Wednesday, November 12, 2008

Chuo Kikuu watimuliwa









UONGOZI wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kampasi ya Mlimani umewasimamisha masomo wanafunzi wa shahada za kwanza kwa muda usiojulikana.

Hatua hiyo imekuja baada ya wanafunzi hao kukaidi amri ya chuo pamoja na ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Prof Jumanne Maghembe, iliyowataka kusitisha mgomo na kurudi madarasani wakati wizara ikishughulikia madai yao.

Kufuatia hatua hiyo, Rais wa Serikali ya wanafunzi wa chuo hicho, Anthony Machibya, aliwatangazia wanafunzi wenzake juu ya kusimamishwa huko na kusisitiza kuwa, pamoja na kufukuzwa chuoni hapo, lakini watakaporudi wataendeleza harakati za kudai haki yao mpaka watakapoipata.

No comments:

NGORONGORO YATOA ELIMU YA UHIFADHI SHIRIKISHI NA KUHAMASISHA UTALII MASHULENI

  Na Mwandishi Wetu, Karatu Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro imeendelea na programu ya kutoa elimu ya uhifadhi shirikishi na kuhamasiha utal...