Tuesday, August 05, 2025

MKUU WA MKOA WA DODOMA AIPONGEZA TUME YA MADINI KATIKA MAONESHO YA NANE NANE







Dodoma, Agosti 5, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, ametembelea Banda la Tume ya Madini katika Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma na kuipongeza Tume  kwa kazi nzuri ya kuelimisha na kuhamasisha umma kuhusu fursa zilizopo katika Sekta ya Madini.

Akizungumza baada ya kutembelea banda hilo, Mhe. Senyamule amesema kuwa Tume ya Madini imekuwa mfano bora wa taasisi za umma zinazotekeleza majukumu yake kwa ufanisi, hususan katika kuonesha kwa vitendo namna Sekta ya Madini inavyoweza kuchangia maendeleo ya kiuchumi kwa wananchi na taifa kwa ujumla.

“Nawapongeza sana kwa kazi kubwa mnayoifanya. Mnaendelea kuwaelimisha wananchi kuhusu namna wanavyoweza kushiriki kikamilifu katika shughuli za uchimbaji, uongezaji thamani madini, na biashara ya madini kupitia masoko ya madini yaliyoanzishwa,” amesema Mhe. Senyamule.

Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa amesisitiza kuwa mkoa wa Dodoma umebarikiwa kuwa na rasilimali nyingi za madini ikiwemo madini ya viwandani, vito, na madini ya ujenzi. Hivyo, ameitaka Tume ya Madini kuendelea kuhamasisha wadau mbalimbali kuchangamkia fursa za uwekezaji kwenye sekta hiyo kwa kutumia sera na sheria zilizopo ambazo ni rafiki kwa wawekezaji.

Kwa upande wake, Maafisa wa Tume ya Madini waliopo katika banda hilo wameeleza kuwa Tume itaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu namna ya kushiriki katika mnyororo mzima wa shughuli za madini, ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa leseni, matumizi sahihi ya teknolojia ya uongezaji thamani madini, na umuhimu wa kuuza madini kupitia masoko rasmi.

Maonesho ya Nane Nane ya mwaka 2025 yanalenga kuonesha mafanikio na fursa mbalimbali za maendeleo kutoka sekta za kilimo, mifugo, viwanda, na madini, ambapo Tume ya Madini ni miongoni mwa taasisi zinazoshiriki kikamilifu kuhamasisha ushiriki wa wananchi na wawekezaji katika Sekta ya Madini.

Monday, August 04, 2025

TUNAPASWA KUJENGA UKANDA WA SADC USIO NA RUSHWA-MAJALIWA



_Asisitiza kuendelea kusimamiwa kwa Itifaki ya SADC dhidi ya Rushwa._*

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ametoa wito kwa Wakuu wa Taasisi za Kupambana na Rushwa  wa Jumuiya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) kuendelea kusimamia kikamilifu na kwa ufanisi utekelezaji wa Itifaki ya Jumuiya hiyo dhidi ya Rushwa ili kujenga ukanda usio na Rushwa.

Amesema kuwa Itifaki ya SADC Dhidi ya Rushwa bado ni nyenzo muhimu katika kufanikisha utawala bora, amani na muungano endelevu wa kikanda hivyo viongozi hao wanapaswa kuhakikisha kuwa juhudi za kupambana na rushwa zinaendelezwa.

Ametoa wito huo leo (Agosti 04, 2025) alipomuwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Ufunguzi wa Maadhimisho ya miaka 20 ya Utekelezaji wa Itifaki ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika Dhidi ya Rushwa, yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Gran Melia, jijini Arusha.

“Lazima tukiri kwamba rushwa ni tishio kwa usalama. Inachochea uhalifu uliopangwa, usafirishaji haramu wa binadamu, ugaidi, na kudhoofika kwa utawala wa sheria.”

Aidha, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa katika kipindi cha hivi karibuni, nchi Wanachama wa SADC ikiwemo Tanzania zimeendelea kuimarisha sheria za mapambano dhidi ya rushwa, kuziwezesha Taasisi zinazosimamia udhibiti na mapambano dhidi ya rushwa pamoja na kutoa elimu kwa wananchi juu ya athari za rushwa kwa ustawi wa Taifa.

“Hata ushirikiano wa kikanda katika mapambano dhidi ya rushwa umeimarika kwa kubadilishana taarifa, mashirikiano katika masuala ya sheria pamoja na uchunguzi wa pamoja katika kushughulikia masuala ya rushwa ya kikanda”

Kadhalika Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Tanzania kwa upande wake, inachukulia mapambano dhidi ya rushwa kama kipaumbele cha kitaifa na jambo la msingi kwa maendeleo Taifa na usalama wa Taifa.

