Msanii kutoka nchini Marekani Kat De Luna usiku wa kuamkia leo alikonga nyoyo za wabongo katika tamasha kubwa la Fiesta 2008’ Jirambe’ baada ya kupiga shoo ya kufa mtu na kuwafanya wanazi wa burudani waliokuwa wamefurika katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam kumshangilia muda wote. Vibao vyake vya Am I Dream’ng na Run the Show ndivyo vilivyowadatisha wengi na kuwafanya mashabiki hao kuimba naye sambamba.
Sambamba na mwanadada huyo, pia kijana kutoka Dodoma ‘East Zuu’ Albert Mangwea ‘Ngweair’ akiwa sambamba na msela wake Mchizi Mox waliwakimbiza vilivyo mashabiki. Wasanii wengine waliokamua ni Ali Kiba, Mr.Blue, Profesa Jay, Nakaaya,Q Jay, Q Chief, Mwasiti, J-Moe, Bushoke, makundi ya TMK Wanaume Family na Halisi, bendi ya FM Academia ‘Wazee wa ngwasuma’ na wengine kibao waliofanya mashabiki kujiramba.
Comments