Thursday, April 30, 2015

MKUU WA WILAYA YA KINONDONI PAUL MAKONDA, APOKEA VIFAA VYA MICHEZO VYENYE THAMANI YA SH.MILIONI 50 KUTOKA KAMPUNI YA TSN

 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam leo, wakati akipokea msaada wa vifaa vya michezo vyenye thamani ya sh. milioni 50 kutoka Kampuni ya Tanzania Sisi Nyumbani (TSN) wa ajili ya mashindano ya Kinondoni Cup yatakayoanza Juni 2015 katika wilaya hiyo.
 Meneja wa Kinywaji cha Chilly Willy  Kinachosambazwa na Kampuni ya TSN, Khamis Tembo (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhi vifaa hivyo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Smart Sports, George Wakuganda, akizungumza katika mkutano huo baada ya kutoa mipira 50 kwa ajili ya mashindano hayo.
  Meneja wa Kinywaji cha Chilly Willy  kinachosambazwa na Kampuni ya Tanzania Sisi Nyumbani (TSN), Khamis Tembo (wa pili kulia), akimkabidhi jezi na vifaa vya michezo Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda Dar es Salaam leo mchana kwa ajili ya mashindano ya Kinondoni Cup yaliyoanzishwa na Makonda. Anayeshuhudia kushoto ni Meneja Mahusiano na Mawasiliano ya Jamii wa TSN , Koiya Kibanga.
Meneja wa Kinywaji cha Chilly Willy  kinachosambazwa na Kampuni ya Tanzania Sisi Nyumbani (TSN), Khamis Tembo akimvalishe moja ya jezi Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda baada ya kukabidhiwa kwa ajili ya mashindano hayo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Smart Sports, George Wakuganda (kushoto), akimkabidhi DC Makonda mpira mmoja kati ya 50 aliyoitoa kwa ajili ya mashindani hayo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na maofisa kutoka kampuni ya TSN ambayo imetoa msaada wa vifaa hivyo vya michezo. Kutoka kushoto ni Meneja wa Kinywaji cha Chilly Willy  kinachosambazwa na Kampuni ya Tanzania Sisi Nyumbani (TSN), Khamis Tembo,Meneja Mahusiano na Mawasiliano ya Jamii wa TSN Group, Koiya Kibanga, Meneja Masoko na Mauzo wa TSN, Nafsa Soud na Mshauri wa TSN, Francis Bonda ‘Kaka Bonda’
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na maofisa kutoka kampuni ya TSN pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Smart Sports, George Wakuganda (kulia), ambaye ametoa mipira 50 kwa ajili ya mashindano hayo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda akiangalia vifaa hivyo baada ya kukabidhiwa na Kampuni ya TSN pamoja na Kampuni ya Smart Sports  ambayo imetoa mipira 50 kupitia Mkurugenzi wake, George Wakuganda.
…………………………………………………………………..
 
Na Suleiman Msuya
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam, Paul Makonda amepokea msaada wa jezi seti 100 na mipira 50 kutoka kampuni ya Tanzania Sisi Nyumbani (TSN), ambavyo vina thamani ya shilingi milioni 50 kwa ajili ya mashindano ya mpira wa netibali na mpira wa miguu yatakayoitwa Kinondano Cup.
Akizungumzia msaada huo Mkuu wa Wilaya ya Kinondani, Paul Makonda alisema mikakati yake ni kuhakikisha kuwa vijana wa Wilaya hiyo wanatumia vipaji vyao kujikwamua katika umaskini.Makonda alisema mashindano hayo yatakuwa ni mpira wa miguu wanaume na wanawake, mpira wa kikapu wanawake na wanaume na mpira wa netibali ambao ni wanawake pekee.“Nimedhamiria kuhakikisha kuwa jamii inaondokana na dhana kuwa wakazi wa wilaya hiyo ni watumia madawa na uchangudoa na njia sahihi ni kuwahusisha vijana na kutumia vipaji vyao,” alisema.
Akizungumza baada ya kutoa msaada huyo Meneja wa Kinywaji cha Chilly Willy ambacho ndio wametoa mtaasa huo kupitia TSN, Khamis Tembo alisema msaada huo una lengo la kumuunga mkono Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.
Tembo alisema kampuni ya TSN inatambua umuhimu wa michezo hivyo kupitia Chilly Willy wameona ni muhimu kutoa msaada huo wa jezi seti 100 na mipira 50 ili kufanikisha malengo hayo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Smart Sport, George Wakuganda ambaye kampuni yake imetoa mipira 50 alisema wameamua kuungana na Mkuu wa Wilaya kwani wao ni wanamichezo.
Wakuganda alitoa wito kwa wadau wengine kuungana na Mkuu huyo wa Wilaya kwani jitihada zake za kuhakikisha vijana wanatoka katika dibwi la umaskini ni za maana.
(Imeandaliwa na mtandao wa http://www.habarizajamii.com/)