“Njia iliyo mbele huenda ikawa ndefu, lakini tusiwaze kushindwa. Kwa ushirikiano endelevu, maono ya kimkakati, na utashi wa kisiasa, tunaweza na tunapaswa kujenga ukanda wa SADC usio na rushwa”

Mheshimiwa Majaliwa amewapongeza viongozi hao kwa kuendelea kusimamia mikakati mbalimbali ya kupiga vita rushwa ikiwemo kuanzishwa kwa mfumo imara ya ufuatiliaji, tathmini na utoaji wa taarifa SADC. Pamoja na Kielelezo cha Jitihada za Kikanda za Kupambana na Rushwa.

Kwa upande wake, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Stegomena Tax amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, inaendelea  kusimama imara katika kuendeleza utawala bora na kuheshimu utawala wa sheria, ambayo ni nguzo kuu katika mapambano yao ya pamoja dhidi ya rushwa.

“Warsha hii, imekuja wakati muafaka, ikiwa ni jukwaa la kubadilishana uzoefu bora, kuimarisha ushirikiano, na kuoanisha juhudi zetu katika kupambana na rushwa kwa ufanisi zaidi katika ukanda huu.”

Naye, Mwenyekiti wa Kamati ya Kupambana na Rushwa ya SADC, ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Crispin Francis Chalamila amesema kuwa kupitia mikakati Miwili ya Kupambana na Rushwa ya (2018-2022) na (2023-2027), wamefanikiwa kuandaa mtaala wa Kikanda uliowekwa viwango vya uchunguzi na kinga dhidi ya rushwa, kuandaa Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Kikanda wa Kupambana na Rushwa pamoja na Kuandaliwa kwa Tathmini ya Kikanda ya Mapambano Dhidi ya Rushwa.

 

KAILIMA ASEMA TUME ITAFANYA KAZI KWA KARIBU NA WAANDISHI WA HABARI KIPINDI CHOTE CHA UCHAGUZI MKUU 2025

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Ramadhani Kailima akizungumza katika Mkutano wa Tume, Wahariri na Waandishi wa Habari, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam, Agosti 4, 2025 ambapo amewahakikishia washiriki hao kuwa, ofisi yake itafanya kazi nao kwa karibu katika kipindi cha uchaguzi mkuu kwa njia mbalimbali ikiwemo kushiriki katika vipindi vya redio na runinga na kutoa taarifa kwa wakati. Picha na INEC.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Ramadhani Kailima akizungumza katika Mkutano wa Tume, Wahariri na Waandishi wa Habari, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam, Agosti 4, 2025 ambapo amewakikishia washiriki hao kuwa, ofisi yake itafanya kazi kwa karibu katika kipindi cha uchaguzi mkuu kwa njia mbalimbali ikiwemo kushiriki katika vipindi vya redio na runinga na kutoa taarifa kwa wakati. Picha na INEC.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Ramadhani Kailima (Katikati waliokaa), Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura, Giveness Aswile (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya Daftari na TEHAMA, Stanslaus Mwita (kushoto), Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Sheria Selemani Mtibora (wa pili kulia), na Mwenyekiti wa Mafunzo ya Wahariri na Waandishi wa Habari, Lilian Timbuka (kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wahariri na waandishi wa habari baada ya kufunguliwa kwa mafunzo hayo katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam, leo Agosti 4, 2025. Picha na INEC.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura, Giveness Aswile akizungumza katika Mkutano wa Tume, Wahariri na Waandishi wa Habari, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam, Agosti 4, 2025. Picha na INEC.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Ramadhani Kailima (Kulia), akimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura, Giveness Aswile, kabla hajafungua Mafunzo ya Wahariri na Waandishi wa Habari, yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam, leo Agosti 4, 2025. Picha na INEC.

BALOZI CHANA ASHIRIKI URITHISHAJI KWA VITENDO KATIKA MAONESHO YA NANENANE







Dodoma, Agosti 4, 2025
– Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Balozi Pindi Chana, amefanya ziara maalum katika banda la Makumbusho ya Taifa lililoko kwenye Maonesho ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi (Nane Nane) yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni, Jijini Dodoma. 

