Jupiter, Venus, mwezi zakutana


VITU vitatu jana vilikuwa viking'aa angani vikiwa vimejipanga pamoja; ni sayari za Jupite na Venus ambazo ziliuzunguka mwezi uliokuwa ukionekana kama mithili ya ukucha uliokatwa.

Ni tukio lisilo la kawaida kutokea, lakini hutokea kila baada ya miaka kadhaa. Baada ya tukio la jana, sayari hizo na mwezi zitakaribiana tena Novemba 18 mwaka 2052.

Jupiter na Venus zilianza kusogea kuelekea karibu na mwezi juzi jioni na ilipofika jana zilionekana zikiwa umbali wa digrii 2, ambazo ni sawa na kidole kilichonyooshwa kwenye mkono, anasema Alan MacRobert, mhariri mwandamizi wa jarida la Sky and Telescope alipoongea na AP.

Tofauti na hali inavyokuwa wakati jua likikamatwa na mwezi, jana haikuhitaji kiona mbali kushuhudia tukio hilo kutokana na vitu hivyo vitatu kutoa mwanga mkali, mwezi ukionekana kuwa mkubwa zaidi na kufuatiwa na Jupiter, ambayo ilionekana upande wa kushoto, huku Venus ikionekana kuwa ndogo kuliko zote.

Comments

Subi Nukta said…
Lazima wanajimu na wabashiri watakuwa na maelezoya jinsi hali hii inavyoathiri hali ya anga na maisha ya watu.
Asante kwa habari!