TASWIRA ZA SUNDAY CELEBRATION SEASON 6 YA GWT

Waimbaji wa Glorious Worship Team (GWT) wakilishambulia jukwaa katika Sunday Celebration Season 6.
Kiongozi wa Bendi ya The Jordan, Daniel Mbepera, akiimba kwa hisia sambamba na bendi yake.
Wageni waliohudhuria wakisifu na kuabudu sambamba na GWT.
Mjasiriamali mahiri Afrika na Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers Ltd, Eric Shigongo akitoa somo la ujasiriamali.
Wageni wakisikiliza somo la ujasiriamali kutoka kwa Shigongo.
Waimbaji wa GWT wakizidi kutoa burudani kwa washiriki wa Sunday Celebration Season 6.

KWA mara nyingine, kile Kikundi cha Kusifu na Kuabudu nchini cha Glorious Worship Team (GWT) Jumapili iliyopita kiliendelea na programu yake ijulikano kwa jina la 'Sunday Celebration' ambayo hufanyika kila Jumapili jioni.

Wiki iliyopita ilikuwa ni Sunday Celebration Season 6 ambapo burudani mbalimbali pamoja na elimu ya ujasiriamali vilitolewa kwa watu waliohudhuria katika Ukumbi uliopo Victoria Service Station, Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Burudani ukumbini hapo ziliongozwa na Kundi la GWT likishirikiana na The Jordan Band huku elimu ya ujasiriamali ikitolewa na Mwalimu mahiri wa Ujasiriamali Afrika ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers Ltd, Eric Shigongo.
(PICHA ZOTE NA GWT)

BENKI YA POSTA YAJIVUNIA UTENDAJI BORA KWA MWAKA 2014 ULIYOIPA FAIDA NONO

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB) Sabasaba Kitewita Moshingi, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam juzi wakati wa kutangaza utendaji wa benki hiyo kwa mwaka 2014 ambapo TBP walipata faida ya shilingi 10.28 bilioni kabla ya kodi. Pamoja nae ni Mkurugenzi Fedha, Regina Samakafu (katikati) na Mkurugenzi wa Sheria, Mystica Mapunda Ngongi
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB) Sabasaba Moshingi, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana wakati wa kutangaza utendaji wa benki hiyo kwa mwaka 2014 ambapo TBP walipata faida ya shilingi 10.28 bilioni kabla ya kodi. Katikati ni Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa benki hiyo, Peter Mapigano na kushoto ni Mkurugenzi wa Uendeshaji na Teknolojia , Jema Msuya.
Mkurugenzi wa Mipango wa Benki ya Posta Tanzania (TPB)Bernadethe Joseph Gogadi (kushoto) akifuatilia mkutano huo leo ambapo waandishi wa habari nao walikuwepo kuchukua taarifa kama wanavyoonekana pichani.

