Wednesday, September 30, 2015
MO KUANZISHA BENKI YA MIKOPO KWA WAFANYABISHARA WADOGO NCHINI
CEO wa Kampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji akiwa ofisini kwake.
………………………………………..
Na Modewjiblog team
Mfanyabiashara Bilionea Mohamed Dewji ambaye hivi karibuni amepata tuzo ya Mfanyabiashara Bora wa Afrika wa mwaka 2015, katika kinyang’anyiro cha tuzo za wafanyabiashara bora wa Afrika (African Business Awards 2015) amebainisha kuwa lengo kuu la kampuni anayoiongoza ya MeTL Group, hadi kufikia mwaka 2022, ni kufikia dola bilioni 5 huku akitarajia kuajiri wafanyakazi zaidi ya Laki moja.
Dewji maarufu kama MO amebainisha hayo wakati wa mahojiano maalum ya moja kwa moja yaliyorushwa hivi karibuni na kituo cha BBC kupitia kipindi cha BBC SWAHILI DIRA YA DUNIA ambapo alibainisha hayo.
Kupitia kipindi hicho cha BBC Swahili, MO aliweza kuelezea mafanikio aliyofikia ikiwemo siri ya kufanya kazi kwa bidii na kujituma.
Ambapo ameeleza kuwa, alianza biashara akiwa mdogo sana kwani wakati huo Baba yake alikuwa akimfundisha kazi na yeye kujituma zaidi bila kuchoka.
Aidha, MO amebainisha kuwa, yupo mbioni kuanzisha Benki ya kuweza kutoa mikopo midogo kwa wafanyabiashara wadogo wadogo kujiendeleza.
Salim Kikeke aliweza kumuuliza swali juu ya vijana wengi wanapenda kufanyabiashara lakini hawana mitaji ambapo MO alifunguka kuwa:
“Unajua na mimi mwenyewe nataka kuanzisha ‘Micro credit bank’, ya kuweza kutoa mikopo midogomidogo kwa wafanyabiashara wadogo. Kwa sasa hivi kuna benk nyingi sana zimezidi ukilinganisha mwaka 1998, nilipotoka Marekani, benki zilikuwa ndogo sana kwa hiyo nimeanza kutafuta pesa kutoka benki za Afrika Kusini” ameeleza MO na kuongeza kuwa mtu unapokuwa na wazo la kuanzisha biashara unaweza kushirikiana na mwenye pesa ama kukopa kwa mtu mwenye pesa. alifafanua MO .
Katika mahojiano hayo, MO alibainisha kuwa, mapato katika akaunti ya MeTL GROUP ina kiasi cha dola bilioni 1.3 huku akiwa ameajiri watu zaidi ya 24,000 huku lengo hadi kufikia mwaka 2022, kuwa na wafanyakazi zaidi ya Laki moja huku mapato kuwa zaidi ya dola bilioni 5.
Tuzo aliyopata MO alikabidhiwa katika hafla hiyo iliyofanyika katika hoteli ya Four Season mkabala na jengo la Umoja wa Mataifa (Baraza Kuu) watu wengine waliopata tuzo ni Aliko Dangote, Daphne Mashile Nkosi, Strive Masiyiwa na Helen Hai.
MO alimshinda Aliko Dangote ambao walikuwa kwenye Kategori moja wakiwania tuzo hiyo ya mfanyabiashara bora wa Afrika, huku wengine walioshindanishwa kwenye kategori hiyo ni CEO wa Paramount Group, Ivor Ichikowitz, CEO wa Groupe Loukil, Groupe UADH, Bassem Loukil, na Oscar Onyema DG wa Nigerian Stock Exchange.
RAIS KIKWETE ATOA HOTUBA YAKE YA MWISHO UMOJA WA MATAIFA NEW YORK
MSAFARA WA LOWASSA WASIMAMISHWA ZAIDI YA MARA NNE WAKATI AKIWA SAFARINI KUTOKEA JIJINI TANGA KUELEKA DAR
Msafara wa Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, ukichanja mbuga kutokea jijini Tanga kuelekea jijini Dar es salaam mapema leo asubuhi.
Sehemu ya wananchi wa Mji wa Muheza Mkoani Tanga, wakiwa wamefunga barabara, wakimtaka Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, azungumze nao jana Septemba 29, 2015, wakati akiwa safarini kwa kuelekea jijini Dar es salaam kwa njia ya barabara akitokea Mkoani Tanga.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akimnadi kwa wananchi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Muheza wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Ilikuwa ni furaha kwa kila aliemuona Mh. Lowassa alipokuwa akizungumza nao.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwapungia wananchi wa Mji wa Muheza Mkoani Tanga, mara baada ya kuzungumza nao, wakati akiwa safarini kwa kuelekea Dar es salaam kwa njia ya barabara akitokea Mkoani Tanga.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwasili kwenye Uwanja wa Chuo cha Walimu Korogwe, Mkoani Tanga kulikofanyika Mkutano wa Kampeni zake jana Septemba 29, 2015.
