Monday, July 16, 2007

Tanzania bila Ukimwi Inawezekana


Mwishoni mwa wiki, Rais Kikwete aliongoza wananchi na viongozi wenzake wa serikali na wa vyama vya kisiasa katika kampeni zilizoanza za kupima Virusi vya Ukimwi. Kitendo cha Rais Kikwete na mkewe (Pichani) na viongozi wengine wote ni kitendo cha kijasiri ambacho hakina budi kupongezwa na kuungwa mkono. Ingawa ni kitendo kilichochelewa lakini kufanyika kwake kumekuja wakati muafaka katika kukoleza mapambano dhidi ya ugojwa huu unaoangamiza jamii yetu na kuweka hatima ya baadaye ya taifa letu mashakani.

Ingawa pia haitoshi kwa viongozi kupima tu bali pia kutangaza matokeo ya vipimo hivyo hadharani ili wawe watakaogundulika wameambukizwa siyo tu wawe mfano wa kupima tu bali pia wawe mfano wa watu wanaoishi kwa matumaini na kuendelea na majukumu yao badala ya kuonekana kuwa kugundulika kuwa na VVU ni leseni ya kifo.

Hata hivyo, katika upande wa kauli mbiu ya 'Tanzania Bila Ukimwi Inawezekana' kunaonekana kuwapo utata wa aina fulani. Moja sababu Ukimwi upo na kwa maana hiyo haujapatiwa dawa na kwa maana hiyo wenye ukimwi wapo. Kwa maana hiyo kusema tanzania bila ukimwi inawezekana ni kuwanyanyapaa wenye virusi. Je wanapopatikana na ukimwi ina maana serikali itafanyaje?

No comments: