Friday, July 31, 2026

Rais Samia Aelekea Angola, Akutana na Mama Maria Nyerere Kabla ya Safari ya Kihistoria






Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya mazungumzo na Mama Maria Nyerere muda mfupi kabla ya kuanza safari yake kuelekea Luanda, Angola, ambako anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika hafla ya uzinduzi wa Hospitali iliyopewa jina la Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, tarehe 31 Julai, 2026.

Ushiriki wa Rais Samia katika hafla hiyo unaendelea kuenzi mchango mkubwa wa Mwalimu Nyerere katika harakati za ukombozi wa Bara la Afrika na kuimarisha uhusiano wa kindugu na kidiplomasia kati ya Tanzania na Angola.

Uzinduzi wa hospitali hiyo ni ishara ya heshima na urithi wa kudumu wa falsafa, uongozi na mchango wa Mwalimu Nyerere, ambao unaendelea kutambuliwa na kuthaminiwa ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.

No comments:

Rais Samia Aelekea Angola, Akutana na Mama Maria Nyerere Kabla ya Safari ya Kihistoria

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan , amefanya mazungumzo na Mama Maria Nyerere muda mfupi kabla ya kuan...