*Asisitiza kuwa mifugo ni uchumi, ajira na biashara
*Atoa wito kwa wakulima na wafugaji wawe wamoja
WAZIRI
MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali inaendelea kuweka mikakati
madhubuti ya kuhakikisha sekta ya mifugo inakuwa endelevu na yenye tija.
Amesema
kuwa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan mara zote ameweka msisitizo
katika kuiendeleza sekta hiyo kwa kuwa mifugo ni uchumi, ajira na ni
biashara.
Ameyasema hayo kwa nyakati tofauti alipozungumza na
wananchi katika mikutano aliyoifanya jana Jumatano (Machi 12, 2025)
Wilayani Igunga, mkoani Tabora ambapo yupo kwenye ziara ya kikazi ya
siku mbili.
“Tunawahamasisha wafugaji, fugeni mifugo ni uchumi,
mifugo ni maisha na mifugo ni pesa na wakulima limeni tupate mazao mengi
ya chakula na biashara na ni lazima wafugaji na wakulima tuelewane.”
Katika
hatua nyingine Mheshimiwa Majaliwa amezitaka halmashauri zote nchini
kuweka mikakati ya kuhakikisha wanakuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na
kuzisimamia fursa zilipo kwenye maeneo yao ili kuwanufaisha wananchi.
“Mkifanya hivyo mtakuwa mmewasaidia wananchi kujiendeleza kiuchumi.”
Akizungumza
baada ya kuweka jiwe la msingi kwenye shule ya Sekondari ya Seif
Gulamali, Mheshimiwa Majaliwa ameitaka jamii kuweka nguvu za pamoja
katika kumlinda mtoto wa kike ili waweze kutimiza ndoto zao.
Pia,
Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Serikali itaendelea kusimamia
utekelezaji wa mikakati iliyopo katika sekta ya elimu ili sekta hiyo
iweze kuwanufaisha watanzania kwa kukuza ubora wa elimu nchini.
Thursday, March 13, 2025
MAJALIWA: SERIKALI ITAENDELEZA MIKAKATI YA KUKUZA SEKTA YA MIFUGO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Waziri Mkuu azindua boti mbili za doria na uokozi
Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba ametoa siku 14 kwa wizara na taasisi zinazohusika na Kituo cha Kitaifa cha pamoja cha Oparesheni zipeleke w...
-
Hapa mmoja wa watoto hao akiwa na kijana mwenzake mwenye miaka 18, wote wako sawa lakini yeye hawezi kuzungumza kama watu wa kawaida. Mama S...
-
Nadhani mtakumbuka kibwagizo maarufu katika TV ambacho kinaimbwa perupe pepero perupe pepero hawa ni vijana wa Sisi Tambala waliokuwapo kati...
-
Mdau Julius Samwel hivi karibuni alikuwa huko Mwanza na hizi ndizo alizofanikiwa kutumegea, wadau hebu someni hicho kibao mniambie kuna nini...






No comments:
Post a Comment