Ziara hiyo ni sehemu ya jitihada za Wizara kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa majukumu ya taasisi zilizo chini yake, hususan katika maeneo ya urithishaji wa historia, utamaduni na sayansi ya Taifa kwa umma.

Katika ziara hiyo, Mhe. Waziri alipokelewa na maafisa waandamizi wa Makumbusho ya Taifa waliomueleza kwa kina kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na taasisi hiyo katika kuhifadhi, kutafiti na kuelimisha jamii juu ya urithi wa kihistoria na kitamaduni wa Tanzania. Alitembelea sehemu mbalimbali za banda hilo na kujionea namna taasisi hiyo inavyotumia teknolojia ya kisasa na mbinu shirikishi kufikisha taarifa muhimu kwa wananchi.

Mhe. Dkt. Balozi Chana alionesha kuridhishwa na juhudi za Makumbusho ya Taifa katika kushiriki kikamilifu kwenye Maonesho hayo, na alisisitiza umuhimu wa kuendeleza ubunifu katika njia za kuwasilisha urithi wa Taifa kwa vizazi vya sasa na vijavyo. Alisema kuwa njia hizo zinapaswa kuwa na mvuto, hasa kwa vijana na wanafunzi, ili kuwahamasisha kushiriki kikamilifu katika kujifunza historia, mila na tamaduni za makabila mbalimbali ya Tanzania.

“Makumbusho ya Taifa yapo katika nafasi ya kipekee ya kuendeleza utalii wa ndani kupitia urithi wetu wa kihistoria na kitamaduni. Tunapaswa kuendelea kubuni mbinu mpya zitakazovutia vijana na kuwaelimisha kwa njia wanayoielewa,” alisema Mhe. Waziri.

Aidha, Mhe. Waziri aliwahimiza wadau wote wa sekta ya urithi na utalii kushirikiana katika kukuza maarifa ya kihistoria na kuongeza mchango wa sekta hiyo katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya Taifa.

Maonesho ya Nane Nane ni jukwaa muhimu kwa taasisi za umma na binafsi kuonesha huduma, teknolojia na mafanikio yao katika nyanja mbalimbali, likiwemo eneo la urithi wa Taifa. Banda la Makumbusho ya Taifa limeendelea kuvutia mamia ya wageni wanaojifunza historia ya Tanzania kupitia maonesho yaliyopangwa kwa ubunifu na weledi mkubwa

Friday, August 01, 2025

KAMISHNA BADRU ATAKA UBUNIFU ILI KUENDELEZA MAPANGO YA AMBONI





KAMISHNA BADRU ATAKA UBUNIFU ILI KUENDELEZA MAPANGO YA AMBONI 

Na Hamis Dambaya, Amboni Tanga.

Kamishna wa Uhifadhi Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) Abdul-razaq Badru amesema mamlaka hiyo Kwasasa itajikita katika kuendeleza ubunifu ili mapango ya Amboni yaliyoko mkoani Tanga yaweze kuvutia wageni wengi kutoka ndani na nje ya Nchi 

Katika mazungumzo yake na watendaji wa kituo hicho Kamishna Badru amesema eneo hilo ni hazina na kinachohitajika ni kulitumia kama fursa ya kiuchumi kupitia shughuli za utalii.

“Tushirikiane kwa umoja wetu na tubuni miradi ambayo italifanya eneo la Amboni liwe na mvuto kwa wageni wetu kutoka ndani na nje ya nchi,”alisema Kamishna Badru.

Mapango ya Amboni yamebeba hazina yenye historia mbalimbali ikiwemo harakati za kudai uhuru wa Tanzania bara,urithi na utamaduni wa makabila na watu wa Tanga pamoja na mafunzo ya jiografia ambapo ni adimu kupatikana katika nchi nyingine duniani.

 

RAIS SAMIA AFUNGUA KITUO CHA BIASHARA NA USAFIRISHAJI AFRIKA MASHARIKI (EACLC), UBUNGO – DAR ES SALAAM









Dar es Salaam, Agosti 1, 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo ameongoza hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Biashara na Usafirishaji Afrika Mashariki (East Africa Commercial and Logistics Centre – EACLC) kilichopo eneo la Ubungo jijini Dar es Salaam, tukio ambalo linachukuliwa kama hatua muhimu katika kuimarisha miundombinu ya biashara na usafirishaji ndani ya kanda ya Afrika Mashariki.

