Tuesday, March 04, 2025

DKT. NCHEMBA ASHIRIKI UZINDUZI WA HUDUMA ZA KIDIGITALI YA BENKI YA NBC











Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb), ameshiriki uzinduzi wa huduma za kidigitali za Benki ya NBC (NBC Kiganjani App) inayomwezesha mteja kupata huduma za kibenki kigigitali kwa kutumia simu za mkononi. tukio ambalo, Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa alikuwa Mgeni Rasmi, lililofanyika katika Ukumbi wa The Super Dome, Masaki, Jijini Dar es Salaam.


Akimkaribisha, Mhe. Waziri Mkuu kuzungumza na kuzindua NBC Kiganjani App, Mhe. Dkt. Nchemba aliipongeza NBC kwa ubunifu walioufanya na kwamba hatua hiyo si tu kwamba inaimarisha maendeleo ya sekta ya benki, bali pia inaendana na dhamira ya serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya kujenga uchumi jumuishi unaowezesha upatikanaji wa huduma za kifedha kwa wananchi wote.

Aidha, Mhe. Dkt. Nchemba, aliipongeza Benki hiyo kwa kudhamini Ligi Kuu ya Tanzania Bara (NBCPL) ambayo kupitia udhamini wao imekuwa na msisimko mkubwa na kuiwezesha Tanzania kupanda viwango na kuwa ligi namba 4 kwa Ubora baranı Afrika.



No comments:

NAIBU WAZIRI WA FEDHA AMWAKILISHA WAZIRI WA FEDHA KATIKA KONGAMANO LA 16 LA MWAKA LA WATAALAM WA UNUNUZI NA UGAVI – ARUSHA

Naibu Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Mhandisi Mshamu Ali Munde, amemwakilisha Waziri wa Fedha katika ufunguzi wa Kongamano la 16 la Mwaka la Wa...