa kisheria ni kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi ambayo itawasaidia wananchi kujua haki zao za msingi katika masuala mbali mbali.
Hayo yamebainishwa na Wakiri George Molel ambaye ni mratibu wa huduma ya kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia katika Halmashauri ya Bagamoyo ambapo amesema kwamba lengo kubwa la msaada huo wa kisheria ni kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi ambayo itawasaidia wananchi kujua haki zao za msingi katika masuala mbali mbali.
Wakiri George amebainisha kwamba katika kampeni hiyo ya msaada wa kisheria Katika Halmashauri ya Bagamoyo imeweza kufanikiwa kupitika katika kata nane, zikiwemo Fukayose,Makurunge, Yombo, Kiromo,Kerege, Nianjema, Kisutu, pamoja na Kata ya Dunda ambapo wameweza kutoa elimu kwa wanafunzi, walimu, wananchi wa kawaida, makanishani pamoja na makundi mbali mbali.
“Kampeni hii ya msaada wa kisheria ya Mama Samia imeanzishwa maalumu kwa lengo la kuweza kuwasaidia wananchi hasa wa hali ya chini kupata msaada wa kisheria kutoka kwa wataalamu mbali mbali kutoka Halmashauri pamoja na baadhi ya mawakiri kutoka Wizaraya Katiba na sheria na kwamba msaada huo unatolewa bila malipo yoyote lengo ikiwa ni kuwasaidia wananchi,”amesema Wakiri George.
Kwa upande wake Afisa maendeleo ya Jamii Kata ya Kerege Lilian Mkosyange amesema kuwepo kwa chanagmoto mbali mbali kwa wananchi ikiwemo suala la wakinababa kuwa na tabia ya kutelekeza familia zao na kupelekea mama na watoto kubaki peke yao bila msaada wowote.
Naye mmoja wakazi wa Wilaya ya Bagamoyo Samweli Ringo amempongeza kwa dhati Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kuanzisha kampeni hiyo na kubainisha kwamba elimu ambayo wameipata itakwenda kuwa mkombozi mkubwa kwani wameweza kujifunza mambo mbali mbali juu ya msaada wa kisheria.
Kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia inaendelea kufanyika katika Mkoa wa Pwani ambapo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo tayari imeshapita katika kata zipatazo nane na kutoa msaada wa kisheria katika masuala ya Ndoa, mirathi,migogoro ya ardhi, wosia,matunzo ya watoto,kesi za madai,unyanyasaji wa kijinsia, pamoja na haki za binadamu na mambo mengine ya kimsingi yanayohitaji msaada huo.
No comments:
Post a Comment