Miss Tourism Queen International 2007

Mrembo wetu Sophia Kapama, Mtanzania anayeshiriki Miss Tourism Queen International 2007 huko China anaendelea vyema na mpambano wa kuwania taji hilo litakalofikia mwisho wake Agosti 2, hapa yupo yeye na wenzake.






Ziara ya Warembo wa Miss Tourism Queen International 2007 katika ziwa maarufu la Wes Lake la jiji la Hangzhou. Marco Polo aliweka nanga ya meli yake karne moja iliyopita na alifurahishwa na mandhari ya Hangzhou West Lake. Mandhari hiyo ya West Lake sasa inapambwa na Warembo kutoka nchi zaidi ya 100 Miss Tourism Queen International 2007. Wakiwa huko warembo walifunzwa kung fu na ngoma za jadi za kichina.



Niungane na Kaka Issa Michuzi kuwatafadhalisha Watanzania tumpigieni kura MTQI Tanzania ambaye yuko China kwenye mashindano.

Bonyeza http://www.misstqi.com/vote/vote_mtqi.phpupate taarifa kwa kina zaidi.

Credit card inahitajika na USD 2 hununua kura 10. Naona kuna watu wameshampigia kura lakini tunaomba tusaidiane kwani haba na haba hujaza kibaba.
Pia wapiga kura wanaweza kujishindia zawadi kama mnavyoweza kusoma kwenye website.

Hii ni picha ya muda kidogo alipokuwa akigombea Miss Sinza.

Picha za Sophia ni ngumu kupata kwani hawana website moja rasmi kwa hiyo ni kazi haswa. Update ni kwamba mpaka sasa hivi wametembelea miji ya China na jana walifanya mashindano ya Miss Best Smile ambayo ameshinda China. Wanaendelea na matokeo yatatangazwa baadaye.

Asanteni

Comments

Anonymous said…
Ηi fгiеnds, іts gгeat piece of wгіting гegarding tutoгingаnd сomplеtely explaіned, keеp іt up all thе tіme.


My website; instant payday Loans online
Also see my web page :: Payday Loans