Wednesday, March 26, 2025

WAZIRI MHAGAMA AWASILISHA UJUMBE MAALUM WA RAIS SAMIA KWA RAIS CHAKWERA WA MALAWI









Waziri wa Afya, Mhe. Jenista Mhagama, amewasilisha ujumbe maalum wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa Rais wa Jamhuri ya Malawi, Mhe. Lazarus Chakwera, katika Ikulu ya Rais jijini Lilongwe, Malawi.

Baada ya kupokea ujumbe huo, Rais Chakwera ameishukuru Tanzania na kusisitiza kuwa Malawi itaendelea kuimarisha ushirikiano wa kihistoria uliopo kati ya mataifa hayo mawili kwa maslahi ya wananchi wa pande zote mbili.

Waziri Mhagama, akiambatana na Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mhe. Agnes Kayola, pamoja na ujumbe wake, amemshukuru Rais Chakwera kwa mapokezi mazuri na kusisitiza kuwa Rais Samia anathamini na kutambua umuhimu wa kudumisha uhusiano mzuri wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Malawi.

Aidha, amebainisha kuwa ushirikiano huo unaleta manufaa makubwa kwa wananchi wa mataifa yote mawili.

No comments:

RAIS SAMlA AFANYA MAZUNGUMZO NA MJUMBE MAALUM WA RAIS TSHISEKEDI

  Dar es Salaam, 26 Machi 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan , amekutana na kufanya mazungu...