Tuesday, September 05, 2017

WAZIRI UMMY MWALIMU AZINDUA UGAWAJI WA VITAMBULISHO VYA TIBA KWA WAZEE MANISPAA YA UBUNGO

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy A. Mwalimu akizungumza wakati wa uzindua wa Ugawaji wa vitambulisho vya matibabu Bure kwa Wazee katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy A. Mwalimu (Wa Tatu Kushoto) akionyesha vitambulisho vya Wazee akiwa na viongozi wengine wa Chama na serikali Wilaya ya Ubungo wakati wa Ugawaji wa vitambulisho vya matibabu Bure kwa Wazee katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akisalimiana na baadhi ya Wazee walioshiriki uzinduzi wa Ugawaji wa vitambulisho vya matibabu Bure kwa Wazee katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam.
 Kaimu Mganga Mkuu Wilaya ya Ubungo Bi Maria Maliwa akisoma taarifa ya huduma za afya, Ustawi wa jamii na Msamaha kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo katika uzinduzi wa vitambulisho vya msamaha kwa wazee wa Manispaa ya Ubungo. 
 Zoezi la Uzinduzi wa Ugawaji wa vitambulisho vya awali 7296 vya matibabu Bure kwa Wazee katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kwa ajili ya uzinduzi wa Ugawaji wa vitambulisho vya awali 7296 vya matibabu Bure kwa Wazee katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy A. Mwalimu akimpatia Mzee Ferooz Kafuru kitambulisho Cha matibabu wakati wa uzindua wa Ugawaji wa vitambulisho vya matibabu Bure kwa Wazee katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Wazee wa Halmshauri ya Manispaa ya Ubungo wakishuhudia zoezi la Ugawaji wa vitambulisho vya awali 7296 vya matibabu Bure kwa Wazee. Zoezi hili limezinduliwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy A. Mwalimu leo Septemba 4, 2017 
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ubungo Ndg Salum A. Kalli akitoa salamu za CCM wakati wa uzinduzi wa Ugawaji wa vitambulisho vya awali 7296 vya matibabu Bure kwa Wazee katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam.Kalli amepongeza uongozi wa serikali Wilaya ya Ubungo kwa kutekeleza ilani ya CCM ya ushindi yenye mkataba na wananchi kwa kipindi cha miaka mitano 2015-2020 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy A. Mwalimu akiteta Jambo na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo mara baada ya kuzindua Huduma ya Ugawaji wa vitambulisho vya matibabu Bure kwa Wazee katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Walaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori akisalimiana na Wazee waliofika kushuhudia zoezi la uzinduzi wa vitambulisho kwa Wazee wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo lilifanywa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy A. Mwalimu.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy A. Mwalimu akimpatia Bi Theresia Mbimbo kitambulisho Cha matibabu wakati wa uzindua wa Ugawaji wa vitambulisho vya matibabu Bure kwa Wazee katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Wazee wa Halmshauri ya Manispaa ya Ubungo wakishuhudia zoezi la Ugawaji wa vitambulisho vya awali 7296 vya matibabu Bure kwa Wazee. Zoezi hili limezinduliwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy A. Mwalimu leo Septemba 4, 2017 .
Baadhi ya Wazee wa Halmshauri ya Manispaa ya Ubungo wakishuhudia zoezi la Ugawaji wa vitambulisho vya awali 7296 vya matibabu Bure kwa Wazee. Zoezi hili limezinduliwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy A. Mwalimu leo Septemba 4, 2017 
Baadhi ya Wazee wa Halmshauri ya Manispaa ya Ubungo wakishuhudia zoezi la Ugawaji wa vitambulisho vya awali 7296 vya matibabu Bure kwa Wazee. Zoezi hili limezinduliwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy A. Mwalimu leo Septemba 4, 2017 
Madiwani wa Manispaa wakishuhudia zoezi la Ugawaji wa vitambulisho vya awali 7296 vya matibabu Bure kwa Wazee. Zoezi hili limezinduliwa na Waziri wa Afya.

Na Mathias Canal, Dar es salaam

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy A. Mwalimu amezindua Ugawaji wa vitambulisho vya awali 7296 vya matibabu Bure kwa Wazee katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam.

Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika katika Viwanja vya TP Sinza E Waziri Ummy alipongeza uongozi wa Wilaya ya Ubungo kwa kutambua umuhimu wa kutekeleza kwa vitendo maelekezo ya serikali ya kuwatambua Wazee katika Halmashauri na kuwapatia vitambulisho vitakavyo wawezesha kupata Huduma za matibabu bila vikwao.

Alisema kuwa Wazee ni asilimia 5.6 ya wananchi wote wa Tanzania idadi ambayo kwa kiasi kikubwa inaleta msukumo wa nchi kuweka mifumo madhubuti ya kuhudumia Wazee ikiwemo kurahisisha upatikanaji wa Huduma katika matibabu.

Alisema kuwa Jambo hilo ni kuzingatia ukweli kwamba Wazee wanakabiliwa na changamoto mbalimbali zinazosababishwa na umri mkubwa na mtazamo wa Jamii ambao umekuwa ukichangia ukiukwaji wa haki na maslahi ya Wazee katika ngazi mbalimbali.

Alisema Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo imeingia kwenye rekodi kwa kuwatambua Wazee wasio na uwezo kwani watapatiwa vitambulisho vitakavyo wawezesha kupata Huduma za matibabu Bure.

