Viongozi mbalimbali wamewasili katika kilele cha Wiki ya Maji, sambamba na Uzinduzi wa Sera ya Maji ya Mwaka 2022 (Toleo la 2025), hafla inayofanyika leo Machi 22, 2025, katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.
Mgeni rasmi katika tukio hili ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye ataongoza uzinduzi wa sera hiyo muhimu kwa maendeleo ya sekta ya maji nchini.
Tukio hili linahudhuriwa na viongozi wa Serikali, wadau wa sekta ya maji, wanazuoni, na washirika wa maendeleo, wakijadili mustakabali wa usimamizi na matumizi endelevu ya rasilimali za maji kwa ustawi wa Taifa.
📸 Picha na: Emmanuel Mbatilo
#WikiYaMaji2025 #SeraYaMaji #MajiNiUhai #SamiaSuluhuHassan
No comments:
Post a Comment