Pichani unaweza kuona aerial view ya uwanja mpya wa taifa wa michezo wa Dar es Salaam ambao wazo lake lilichipukia toka kwa Rais Mstaafu Benjamin Mkapa na sasa unakamilika chini ya utawala wa Jakaya Mrisho Kikwete sijui watauitaje?? Picha ya Fredrick Felix.
Saturday, June 30, 2007
Uwanja mpya wa Taifa
Pichani unaweza kuona aerial view ya uwanja mpya wa taifa wa michezo wa Dar es Salaam ambao wazo lake lilichipukia toka kwa Rais Mstaafu Benjamin Mkapa na sasa unakamilika chini ya utawala wa Jakaya Mrisho Kikwete sijui watauitaje?? Picha ya Fredrick Felix.
Uwanja mpya wa Taifa
Mambo ya Uwanja Mpya
Wednesday, June 27, 2007
Buriani Amina Chifupa

Mheshimiwa Amina Chifupa hatunaye tena, kwa mujibu wa baba yake Amina, Mzee Hamis Chifupa, bintiye alikutwa na mauti saa tatu kasorobo usiku katika Hospitali ya Jeshi ya Lugalo alikokuwa amelazwa. Kifo chake kimepokelewa kwa hisia mbalimbali na watu wa rika tofauti nchi nzima.

Medy Mpakanjia analia.

Gari iliyobeba mwili wa Amina.
Kwaheri Amina Picha hii imepigwa na Mpoki Bukuku.
RATIBA YA MAZISHI ILIYOPATIKANA NYUMBANI KWA MZEE CHIFUPA
MIKOCHENI ENEO LA TPDC ZINASEMA...
Mazishi yatafanyika Kesho, Kijijini Kwao Luhanjo, Lupembe, Njombe Mkoani Iringa, Ngugu, jamaa na Marafiki wanaotaka kuhudhuria Mazishi hayo kutoka Dar es salaam Wanatakiwa Kutoa Mchango wa Tshs 40,000/= Ili waondoke kwa Msafara wa Pamoja! Dk. Tamba ndo Mweka hazina wa kamati ya Mazishi na ndo anapokea Michango hiyo ya tshs. 40,000/= kwa Kila mmoja kama nauli ya kwenda na Kurudi Mazishini!
Taarifa hizi kwa mujibu wa Ngowi au Michuziutapata taarifa za kina.
Mola ailaze pema Roho ya Mpendwa wetu Amina Chifupa- Amina.
Tuesday, June 26, 2007
Saturday, June 23, 2007
Sio Geneva Wala nini ni Kijenge
Mlima Meru uleee
KITUO CHA KIMATAIFA CHA MIKUTANO (AICC)
Mnara wa Saa A Town
Sky Scrapper yetu ya PPF
Watoto wa Tanzania
Watoto wa Tanzania miongoni mwao wakiwa hawa wamewekewa mkakati gani wa kuwafanya waishi katika usawa bila ubaguzi, bila matabaka kama tulivyokuwa wazazi wao. Hivi sasa mali zote zinauzwa si misitu, madini yetu yote na kila rasilimali ipo siku watoto hawa wenye taifa lao watakuja kuuliza hivi wazazi tulikuwa wapi?
Saturday, June 16, 2007
Miwaa
Changamoto na Utekelezaji wa Mizani Mpya: Tathmini ya Mizani ya Kibaha, Himo na Mikumi
Lengo la kuanzisha mizani katika maeneo mbalimbali nchini lilikuwa kuhakikisha udhibiti wa uzito wa magari makubwa ili kulinda miundombinu ya barabara na kuimarisha usalama wa usafirishaji. Hata hivyo, changamoto zinazoonekana katika mizani hii, hasa ile ya Kibaha, Himo, na Mikumi, zinaonyesha kuwa kazi bado ni kubwa katika kuhakikisha ufanisi wake.
Mizani hii imekuwa na shughuli pevu kutokana na msongamano wa magari, ucheleweshaji wa huduma, na changamoto za kiutendaji. Madereva wengi wamekuwa wakilalamikia muda mrefu wa kusubiri kupimwa, hali inayosababisha ucheleweshaji wa safari zao. Aidha, baadhi yao wanadai kuwa mifumo ya mizani haijaboreshwa ipasavyo, jambo linaloweza kusababisha mkanganyiko katika vipimo vya uzito wa magari yao.
Katika mizani ya Kibaha, kutokana na kuwa lango kuu la kuingilia Dar es Salaam, msongamano wa magari ni mkubwa, jambo linalohitaji maboresho ya haraka katika taratibu za upimaji ili kupunguza foleni na kuongeza ufanisi. Mizani ya Himo, ambayo inahudumia magari mengi yanayokwenda mikoa ya kaskazini na hata nje ya nchi, pia inakumbwa na changamoto kama hizo. Wakati huohuo, mizani ya Mikumi, ambayo ni lango muhimu kwa magari yanayotoka na kuingia Nyanda za Juu Kusini, inakabiliwa na tatizo la upungufu wa vifaa vya kisasa vya kupimia uzito, jambo linaloathiri utendaji wake.
Ili kuhakikisha mizani hizi zinafanya kazi kwa ufanisi, hatua zinahitajika kuchukuliwa ili kuboresha mifumo ya upimaji, kuongeza vifaa vya kisasa, na kuweka utaratibu bora wa kuhudumia madereva kwa haraka. Serikali na mamlaka husika zinapaswa kushirikiana na wadau wa sekta ya usafirishaji ili kuboresha hali hii kwa manufaa ya wote.
Safari ya Arusha
Tuesday, June 12, 2007
Kwa mtaji huu, tunaelekea kwenye utawala wa kifalme-2
Nimefurahi kwamba wapo wengi ambao walikuwa na mtazamo kama wangu, yaani wa kupinga mifumo inayowafanya nafasi watoto wa vigogo na watu wengine wenye uwezo kuwa na uwezekano mkubwa wa kunyakua madaraka ya uongozi kwa hali yoyote ile na hivyo kuwanyima fursa wale wasio nacho hata kama wana uzoefu au uwezo mkubwa.
Nimefurahi, pia kwamba wapo watu wengine wenye mitazamo inayoafiki kwamba wao ndiyo wao, ndio wateule na kwamba eti kwa sababu watoto wao wamezaliwa katika siasa, basi wataendelea kuwa wafalme wa siasa, daima dawamu hadi dunia hii inakwisha.
Sunday, June 03, 2007
Mpango wa njia tatu Dar ufutwe, haufai

