MWAKILISHI wa Tanzania katika mashindano ya Miss Earth, Miriam Odemba ameibuka mshindi wa nafasi ya pili katika kinyangíanyiro hicho kilichofanyika Jumapili usiku kwenye ukumbi wa Clark Expo Amphitheater, Angeles City, Pampanga nchini Philippines.
Hii ni mara ya kwanza tokea kuanzishwa kwa mashindano hayo kwa Mtanzania kumaliza katika nafasi ya juu na ni mara ya pili katika Afrika kushika nafasi hiyo ya juu kabisa katika mashindano hayo.
Nyota ya Odemba ilianza katika mashindano ya awali ambapo alifanikiwa kutwaa tuzo ya Miss Aficionado. Ameibuka mshindi wa kipengele cha masuala ya mazingira kinachohusu hali ya hewa.
Mrembo wa Kenya, Winfred Omwakwe alishinda taji la Miss Earth mwaka 2002 mjini Manila na kuweka historia kuwa msichana wa kwanza kutwaa taji hilo duniani.
ìNina furaha kubwa kutwaa nafasi hii, niliandaliwa kushinda na nimeshinda, namshukuru Mungu na pia mwandaaji wangu, Sarungi (Maria) kwa kunipa nafasi hii ya kuiwakilisha taifa na kufanikiwa kutwaa nafasi hii, nawashukuru Watanzania wote walionipa sapoti kubwa kabla ya mashindano,î alisema Odemba kwa njia ya simu jana baada ya kuisha kwa mashindano hayo.
Alisema kuwa ushindi huo ni sifa kwake, kwa Kampuni ya Compass Communication chini ya Maria Sarungi na Tanzania nzima kwani lengo lilikuwa kuipromoti Tanzania nje ya mipaka na lengo limetiamia.
Kwa mujibu wa Odemba, mashindano hayo yalikuwa magumu sana na alijitahidi na kutumia uwezo wake wa kimataifa kufanya vyema.
Katika mashindano hayo, mrembo wa Philippines Karla Henry, 22, alifanikiwa kutwaa taji hilo kwa kuwashinda warembo 84 kutoka nchi mbalimbali duniani.
Miss Mexico, Abigail Elizalde alishinda nafasi ya tatu wakati ya nafasi ya nne ilichukuliwa na mrembo wa Brazil, Tatiane Alves.
Warembo nane bora wa mashindano hayo ni Mariana RodrÌguez (Colombia), Adriana ReverÛn (Hispania), Nasanin Nuri (Uswisi) na Daniela Torrealba wa Venezuela.
Warembo 16 bora wa mashindano hayo ni Hana Svobodov· (Jamhuri ya Czech), Seo Seol-hee (Korea), Uko Ezinne (Nigeria), Karolina Filipkowska (Poland), Ruxandra Popa (Romania), Anna Mezentseva (Russia), Piyaporn Deejing (Thailand), Jana Murrell (Marekani)
Habari hii ni kwa mujibu wa Majuto Omary wa The Citizen
Comments