Tuesday, September 12, 2017

MPAKA MAFUTA WA KANISA LA SILOAM TANZANIA, AMFANYIA MAOMBI YA BARAKA KUHANI WA KANISA HILO NCHINI KENYA KUFUATIA KUWA MBUNGE NCHINI HUMO


Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Siloamu, Mpaka Mafuta akimfanyia maombi rasmi ya kumbariki Kuhani wa kanisa hilo nchini Kenya Agatha Mtindi, kwenye Ibada ya Mungu Baba, iliyofanyika jana katika Kanisa hilo, Mbezi Makonde jijini Dar es Salaam. Agatha alifanyiwa maombi hayo maalum ya kumbariki kufuatia kuteuliwa kwake kuwa Mbunge kwenye Akaunti ya Machakosi nchini Kenya katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika hivi karibuni.Zifuatazo ni picha za tukio hilo, tangu mwanzo hadi mwisho wa ibada. Picha zote na Bashir Nkoromo 











































































































































Monday, September 11, 2017

WIZARA YA AFYA YAPOKEA BIL. 227.76 KUSAIDIA SEKTA YA AFYA NCHINI

Picha ya Pamoja ya makabidhiano ya mkataba wa mfuko wa pamoja (Health Basket Fund) kwa ajili ya kufadhili shughuli mbalimbali za sekta ya afya nchini ikiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Mh. Dotto James na Balozi wa Denmark nchini Tanzania Bw. Einar katika kikao kilichofanyika ofisi ndogo za Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es salaam,wakwanza kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya 

Balozi wa Denmark nchini Tanzania Bw. Einar Jensen akisisitiza jambo katika kikao cha makabidhiano ya mkataba wa mfuko wa pamoja (Health Basket Fund), kilichofanyika mapema leo katika ofisi ndogo za Wizaraya Fedha na Mipango jijini Dar es salaam. 
Watumishi wa Serikali wakiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya wakifuatilia kwa karibu majadiliano katika kikao cha makabidhiano ya mkataba wa mfuko wa pamoja (Health Basket Fund) kwa ajili ya kufadhili shughuli mbalimbali za sekta ya afya nchini.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akisaini mkataba wa mfuko wa pamoja (Health Basket  Fund) kwa ajili ya kufadhili shughuli mbalimbali za sekta ya afya nchini, tukio lililofanyika katika ofisi ndogo za Wizara ya Fedha na Mipango leo jijini Dar es salaam. 
NA WAMJW-DAR ES SALAAM.

WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto imepokea shilingi Bilioni 227.76 kutoka kwenye mfuko wa pamoja (Health Basket Fund) kwa ajili ya kufadhili shughuli mbalimbali za sekta ya afya nchini.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam wakati wa kupokea fedha hizo , Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya amesema kuwa fedha hizo zitaelekezwa katika uboreshaji wa huduma za afya nchini.“Fedha hizi zitasaidia pia kutoa huduma za chanjo kwani ni afua muhimu kwa wananchi hususan katika kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miaka mitano nchini” alisema Dkt. Ulisubisya.

Aidha Dkt. Ulisubisya amesema kuwa kwa mara ya kwanza wameamua kupeleka fedha hizo moja kwa moja kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ili kuepuka changamoto za vituo hivyo kukosa dawa muhimu mara kwa mara.Mbali na hayo Dkt. Ulisubisya alisema kuwa asilimia 90 ya fedha hizo zinaenda moja kwa moja kwenye vituo vinavyotolea huduma za afya vya ngazi ya Halmashauri na asilimia 10 inatumika kwa ajili ya shughuli mbalimbali za usimamizi wa kisera katika sekta ya afya nchini. 

Aidha Dkt. Ulisubisya amesema kuwa fedha hizo pia zitasaidia katika kuimarisha miundombinu katika vituo vya afya na zahanati ili viweze kutoa huduma za upasuaji wa dharura kwa ajili ya akina mama wajawazito wanaokabiliwa na uzazi pingamizi.

Kwa upande wake Balozi wa Denmark nchini Tanzania Bw. Einar Jensen kwea niaba ya wadau wa mfuko huo amesema kuwa mbali na Fedha hizo kushughulikia maswala ya afya nchini hapa pia zitakuwa na shughuli mbalimbali za maendeleo .

“Mbali na kushughulikia masuala ya afya pia napendekeza fedha hizi zihusike katika kuhudumia wakimbizi wanaongia Tanzania hasa katika maeneo ya Kigoma na Kibondo” alisema Bw. Jensen.

