Tuesday, June 12, 2007

Kwa mtaji huu, tunaelekea kwenye utawala wa kifalme-2

NIMELAZIMIKA kuendeleza mjadala huu kutokana na mwitikio mkubwa wa wasomaji wetu wa safu hii ya siasa. Wiki iliyopita, nilizungumzia kwa kina kuhusu namna ambavyo watoto wa maskini na au maskini wenyewe wazazi au wao walivyo na fursa ndogo ya kuweza kupata madaraka katika chama na au serikali.

Nimefurahi kwamba wapo wengi ambao walikuwa na mtazamo kama wangu, yaani wa kupinga mifumo inayowafanya nafasi watoto wa vigogo na watu wengine wenye uwezo kuwa na uwezekano mkubwa wa kunyakua madaraka ya uongozi kwa hali yoyote ile na hivyo kuwanyima fursa wale wasio nacho hata kama wana uzoefu au uwezo mkubwa.

Nimefurahi, pia kwamba wapo watu wengine wenye mitazamo inayoafiki kwamba wao ndiyo wao, ndio wateule na kwamba eti kwa sababu watoto wao wamezaliwa katika siasa, basi wataendelea kuwa wafalme wa siasa, daima dawamu hadi dunia hii inakwisha.

No comments:

RC ARUSHA APOKEA UJUMBE WA MABUNGE DUNIANI (IPU)

  . Kufanya Mkutano wa Mabunge Mkoani Arusha  .Wajumbe zaidi ya 1500 kutoka nchi wanachama wa IPU kuhudhuria  . Rais Dkt. Samia apendekezwa ...