Wednesday, April 29, 2015

TANZANITE YAKOSA SOKO HAPA NCHINI KUTOKANA NA WATANZANIA KUTOKUVAA MADINI HAYO

SAM_2162
Kulia Mkurugenzi wa kampuni ya madini ya Moreshine  Gibson A.Kilala akitoa maelezo kwa Waziri wa nishati na madini George  Simbachawene hivikaribuni jijini Arusha mara baada ya Waziri huyo kutembelea banda lao katika maonyesho ya nne ya madini na vito yaliyofanyika katika hotel ya Mount Meru jijini Arusha.
(Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
SAM_2156
Baadhi ya madini
SAM_2163
Mkurugenzi wa kampuni ya madini ya Moreshine  Gibson A.Kilala akimuonyesha Waziri baadhi ya madini yanayopatikana katika kampuni yao
SAM_2160
Waziri wa nishati na madini George  Simbachawene kushoto akipata maelezo mafupi kutoka kwa mfanyakazi wa Moreshine Bw.William Simba
SAM_2161
Waziri wa nishati na madini George  Simbachawene akiangalia madini.
SAM_2159
Waziri wa nishati na madini George  Simbachawene akiangalia baadhi ya madini yanayopatikana katika banda la Moreshine kushoto ni mkurugenzi wa kampuni hiyo Gibson A.Kilala na kulia ni William Simba mfanyakazi wa Moreshine
SAM_2166
Bango la Kampuni ya Moreshine.
SAM_2164
Mkurugenzi wa kampuni ya madini moreshine ya jijini Dar es saalamu  Gibson A.Kilala akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani)
……………………………………………………..
Changamoto ya Watanzania kutokuvaa vito vya thamani vinavyotengenezwa na mawe mbali mbali yanayopatikana hapa nchini  imepelekea madini yakiwamo Tanzanite kukosa soko hapa nchini,Soko la madini haswa tanzanite limekuwa nje ya mipaka ya Tanzania kwa kuwa watanzania hawana desturi ya kuvaa madini hayo
Akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni jijini Arusha mkurugenzi wa kampuni ya madini moreshine ya jijini Dar es saalamu Gibson A.Kilala alisema kuwa kutokuwepo kwa utamaduni huo miongoni mwa watanzania kumepelekea soko la madini kupatikana nje ya nchi badala ya hapa nchini ambapo yanapatikana.
Aidha ameiomba serikali kuweza kusajili kampuni ambayo itasaidia kusafirisha madini kama zilizo kampuni nyingine za kusafirishia mizigo hapa nchini kama {DHL)ili kuwawezesha wafanyabiashara kusafirisha mizigo yao kwa usalama zaidi kama zilivyo nchi za jirani kama Kenya.
Hata hivyo ameiomba serikali kuondoa changamoto ya mipaka kwa wafanyabiashara wa madini kwa kuwaruhusu kufuata madini yalipo badala ya kusubiria brokers hali ambayo inawagharimu muda mwingi lakini pia gharama kuongezeka.
Amesema ni vyema wafanyabiashara wakaruhusiwa kwa leseni zao kufuata madini yalipo ili kuwawezesha kufikia migodini tofauti na sasa ambapo leseni zao haziruhusu kufuata madini yanapopatikana badala yake kusubiria broker wawaletee.