Saturday, September 09, 2017

SERIKALI ZA TANZANIA NA KENYA ZAMALIZA MZOZO WA VIKWAZO VYA BIASHARA BAINA YA MATAIFA HAYO

Baadhi ya Maafisa Waandimizi wa Serikali, Wafanyabiashara na Wazalishaji wa bidhaa za Kilimo kutoka wakulima kutoka Tanzania na Kenya wakifuatilia taarifa mbalimbali zilizotolewa na Wenyeviti wa Mkutano huo uliojadili changamoto na utatuzi wa vikwazo vya biashara na uwekezaji katika Mataifa hayo.
Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dkt. Pindi Chana akitoa taarifa ya majadiliano ya mkutano baina ya Watendaji Wakuu wa Serikali ya Tanzania na Kenya uliojadili changamoto na utatuzi wa vikwazo vya biashara na uwekezaji katika Mataifa. Mkutano huo ulifanyika jana Septemba 8 Jijini Dar es Salaam. Wengine katika Picha ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara ya Tanzania, Prof. Adolf Mkenda na Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara ya Kenya Dkt. Chris Kiptoo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji (Baishara na Uwekezaji), Prof. Adolf Mkenda akizungumza na Watendaji Wakuu wa Serikali, Wafanyabiashara na Wazalishaji wa bidhaa za kilimo katika Mataifa hayo. Mkutano huo ulifanyika jana Septemba 8 Jijini Dar es Salaam. Wengine katika Picha ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara ya Tanzania, Prof. Adolf Mkenda na Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara ya Kenya Dkt. Chris Kiptoo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Ushirikiano wa Kenya, Dkt. Chris Kiptoo akizungumza na Watendaji Wakuu wa Serikali, Wafanyabiashara na Wazalishaji wa bidhaa za kilimo katika Mataifa hayo. Mkutano huo ulifanyika jana Septemba 8 Jijini Dar es Salaam. Wengine katika Picha ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara ya Tanzania, Prof. Adolf Mkenda na Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara ya Kenya Dkt. Chris Kiptoo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara, Uwekezaji na Ushirikiano wa Kenya, Dkt. Chris Kiptoo na Mwenjeji wake Prof. Adolf Mkenda wakionyesha Sera ya Taifa ya Biashara ya Kenya wakati mkutano baina ya Watendaji Wakuu wa Serikali, Wafanyabiashara na Wazalishaji wa bidhaa za kilimo katika Mataifa hayo uliojadili changamoto na utatuzi wa vikwazo vya biashara na uwekezaji katika Mataifa hayo. Mkutano huo ulifanyika jana Septemba 8 Jijini Dar es Salaam.(PICHA NA ELIPHACE MARWA-MAELEZO)

Na Ismail Ngayonga-MAELEZO-DAR ES SALAAM

SERIKALI za Tanzania na Kenya zimekubaliana kwa pamoja kumaliza vikwazo vya kibiashara katika usafirishaji na uingizaji wa bidhaa katika mipaka baina ya nchi hizo mbili hatua inayokusudia kuimarisha ushirikiano wa biashara na uwekezaji katika Mataifa hayo.

Hayo yamesemwa jana Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Wizara, Biashara na Uwekezaji (Biashara na Uwekezaji) Prof. Adolf Mkenda mara baaada ya kumalizika kwa mkutano wa pamoja yao ulioshirikisha Viongozi Waandamizi wa Serikali hizo, Wafanyabiashara na Wakulima kutoka Mataifa hayo.

Anasema katika mkutano huo Serikali ya Tanzania iliwasilisha mapendekezo 15 kwa Serikali ya Kenya yanayopaswa kupatiwa ufumbuzi, ambapo kwa upande wa Kenya waliwasilisha mapendekezo 16 ambapo kwa kiasi kikubwa hoja hizo zimekubaliwa na kupatiwa majibu yake katika mkutano huo.

Prof. Mkenda alisema kupatikana kwa mwafaka wa majadiliano hayo ni maelekezo ya Viongozi Wakuu wa Mataifa hayo, Rais Dkt. John Pombe Magufuli wa Tanzania na Uhurru Kenyatta wa Kenya kwa kuwa Viongozi hao wametaka suala hilo lipatiwe mwafaka wa haraka ili kuweza kuendeleza ushirikiano na uhusiano katika nyanja mbalimbali baina ya nchi hizo.

