Hebu cheki wananchi wa Mto Kizinga wanavyopata shida kuweza kupita kwenda au kurudi kutoka kwao Mbagala ni karaha kubwa mno, jana jeshi la polisi lilimwaga askari wake katika daraja la Mto Kizinga lililopo Mtongani jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kudhibiti vibaka walioanza kutumia fursa ya adha ya kuvuka mto huo kuwapora watu mali zao.
Daraja la mto Kizinga limefunikwa na maji baada ya mvua kubwa iliyonyesha juzi maeneo ya Kisarawe hali ambayo imewalazimisha watu kuvuka mto huo kwa miguu baada ya magari kushindwa kupita.
Vibaka hao walikuwa wakijibanza pembeni mwa daraja hilo lilofunikwa na maji na kuwapora watu wanaopita eneo hilo kwa miguu vitu mbalimbali na kusababisha uvunjifu wa amani.
Polisi hao wamemwagwa eneo hilo baada ya malalamiko kadhaa ya watumiaji wa njia hiyo kutaka polisi wadhibiti vitendo hivyo kwa ulinzi wa silaha.
“Kwa kweli hali ilikuwa mbaya sana katika daraja hili tulikuwa hatupiti kwa raha yaani Jana na juzi ikifika saa moja asubuhi au jioni hujavuka katika daraja hili basi ujue lazima utakabwa,” alisema Irene John wakati akiongea na Mwananchi na kuongeza kuwa
“Jana mama mmoja alikuwa akipita eneo hili alipigwa na kuporwa pochi pamoja na simu na vibaka na polisi walifika mara moja na kumkamata tunashukuru kwani polisi wamefika na hali ni shwari kabisa hakuna tena matukio ya uporaji” . Habari imeandikwa na Christina Kabadi.
Comments