Friday, April 20, 2018
Wednesday, April 18, 2018
RAIS DKT MAGUFULI ATOA MKONO WA POLE FAMILIA YA MRISHO GAMBO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiweka saini kwenye kitabu cha maombolezo baada ya kuwasili mtaa wa Muheza Kariakoo jijini Dar es salaam kutoa pole kwa familia ya Mzee Mashaka Gambo kwa kufiwa na mkewe ambaye pia ni mama mzazi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo kwa kufiwa na mama yake mzazi Marehemu Rehema Paul Mumbuli leo Aprili 18, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimpa pole Mzee Mashaka Gambo kwa kufiwa na mkewe Marehemu Rehema Paul Mumbuli ambaye pia ni mama wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo leo Aprili 18, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimpa pole Muu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo alipofika nyumbani kwao mtaa wa Muheza Kariakoo jijini Dar es salaam kumfariji kwa kufiwa na mama yake mzazi Marehemu Rehema Paul Mumbuli leo Aprili 18, 2018.
Mama janeth Magufuli akimpa pole Muu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo alipofika nyumbani kwao mtaa wa Muheza Kariakoo jijini Dar es salaam kumfariji kwa kufiwa na mama yake mzazi Marehemu Rehema Paul Mumbuli leo Aprili 18, 2018.
Mama Janeth Magufuli akimpa pole Mzee Mashaka Gambo kwa kufiwa na mkewe ambaye pia ni mama mzazi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo alipofika nyumbani kwao mtaa wa Muheza Kariakoo jijini Dar es salaam kuwafariji leo Aprili 18, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwasili mtaa wa Muheza Kariakoo jijini Dar es salaam kutoa pole kwa familia ya Mzee Mashaka Gambo kwa kufiwa na mkewe ambaye pia ni mama mzazi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo kwa kufiwa na mama yake mzazi Marehemu Rehema Paul Mumbuli leo Aprili 18, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiaga waombolezaji baada ya kutoa mkono wa pole kwa familia ya Mzee Mashaka Gambo kwa kufiwa na mkewe ambaye pia ni mama mzazi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo kwa kufiwa na mama yake mzazi Marehemu Rehema Paul Mumbuli leo Aprili 18, 2018. Picha na IKULU
WAZIRI PROFESA MAKAME MBARAWA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA (TPC) KUKAGUA UTENDAJI
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (katikati), akizungumza na Uongozi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakati alipofika kwenye Ofisi za shirika hilo, kukagua utendaji katika Idara mbalimbali za shirika hilo leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya TPC, Dk. Haruni Kondo na kushoto ni Kaimu Postamasta Mkuu, Hassan Mwang'ombe.
Meneja Masoko wa Shirika la Posta, David George akimpatia maelezo Waziri Profesa Mbarawa kuhusu mikataba ya Kibiashara iliyoingiwa na shirika.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akiangalia baadhi ya mikataba iliyoingiwa na shirika hilo.
Kaimu Postamasta Mkuu, Hassan Mwang'ombe (katikati), akimweleza jambo Waziri Profesa Mbarawa (kulia), katika ziara hiyo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akimsikiliza mmoja wa wafanyakazi wa Idara ya Kompyuta ya Shirika la Posta, Agnes Mtango. Kushoto ni Postamasta Mkuu, Hassan Mwang'ombe.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akielekeza jambo katika Idara ya Kompyuta ya Shirika la Posta. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya shirika hilo, Dk. Haruni Kondo na kushoto ni Postamasta Mkuu, Hassan Mwang'ombe.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akielekeza jambo katika Idara ya Usafirishaji ya Shirika la Posta, alipoangalia mfumo wa usafirishaji kwenye moja ya kompyuta za idara hiyo.
Afisa Msimamizi wa Magari ya Shirika (Transport Officer), Mhandisi Lameck Francis (kulia), akimweleza Waziri Profesa Mbarawa namna ya mfumo wa Udhibiti wa magari na mafuta kwenye moja ya kompyuta za idara hiyo, unavyofanyakazi.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akikagua mfumo wa Udhibiti wa magari na mafuta ya shirika ya kwenye moja ya kompyuta za idara hiyo.
Meneja Fedha wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Rajab Mngong'e (kushoto), akimweleza jambo Waziri Profesa Makame Mbarawa, alipofika katika Idara ya Fedha katika ziara hiyo.
Meneja Msaidizi Idara ya Fedha, Aron Samwel (kushoto), akimuonesha Waziri Profesa Makame Mbarawa, mfumo wa utunzaji wa fedha za shirika unavyofanya kazi.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (wa pili kushoto), akisindikizwa na Mwenyekiti wa Bodi ya TPC, Dk. Haruni Kondo (wa pili kulia), Kaimu Postamasta Mkuu, Hassan Mwang'ombe (kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Elia Madulesi, mara baada ya kumaliza ziara hiyo.
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mh. Profesa Makame Mbarawa (MB) leo tarehe 17 Aprili, 2018 amefanya ziara ya kushtukiza Makao Makuu ya Shirika la Posta Tanzania.