Kwa mujibu wa Prof. Mkenda alisema mkutano huo uliofanyika kwa muda wa siku tatu ulilenga kumaliza changamoto za biashara zinazojitokeza kwa Wafanyabiashara wa Tanzania na Kenya, ambapo Timu za Wataalam wa Serikali hizo ambapo hoja hizo zimeweza kujadiliwa na kupatiwa ufumbuzi wa pamoja, hatua inayolenga kufungua upya milango ya ushiriakiano baina ya Wafanyabiashara na Wakulima wa Tanzania na Kenya. 

“Katika majadiliano yetu tumekubaliana kuwa sasa bidhaa ya gesi ya kupikia na ungano wa ngano ambazo zilizuliwa kuingia Kenya sasa zitaruhusiwa kuingia nchini humo, na sisi kwa upande wetu Tanzania tumeruhusu maziwa na sigara kutoka Kenya zianze kuingia nchini” alisema Prof. Mkenda.

Akifafanua zaidi Mkenda anasema Mkutano huo pia uliwashirikisha Wafanyabiashara na Kampuni za uzalishaji wa bidhaa za ngano ikiwemo kampuni ya Azam Bakhressa ambayo huzalisha na kusambaza ngano hapa nchini pamoja na nchi jirani ikiwemo Kenya pamoja na wakulima wa zao hilo kutoka mikoa ya Sumbawanga, Iringa na Manyara.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Ushirikiano ya Kenya, Dkt. Chris Kiptoo alisema Serikali ya Kenya itayachulia kwa uzito unaostahili mwafaka wa majadiliano hayo, kwa kuzingatia kuwa Serikali ya Tanzania na Kenya zina uhusiano na ushirikiano wa muda mrefu katika masuala ya biashara na uwekezaji.

Alisema kuwa Serikali ya Kenya imewekeza jumla Dola Bilioni 1.5 katika sekta ya viwanda, ambapo hadi sasa vimeweza kuajiri jumla ya watu 50,000 na pia msingi wa biashara ya Kenya katika Tanzania imeweza kuongeza kutoka Tsh. Bilioni 17 mwaka 2004 hadi kufikia Dola Bilioni 34 mwaka 2015.

Dkt. Kiptoo anasema mara baada ya mkutano huo, Viongozi wa Serikali hizo pamoja na Wafanyabiashara kutoka upande za Tanzania na Kenya wanatarajia kukutana kwa mara ya mwisho Mombasa nchini Kenya kwa ajili ya kuhitimisha makubaliano ya pamoja ya uingizaji na usafirishaji wa bidhaa.

Akifafanua zaidi Dkt. Kiptoo anasema katika majadiliano hayo Idara muhimu zinazohusika na masuala ya biashara na uwekezaji kutoka Serikali za Tanzania na Kenya zilishiriki katika mkutano huo, ikiwemo Maafisa wa Idara za forodha, kodi na ushuru.

Tarehe 3 Agosti mwaka huu, Viongozi Waandamizi wa Serikali za Tanzania na Kenya walikutana katika Mpaka wa Namanga kwa ajili ya kikao cha majadiliano ya pamoja kilicholenga kumaliza mzozo wa kuzuiwa kwa Wafanyabiashara ya Ngano nchini kuingiza bidhaa hiyo nchini Kenya.

WAZIRI WA FEDHA AKAGUA NA KUTOA MAAGIZO KUHUSU MADINI YA ALMASI YALIYOKAMATWA AIRPORT DAR ES SALAAM


 Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Filip Mpango (katikati) akiwa na viongozi wengine wa Serikali, Mkurugenzi wa Mashtaka(DPP) Biswalo Mganga (kushoto), Kamishna Mkuu wa  Mamlaka ya Mapato nchini TRA Charles Kichere(kulia) Naibu Kamishna Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Brigedia Jenerali John Mbungo wakiangalia Mzigo wa Almasi uliokamatwa katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Filip Mpango akisoma maelezo ya mzigo huo ambayo yalikuwa tofauti kabisa na uhalisia mara baada ya kuhakikiwa na timu ya  Wataalamu wa Kitanzania wazalendo.
 Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Filip Mpango akipata maelezo ya mzigo huo ambayo yalikuwa tofauti kabisa na uhalisia mara baada ya kuhakikiwa na timu ya  Wataalamu wa Kitanzania wazalendo.
 Sehemu ya Mzigo huuo wa Almasi uliokamatwa katika uwanja wa Ndege ambao thamani yake ni zaidi ya Tsh. Bilioni 65.
 Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Filip Mpango akizungumza wakati akipokea Ripoti ya Uchunguzi wa Madini hayo ya Almasi jijini Dar es Salaam.
Profesa Abdulkarim Mruma akiwasilisha Taarifa yake ya Uchunguzi wa Madini yaliyokamatwa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Picha na Mpiga Picha Maalum.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akiongea na wanahabari baada ya kufanya  ziara ya kushtukiza, kufuatilia Almasi iliyokamatwa ikisafirishwa kwenda nje ya nchi huku ikiwa imethaminiwa chini ya kiwango katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam. Kulia kwake ni Naibu Kamishna Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Brigedia Jenerali John Mbungo, Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Charles Kichere na Kushoto kwake ni Kamishna wa Madini Tanzania Mhandisi Benjamini Mchwampaka Msajili wa Hazina Dkt. Oswald Mashindano na kulia kabisa ni Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Bw. John Biswalo. 



