Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, ameungana na waombolezaji katika msiba wa Bi. Damaris Simeon Hawassi, mwenza wa Dkt. Frank Haule Hawassi, Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Idara ya Uchumi na Fedha.
Balozi Nchimbi alifika nyumbani kwa marehemu, eneo la Mihuji, Dodoma, leo Jumamosi, Machi 22, 2025, ambapo alitia saini kitabu cha maombolezo na kumfariji Dkt. Hawassi na familia yake.
Mbali na hilo, akiwa pamoja na viongozi wengine waandamizi wa Chama na Serikali, wa sasa na wastaafu, Balozi Nchimbi alitoa heshima za mwisho kwa marehemu, akitoa pole kwa familia na ndugu walioguswa na msiba huu mzito.
CCM inaendelea kuwa bega kwa bega na familia ya Dkt. Hawassi katika kipindi hiki kigumu, ikiwapa faraja na mshikamano wa dhati.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. 🙏🏽🕊️
#CCM #BaloziNchimbi #Maombolezo #MunguAilazeRohoYaMarehemuMahaliPema
No comments:
Post a Comment