Waziri Mkuu wa zamani, Mh. Fredrick Sumaye akiwahutubia wananchi wa Mji wa Korogwe, katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Chuo cha Walimu Korogwe, Mkoani Tanga jana Septemba 29, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Korogwe, Mkoani Tanga, wakati wa Mkutano wa Kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Chuo cha Walimu Korogwe, Mkoani Tanga leo Septemba 29, 2015.
NAMELOK SOKOINE AZINDUA KAMPENI ZA UBUNGE MONDULI AHIDI KUENDELEZA ALIPOISHIA LOWASSA
MGOMBEA jimbo la Monduli kupitia Chama Cha
Mapinduzi (CCM), Namelok Sokoine, akihutubia mkutano wa hadhara wakati wa
uzinduzi wa kampeni zake zilizofanyika katika viwanja vya Nanja Mnadani Monduli
mkoani Arusha Septemba 28,2015 ambapo pamoja na mambo mengine ameahidi
kuendeleza yote aliyoasisi, kusimamia na kutekeleza aliyekuwa mbunge wa jimbo
hilo, Edward Lowassa.
Mapinduzi (CCM), Namelok Sokoine, akihutubia mkutano wa hadhara wakati wa
uzinduzi wa kampeni zake zilizofanyika katika viwanja vya Nanja Mnadani Monduli
mkoani Arusha Septemba 28,2015 ambapo pamoja na mambo mengine ameahidi
kuendeleza yote aliyoasisi, kusimamia na kutekeleza aliyekuwa mbunge wa jimbo
hilo, Edward Lowassa.
Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Asha-Rose Migiro akihutubia mkutano wa uzinduzi wa Kampeni za Mgombea Ubunge wa Jimbo la Monduli Mkoani Arusha kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Namelok Sokoine.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Monduli kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Namelok Sokoine akihutubia wananchi katika mkutano huo wa hadhara wa uzinduzi wa kampeni zake.
Namelok Moringe Sokoine akiwasili katika uwanja huo wa Nanja tayari kwa uzinduzi wa kampeni.
Wazee wa Kimila wa Jamii ya Kimaasai wa Monduli wakiongoza dua maalim ya kumuombea Binti yao Namelok.
Mwalimu Lorinyu Nkoosi, mmoja wa waliochuana na Namelok Sokoine katika mchakato wa uteuzi ndani ya CCM akiongea.
Wananchi wa Monduli wakiwa katika mkutano huo.
Wajane
wa Waziri Mkuu wa Zamani wa Tanzania, Edward Moringe Sokoine ambao ni
mama za Namelok Sokine wakitambulishwa mkutanoni hapo na Mwenyekiti
wa kamati ya kampeni za CCM jimbo la Monduli, Paul Kiteleki.
wa Waziri Mkuu wa Zamani wa Tanzania, Edward Moringe Sokoine ambao ni
mama za Namelok Sokine wakitambulishwa mkutanoni hapo na Mwenyekiti
wa kamati ya kampeni za CCM jimbo la Monduli, Paul Kiteleki.
Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Asha-Rose Migiro (kulia) akimkabidhi ilani ya Chama cha Mapinduzi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Monduli Mkoani Arusha kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Namelok Sokoine wakati wa uzinduzi wa jkampebni zake uliofanyika Monduli jana.
Dk Asha-Rose Migiro akisalimiana na wamama wa kimaasai alipowasili mkutanoni hapo
Subscribe to:
Posts (Atom)
WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU AMPONGEZA NDEJEMBI, AMSIFIA KWA UADILIFU NA UCHAPAKAZI
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba , amempongeza Mhe. Deogratius John Ndejembi kwa kuaminiwa ...
-
Hapa mmoja wa watoto hao akiwa na kijana mwenzake mwenye miaka 18, wote wako sawa lakini yeye hawezi kuzungumza kama watu wa kawaida. Mama S...
-
Nadhani mtakumbuka kibwagizo maarufu katika TV ambacho kinaimbwa perupe pepero perupe pepero hawa ni vijana wa Sisi Tambala waliokuwapo kati...
-
Mdau Julius Samwel hivi karibuni alikuwa huko Mwanza na hizi ndizo alizofanikiwa kutumegea, wadau hebu someni hicho kibao mniambie kuna nini...
