Dare es Salaam, 09 Septemba, 2017: Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), ameviagiza vyombo vinavyohusika kuchukua hatua za kisheria dhidi ya kampuni ya Williamson Diamond Ltd na wote waliohusika kuidhinisha usafirishaji wa madini ya almasi kutoka migodi ya kampuni hiyo na kudanganya thamani halisi ya madini hayo kwa lengo la kuisababishia hasara Serikali. 
Dkt. Mpango ametoa agizo hilo leo tarehe 09 Septemba, 2017 baada ya kukagua madini ya almasi yaliyokamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam yakisafirishwa kupelekwa nchini Ubelgiji. 
Miongoni mwa hatua za kisheria ni pamoja na kutaifisha madini yote ya almasi yaliyokamatwa baada ya kubainika udanganyifu wa thamani yake halisi, kuwakamata na kuwachunguza wote waliohusika katika udanganyifu huo wakiwemo wajumbe wa bodi zilizomaliza muda wake na wafanyakazi waliopo na waliostaafu. 
Almasi hiyo ilikamatwa tarehe 31 Agosti, 2017 muda mfupi kabla ya kupakizwa kwenye ndege ili isafirishwe kwenda nchini Ubelgiji, na ilipochunguzwa ilibainika kuwa nyaraka za kampuni ya Williamson Diamond Ltd zimeonesha kuwa almasi hiyo ina thamani ya Dola za Marekani Milioni 14.798 sawa na Shilingi Bilioni 33 za Tanzania wakati thamani yake halisi ni Dola za Marekani Milioni 29.5 sawa na Shilingi Bilioni 65 za Tanzania. 
Kabla ya kukagua almasi hiyo Waziri Mpango amepokea taarifa ya timu ya wataalamu iliyofanya tathmini ya thamani halisi ya madini hayo ambapo kiongozi wa timu hiyo Prof. Abdulkarim Mruma amesema pamoja na kubaini upotevu mkubwa wa fedha, kuna dosari nyingine zikiwemo kukosekana kwa vifaa ya kupimia madini hayo, almasi kusafirishwa na kuuzwa sokoni bila uwepo wa mwakilishi wa Serikali na ameshauri hatua za udhibiti huo zifanyike katika madini yote yanayochimbwa hapa nchini.

Pamoja na kuipongeza timu iliyofanya tathmini hiyo na vyombo vya dola vilivyokamata madini hayo Waziri Mpango amesema Serikali itatekeleza ushauri wote uliotolewa na timu ya Prof. Mruma na kwamba kuanzia sasa almasi inayozalishwa hapa nchini itasindikizwa na maafisa wa Serikali hadi sokoni na inataka kuanza kupokea gawio halali kutoka mgodi huo. 

Waziri Mpango ametoa maagizo hayo mbele ya viongozi wa vyombo mbalimbli wakiwemo Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere, Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Bw. Biswalo Mganga, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Brigedia Jenerali John Julius Mbungo, Kamishna wa Madini Tanzania Mhandisi Benjamin Mchwampaka na Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam SACP - Lazaro Mambosasa. 