BALOZI WA UMOJA WA AFRIKA AMINA SALUM ALI- ATOA RAMBI RAMBI KWA KIFO CHA BRIGEDIA JENERALI HASHIM MBITA

Balozi Amina Salum Ali
 …………………………………………
Na mwandishi wetu Washington, DC
Balozi wa kudumu wa Umoja wa Afrika, Mhe. Amina Salum Ali leo ametoa salamu za rambi rambi kwa Brigedia Jenerali mstaafu Hashim Mbita aliyefariki siku ya siku ya Jumapili April 26, 2015 asubuhi na kuzikwa siku ya Jumanne April 28, 2015 katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Balozi Amina Salum Ali alisema amepokea kwa majonzi na simanzi kubwa taarifa za kifo cha mmoja wa watumishi wa miaka mingi wa Serikali, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (TPDF), aliendelea kwa kusema Brigedia Jenerali msataafu Hashim Mbita atakumbukwa Tanzania, bara nzima la Afrika na dunia kwa jumla kama mmoja wa makamanda mahiri aliyeshiriki kikamilifu katika uondoshaji wa utawala wa ukoloni barani Afrika, hususan utawala wa kidhalimu wa makaburu Zimbabwe na Afrika ya Kusini na hatimaye kuachiwa huru kwa aliyekuwa Rais mzawa wa kwanza nchini Afrika Kusini, hayati Nelson Mandela.
Mzee Mbita alijitoa mhanga kuongoza mapambano ya ukombozi wa Afrika, Atakumbukwa milele kwa kurudisha heshima ya Muafrika.
Brigedia Jenerali msataafu Hashim Mbita ni mfano uliotukuka kwa watanzania na Afrika.Aliiongoza vizuri sana kamati ya ukombozi ya Umoja wa Afrika Mungu amlaze pema peponi, Amin.
 
Balozi Amina Salum Ali yupo safarini kuelekea Tanzania.

PINDI CHANA ATEMBELEA KITUO CHA KULELEA WATOTO.

1
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Mheshimiwa Dkt. Pindi Chana akisisitiza jambo wakati akiongea na watoto pamoja na walezi wa kituo cha Malezi na Makuzi ya Watoto cha Mtambani, Mlandizi wilaya ya Kibaha mkoa wa Pwani.
(Picha zote na Hassan Mabuye)
3 
Baadhi ya watoto wa kituo cha Malezi na Makuzi ya Watoto cha Mtambani wakiwa katika kikao hicho.
5
 Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Mheshimiwa Dkt. Pindi Chana akisisitiza jambo wakati akiongea na wanachuo cha Maendeleo ya Wananchi Kibaha.
4
Wanachuo cha Maendeleo ya Wananchi Kibaha pamoja na viongozi mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Mheshimiwa Dkt. Pindi Chana.
………………………………………………..
Na Hassan Mabuye 
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Mheshimiwa Dkt. Pindi Chana amefanya ziara ya kutembelea kituo cha kulelea Watoto Wilayani Kibaha mkoa wa Pwani kwa lengo la kuangalia maeneo ambayo yanahitaji maboresho pamoja na kujionea hali halisi ya uendeshaji wa vituo vya kulelea Watoto.
Katika ziara hii Mheshimiwa Naibu Waziri alitembelea kituo cha Malezi na Makuzi ya watoto Kilichopo katika kata ya Mtambani Mlandizi jumatatu tarehe 27 Aprili 2015, ambapo aliongea na Walezi na wasimamizi kukienzi na kukitunza kituo hicho. Aidha Mheshimiwa Pindi Chana amewahusia wasimamizi na wazazi kuyapa kipaumbele mambo yanayohusu Watoto kuanzia kwenye familia na kuyaweka katika bajeti za kila siku za familia kwani taifa la kistaarabu linajengwa kuanzia kwa watoto wadogo.
Mheshimiwa Naibu Waziri alifanikiwa pia kukutana na wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kibaha ambapo aliwahusia vijana kuzingati masomo yao wakati wazazi bado wana nguvu za kuwasomesha. “Unadhani siku hizi ukikimbia shule au kutoroka masomo unamkomoa nani, mzazi au mwalimu? Unajikomoa mwenyewe sababu baadae wewe ndo utabeba majukumu na pengine ndio utakuwa mzazi na maisha ya sasa ni elimu na ujuzi” alisisitiza Mhe. Pindi Chana.
Aidha Mheshimiwa Pindi Chana katika ziara hii  alikutana na vikundi vya Wanawake walionufaika na mikopo inayotolewa na Benki ya Wanawake Tanzania eneo la Picha ya Ndege Kibaha.

Waziri Mkuu azindua boti mbili za doria na uokozi

Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba ametoa siku 14 kwa wizara na taasisi zinazohusika na Kituo cha Kitaifa cha pamoja cha Oparesheni zipeleke w...