Mhe. Profesa Mbarawa ametembelea Makao Makuu ya Shirika la Posta Tanzania kwa lengo la kukagua utendaji na uendeshaji wa shughuli mbalimbali za Posta, katika ziara hiyo Mhe. Waziri aliongozana na Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Shirika la Posta Luteni Kanali mstaafu Dr. Haruni Kondo.
Katika ziara hiyo Mhe. Waziri alitaka kujionea matumizi ya mifumo ya kielektronik na namna ambavyo Shirika limejipanga kuitumia mifumo mbalimbali ili kusimamia utendaji kwa ukaribu. Mhe. Waziri Mbarawa alitembelea idara ya Fedha, Idara ya Barua na Logistiki, Idara ya Sheria, Idara ya Masoko na pia alikagua mifumo udhibiti wa gharama za mafuta na mwenendo wa magari ya Shirika yanayosafiri kati ya Dar es salaam na mikoani.
Katika ziara hiyo Mh. Waziri ameitaka menejimenti ya Shirika kusimamia utendaji kazi na kuzingatia weledi na matumizi ya mifumo ya kielektroniki na kufanya kazi kwa bidii kwa kuzingatia kasi ya Serikali ya awamu ya tano na kuacha kufanya kazi kwa mazoea.
Mhe. Waziri alitoa msisitizo wa kufanya kazi kwa bidii ili kuongeza ufanisi na kukuza tija kwa kila Idara ndani ya Shirka la Posta. Waziri amemwaagiza Kaimu Postamasta Mkuu Hassan Mwang’ombe kufuatilia utendaji wa kila idara na kupata taarifa za mara kwa mara ili kuimarisha utendaji wa shirika.
Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Shirika la Posta alimshukuru Waziri Mhe. Mbarawa kwa kutembelea Shirika la Posta na kuahidi kuwa maagizo yote na maelekezo aliyoyatoa atayasimamia kikamilifu ili kuleta tija na Ufanisi zaidi.

TAMASHA LA AMKA KIJANA, TUIJENGE IRINGA YETU LAFANA MJINI IRINGA
Mkuu wa wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela (kushoto) akifurahia burudani iliyokuwa ikitolewa na msanii wa Muziki wa Singeli, Dulla Makabila wakati wa Tamasha la Amka Kijana, Tuijenge Iringa Yetu lililofanyika uwanja wa MwembeTogwa, Iringa mwishoni mwa wiki iliyopita.
Msanii wa Bongo Fleva, Nuh Mziwanda nae hakuwa nyuma kutoa burudani.
Mkuu wa wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela akizungumza na wana-Iringa waliojitokeza katika amasha la Amka Kijana, Tuijenge Iringa Yetu lililofanyika uwanja wa MwembeTogwa, Iringa mwishoni mwa wiki iliyopita. 
Mwenyekiti wa Uzalendo Kwanza, Msanii wa Bongo Movies, Steve Nyerere ambao ndiyo waandaaji wa Tamasha la Amka Kijana, Tuijenge Iringa Yetu akizungumza machache na wakazi wa Iringa juu ya kutunza Amani, Upendo na Mshikamano wetu katika uwanja wa MwembeTogwa, Iringa mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mkuu wa wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela akiwatambulisha wasanii wa Bongo Movie waliofika katika Tamasha la Amka Kijana, Tuijenge Iringa Yetu lililofanyika uwanja wa MwembeTogwa, Iringa mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mratibu wa Tamasha la Amka Kijana, Tuijenge Iringa Yetu, Msanii wa Bongo movies, Single Mtambalike (Rich Rich) akizungumza machache wakati wa tamasha hilo lililofanyika uwanja wa MwembeTogwa, Iringa mwishoni mwa wiki iliyopita.
Msanii maarufu wa Bongo Movies Jacob Steven 'JB ' akieleza machache.
Msanii maarufu wa Bongo Movies Jacob Steven 'JB ' akimtambulisha msanii mwenzake Weru Sengo.
Msanii wa Kundi la Ze Komed akitoa burudani.
Mchekeshaji maarufu, Mama Asha Boko akitoa burudani.
Dj Choka nae alipata wasaa wa kutoa neno kwa wana-Iringa.
Msanii wa Bongo Movies, Anti Ezekiel akiwasalimu wakazi wa Iringa.
Subscribe to:
Posts (Atom)
WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU AMPONGEZA NDEJEMBI, AMSIFIA KWA UADILIFU NA UCHAPAKAZI
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba , amempongeza Mhe. Deogratius John Ndejembi kwa kuaminiwa ...
-
Hapa mmoja wa watoto hao akiwa na kijana mwenzake mwenye miaka 18, wote wako sawa lakini yeye hawezi kuzungumza kama watu wa kawaida. Mama S...
-
Nadhani mtakumbuka kibwagizo maarufu katika TV ambacho kinaimbwa perupe pepero perupe pepero hawa ni vijana wa Sisi Tambala waliokuwapo kati...
-
Mdau Julius Samwel hivi karibuni alikuwa huko Mwanza na hizi ndizo alizofanikiwa kutumegea, wadau hebu someni hicho kibao mniambie kuna nini...