Imetolewa na Benny Mwaipaja
MKUU WA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO

MKUTANO WA 17 WA BARAZA LA MAWAZIRI UMOJA WA NCHI ZA MASHARIKI NA KUSINI MWA AFRIKA KUHUSU UDHIBITI WA BIASHARA FEDHA HARAMU


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Waziri wa Fedha na Mipango wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip I.Mpango mara alipowasili Zanzibar Beach Resort Hotel Mbweni Nje ya Mji wa Zanzibar katika Mkoa wa Mjini Magharibi katika Ufunguzi wa Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Umoja wa Nchi za Umoja wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa Udhibiti wa Biashara ya Fedha Haramu,uliofanyika leo.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar  Dkt. Khalid Salum Mohamed mara alipowasili Zanzibar Beach Resort Hotel Mbweni Nje ya Mji wa Zanzibar katika Mkoa wa Mjini Magharibi katika Ufunguzi wa Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Umoja wa Nchi za Umoja wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa Udhibiti wa Biashara ya Fedha Haramu,uliofanyika leo.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa na Viongozi mbali mbali wajkati wimbo wa Taifa Ukipigwa katika  Ufunguzi wa Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Umoja wa Nchi za Umoja wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa Udhibiti wa Biashara ya Fedha Haramu,uliofanyika leo katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort Hotel Mbweni Nje ya Mji wa Zanzibar katika Mkoa wa Mjini Magharibi.
 Washiriki wa Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Umoja wa Nchi za Umoja wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa Udhibiti wa Biashara ya Fedha Haramu,kutoka Nchini South Afrika wakiwa  katika ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika leo katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort Hotel Mbweni Nje ya Mji wa Zanzibar katika Mkoa wa Mjini Magharibi,mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)
 Washiriki wa Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Umoja wa Nchi za Umoja wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa Udhibiti wa Biashara ya Fedha Haramu,kutoka Nchini SWAZILAND wakiwa  katika ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika leo katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort Hotel Mbweni Nje ya Mji wa Zanzibar katika Mkoa wa Mjini Magharibi,mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).
 Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Umoja wa Nchi za Umoja wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa Udhibiti wa Biashara ya Fedha Haramu,wakiwa  katika ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika leo katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort Hotel Mbweni Nje ya Mji wa Zanzibar katika Mkoa wa Mjini Magharibi,mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).
 Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Umoja wa Nchi za Umoja wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa Udhibiti wa Biashara ya Fedha Haramu,wakiwa  katika ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika leo katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort Hotel Mbweni Nje ya Mji wa Zanzibar katika Mkoa wa Mjini Magharibi,mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).
 Washiriki wa Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Umoja wa Nchi za Umoja wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa Udhibiti wa Biashara ya Fedha Haramu,kutoka Zanzibar Nchini Tanzania wakiwa  katika ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika leo katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort Hotel Mbweni Nje ya Mji wa Zanzibar katika Mkoa wa Mjini Magharibi,mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).
 Washiriki wa Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Umoja wa Nchi za Umoja wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa Udhibiti wa Biashara ya Fedha Haramu,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipokuwa akitoa hutuba ya ufunguzi wa Mkutano huo leo  katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort Hotel Mbweni Nje ya Mji wa Zanzibar katika Mkoa wa Mjini Magharibi.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akitoa hutuba yake ya  Ufunguzi wa Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Umoja wa Nchi za Umoja wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa Udhibiti wa Biashara ya Fedha Haramu,uliofanyika leo  katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort Hotel Mbweni Nje ya Mji wa Zanzibar katika Mkoa wa Mjini Magharibi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akitoa hutuba yake ya  Ufunguzi wa Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Umoja wa Nchi za Umoja wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa Udhibiti wa Biashara ya Fedha Haramu,uliofanyika leo  katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort Hotel Mbweni Nje ya Mji wa Zanzibar katika Mkoa wa Mjini Magharibi (Picha na Ikulu)

Friday, September 08, 2017

WAZIRI LUKUVI AZINDUA NYUMBA ZA MAKAZI ZA NHC CHATO

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi akiwasili eneo la mradi wa Nyumba za NHC Chato. Mradi una Nyumba 20 zenye Nyumba vitatu kila moja.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi akiwasili eneo la mradi wa Nyumba za NHC Chato. Mradi una Nyumba 20 zenye Nyumba vitatu kila moja.

Mradi wa Nyumba za NHC Chato. Mradi una Nyumba 20 zenye Nyumba vitatu kila moja

Waziri Lukuvi akishereheka kwa pamoja na wananchi wa Chato alipowasili eneo la mradi.

Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Kyando Mchechu akiwahutubia wananchi wakati wa Uzinduzi.

WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU AMPONGEZA NDEJEMBI, AMSIFIA KWA UADILIFU NA UCHAPAKAZI

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba , amempongeza Mhe. Deogratius John Ndejembi kwa kuaminiwa ...