Akihutubia mamia ya wananchi, wadau wa sekta ya usafirishaji, viongozi wa serikali, na wawakilishi kutoka nchi jirani, Rais Samia amesisitiza kuwa uzinduzi wa kituo hiki ni sehemu ya juhudi za serikali yake katika kuhakikisha Tanzania inakuwa kitovu cha biashara na usafirishaji katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

> "Kituo hiki ni ushahidi wa dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita kuimarisha miundombinu ya kimkakati inayowezesha ukuaji wa biashara za kikanda na kuvutia uwekezaji wa ndani na nje ya nchi," alisema Rais Samia.



Kituo cha EACLC ni jukwaa la kisasa litakalowahudumia wafanyabiashara na wadau wa sekta ya usafirishaji kwa kuwapatia huduma mbalimbali zikiwemo maeneo ya kuhifadhi mizigo, ofisi za kampuni za usafirishaji, huduma za forodha, huduma za kibenki, pamoja na teknolojia ya kisasa ya ufuatiliaji wa mizigo. Kituo hiki pia kinatarajiwa kupunguza gharama na muda wa kusafirisha bidhaa, hivyo kuongeza ushindani wa bidhaa za Tanzania katika soko la kikanda.

Rais Samia pia alitumia fursa hiyo kuwataka wafanyabiashara, wawekezaji na wadau wote wa sekta binafsi kutumia vizuri miundombinu hii na kuendelea kushirikiana na Serikali katika kujenga uchumi wa kisasa, jumuishi na shindani.

Kwa upande wao, viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliokuwepo kwenye uzinduzi huo wameipongeza Tanzania kwa kuendelea kuwa mfano wa kuigwa katika uwekezaji wa miundombinu ya biashara, hatua ambayo inachangia kufanikisha ndoto ya soko la pamoja la kikanda.

Uzinduzi wa kituo hiki ni muendelezo wa miradi mikubwa inayotekelezwa chini ya Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa, huku ukisisitiza nafasi ya Tanzania kama lango kuu la biashara katika ukanda huu.

#EACLC2025 #BiasharaNaUsafirishaji #SamiaSuluhu #UchumiImara #TanzaniaInajengwa


RAIS SAMIA AFUNGUA KITUO KIKUBWA CHA BIASHARA NA USAFIRISHAJI AFRIKA MASHARIKI (EACLC) UBUNGO
















Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameendelea kuonesha dhamira ya kukuza uchumi wa nchi kwa vitendo baada ya kufungua rasmi Kituo cha Biashara na Usafirishaji Afrika Mashariki (EACLC) kilichopo Ubungo, jijini Dar es Salaam leo tarehe 1 Agosti 2025.

Kituo hicho ni cha aina yake katika ukanda wa Afrika Mashariki, kikilenga kuwa kitovu cha biashara, usafirishaji na huduma za kisasa, chenye uwezo wa kuhudumia wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi kwa ufanisi mkubwa.

Katika hotuba yake ya uzinduzi, Mhe. Rais Samia alisisitiza kuwa mradi huu ni sehemu ya ajenda ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kuwezesha biashara, kuhamasisha uwekezaji na kupanua fursa za ajira kwa Watanzania.

“Kituo hiki si tu miundombinu ya kisasa, bali ni jukwaa la mawasiliano ya kibiashara kati ya Tanzania na nchi jirani. Ni chachu ya ukuaji wa biashara ndogo, za kati na kubwa, huku tukijenga mazingira rafiki kwa wawekezaji,” alisema Rais Samia.

Umuhimu wa Kituo cha EACLC:

Kituo hiki kinatarajiwa kuongeza mnyororo wa thamani wa biashara za kikanda, kwa kurahisisha upatikanaji wa huduma mbalimbali kwa wafanyabiashara na wasafirishaji. Pia, kitasaidia kuharakisha na kuimarisha usalama wa usafirishaji wa bidhaa, hali itakayoboresha ushindani wa Tanzania katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Vilevile, kwa kutoa huduma bora, kituo hiki kitawavutia wawekezaji wa kimataifa, jambo litakalosaidia kukuza uchumi wa taifa. Kwa ujumla, mradi huu mkubwa utatoa maelfu ya ajira kwa Watanzania, moja kwa moja na kwa njia zisizo za moja kwa moja, hivyo kuchochea ustawi wa jamii na maendeleo ya nchi.

Waziri Mkuu azindua boti mbili za doria na uokozi

Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba ametoa siku 14 kwa wizara na taasisi zinazohusika na Kituo cha Kitaifa cha pamoja cha Oparesheni zipeleke w...