Miaka 47 ya uhuru wa tanzania




MAMA Maria Nyerere na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, jana walikuwa kivutio katika maadhimisho ya Sherehe za Uhuru yaliyofanyika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam baada ya kushangiliwa na umati wa watu waliohururia sherehe hizo huku viongozi wengine wakiingia kimya kimya.

Kitendo cha wananchi kuwashangilia viongozi hao kwa nderemo na vifijo bila hata kuhamasishwa ilileta utofauti mkubwa kati yao na Rais Jakaya Kikwete ambaye alishangiliwa na baadhi ya makundi hasa baada ya kutangaziwa na mwongoza sherehe.

Akitangaza wakati msafara wa rais unakaribia kuingia uwanjani huku watu wakiwa kimya, mwongoza sherehe huyo alisema: “Mabibi na mabwana tunayemtarajia kuingia uwanjani hivi sasa ni Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Jakaya Kikwete, hivyo atakapoingia uwanjani ninaomba tumshangilie kwa nguvu zetu zote.”

Hata hivyo, muda mfupi baada ya tangazo hilo Rais Kikwete akaingia uwanjani kwa kutumia geti kubwa na kuzunguka uwanja akiwa katika gari la wazi la Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), ndipo makundi hayo yakijaribu kushangilia kwa sauti ya chini huku baadhi yao wakipeperusha bendera ya Taifa.

Comments