Barabara ya Morogoro.
WIKI hii tumeshuhudia utekelezwaji wa maamuzi makubwa na ya haraka haraka mno ambayo kwa upande mmoja yanaweza kuonekana kama ni ukombozi kwa watu wengine, lakini kwa upande mwingine ni kero na tatizo kubwa zaidi kwa raia wa taifa hili walioko jijini Dar es Salaam.
Hii inafuatia utekelezwaji wa amri ya Waziri Mkuu Edward Lowassa, aliyetaka kumalizwa kwa tatizo la msongamano wa magari jijini Dar es Salaam na hivyo kuchukuliwa maamuzi ya haraka haraka ya kuanza kutumika kwa njia nyingine ya ziada kwa magari yanayokwenda na au kurudi mjini wakati wa asubuhi na jioni.
Sikatai kwamba ili kifanyike kitu kikubwa, ni lazima kufanya maamuzi magumu, lakini kwa mantiki ya sasa uamuzi huu mgumu hauna manufaa makubwa kuliko hasara zilizopo. hapa
Kwa mtaji huu, tunaelekea kurudi kwenye utawala wa kifalme
HATA kama hatutaki, basi hivi ndiyo ilivyo, pia ndivyo ilivyojengwa ikafanyiwa mikakati ya makusudi na kama haikemewi haitabadilika, tunaelekea kunako utawala wa familia, utawala wa kifalme wa baba kumwachia mwana na mwana, mke na hadi mjukuu au mkwe na mzunguko unabakia kuwa ule ule.

*WATAFITI WA MIMEA VAMIZI WATUA SERENGETI
Na Sixmund Begashe - Serengeti Ziara ya kikazi ya watafiti wa mimea vamizi kutoka Jamhuri ya Cuba walioungana na wataalam wa ikolojia kutok...

-
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu na timu ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwa katika ...
-
(Picha na Yahya Charahani) Kwa wale waliokulia maeneo haya, hili ni jambo la kawaida ukitoka mjini, shambani sijui hadi wapi kote ni haya h...
-
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2014 EXAMINATION RESULTS ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA ...