Sunday, March 16, 2025

*KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE LAAC YAWASILI IRINGA.

   









 Kamati ya kudumu ya Bunge ya hesabu za Serikali za Mitaa LAAC, imewasili mkoani Iringa mapema leo kwaajili ya kuanza ziara yake ya ukakuguzi wa miradi ya maendeleo katika Sekta ya Elimu, Afya, Kilimo na uzalishaji mali.     

Akiwasilisha salamu za Serikali kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Iringa, Mkuu wa wilaya ya Iringa Komred Kheri James ameikaribisha kamati hiyo na ameihakikishia ushirikiano na utayari wa kupokea na kufanyia kazi maoni, Ushauri na maelekezo yote yatakayo tolewa na kamati hiyo.                                            

Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge LAAC Mheshimiwa Halima James Mdee, ameeleza kuwa Kamati hiyo ikiwa Mkoani Iringa itatembelea Halmashauri ya Kilolo, Manispaa ya Iringa na Halmashauri ya wilaya ya Mufindi.                                                 

 *#Iringa Imara, Tutaijenga kwa Umoja na Uwajibikaji.*

No comments:

NAIBU WAZIRI WA FEDHA AMWAKILISHA WAZIRI WA FEDHA KATIKA KONGAMANO LA 16 LA MWAKA LA WATAALAM WA UNUNUZI NA UGAVI – ARUSHA

Naibu Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Mhandisi Mshamu Ali Munde, amemwakilisha Waziri wa Fedha katika ufunguzi wa Kongamano la 16 la Mwaka la Wa...