Mhe Ummy alisema kuwa Halmashauri zingine kote nchini zinapaswa kuanzisha haraka zoezi la kuwathamini Wazee kwa kuwapatia Huduma Bora za afya kabla ya kutoa Huduma za matibabu kwa Wazee kote nchini kwa kuanzisha dirisha maalumu na wataalamu wa kuwahudumia Wazee.

Alitoa Rai kwa watoa Huduma wa Afya kuviheshimu vitambulisho wakati wote Wazee wanapoenda navyo kupatiwa matibabu huku akiwasihi Wazee kutumia vitambulisho hivyo kwa kuzingatia maelekezo sio kwa kuwapa watu wengine wasiohusika navyo.

Aidha waziri Ummy ameahidi bima ya afya kwa watoto 100 wenye umri chini ya miaka 18 wanaoishi kwenye mazingira magumu wilaya ya Ubungo na uandikishwaji utaanza leo pia ameahidi kujenga wodi ya wazazi, watoto na maabara ya damu kwenye kituo kimoja cha afya wilaya ya ubungo mara baada ya kusikia hotuba ya kaimu mganga mkuu wa wilaya ya Ubungo.

Muheshimiwa waziri ameiomba jamii kujiunga na bima za afya za gharama nafuu ili kupunguza mzigo kwa halmashauri na kulinda afya za wananchi.Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori alisema kuwa lengo la uzinduzi huo wa ugawaji wa vitambulisho ni kuonesha umma kuwa Wilaya ya Ubungo inawajali Wazee ikiwa ni Sehemu ya utekelezaji wa ilani ya ushindi ya Chama Cha Mapinduzi katika kipindi Cha mwaka 2015-2020, sera ya Taifa ya Wazee ya mwaka 2003 na sera ya Afya ya Mwaka 2007.

Mhe Makori alisema kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya Uongozi wa Mheshimiwa Dkt John Pombe Magufuli imejipanga kuhakikisha Wazee wote nchini wanapata Huduma Bora za afya bila vikwao hivyo Wilaya ya Ubungo imeanza na utoaji vitambulisho kea Wazee 7296 waliojiandikisha na zoezi hilo litakuwa endelevu.

Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akizungumza na mtandao wa www.wazo-huru.blogspot.com mara baada ya uzinduzi wa ugawaji wa vitambulisho vya Tiba kwa Wazee alisema kuwa Manispaa ya Ubungo imetekeleza agizo la serikali lililotolewa na Waziri Mkuu kwenye maadhimisho ya siku ya Wazee Octoba 1, 2009 kuwa Hospitali zote na Vituo vya Afya vya Umma kutenga dirisha na watumishi maalumu wa Afya kwa ajili ya kutoa Huduma za matibabu bure kwa Wazee.

Mkurugenzi Kayombo alisema kuwa Manispaa ya Ubungo ina jumla ya Vituo 19 vya kutolea Huduma za afya ikiwa ni pamoja na Hospitali moja, Vituo vya afya vitatu, Zahanati 15, na Kliniki Moja ya Mama na Mtoto hivyo Vituo hivyo vyote vitaanza kutoa Huduma za matibabu kwa Wazee wasio na uwezo bila malipo.

KAMPENI YA UZALENDO KWANZA YAZINDULIWA JIJINI DAR,KUHAMASISHWA NCHI NZIMA

Mwenyekiti wa Kampeni ya Uzalendo Kwanza, Steven Mengele almaarufu kwa jina la kisanii Steven Nyerere, akizungumza mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo jijini Dar kuhusina na uzinduzi wa kampeni yao itakayojulikana kwa jina la UZALENDO KWANZA. Pichani kulia ni Msanii wa Filamu Wastara na kulia kwake ni Misayo Ndumbagwe.

kampeni hiyo imezinduliwa rasmi leo, ikiwa na lengo la kuunga mkono jitihada na juhudi zinazofanywa na Rais Dkt John Pombe Magufuli katika suala zima la kuhakikisha Tanzania inasonga mbele kimaendeleo ambapo wasanii wa muziki na filamu wapatao 250 wameshirkishwa pamoja na wachezaji wa mpira.

Steve amesema kuwa, ni wakati sasa kwa Watanzania kujenga utamaduni wa kuvienzi na kuvipenda vitu vyao kwa namna moja ama nyingine katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo, kwa sababu nchi ni Yetu,rasimali zilizopo ni zetu,madini ni yetu,mbuga za wanyama ni vya kwetu, hivyo ni muhimu Watanzania wakaamka sasa na kuonesha uzalendo wao halisi kama ambavyo Rais Dkt John Pombe Magufuli amekuwa akionesha kwa vitendo na kusisitiza suala zima la Uzalendo ndani ya nchi yetu.

"Sisi kama Wasanii, kwa moyo mmoja tumeamua kushikamana kwa pamoja na baraka zote tunazo kushikamana na kuiunga mkono kauli mbiu ya Rais Dkt Joh Pombe Magufuli ya UZALENDO KWANZA kuwa na harakati za kuifanya Tanzania yetu na Watanzania wenyewe kuwa Wazalendo kwa nchi yao",alisema Steve Nyerere na kuongeza kuwa kauli mbiu hiyo sio kwa ajili ya Dar Es Salaam tu bali,ni kwa ajili ya Tanzania nzima.
Wasanii wa mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa kampeni ya UZALENDO KWANZA.
Mwenyekiti wa Kampeni ya Uzalendo Kwanza Steven Mengele almaarufu kwa jina la kisanii Steven Nyerere akitoa ufafanuzi zaidi kuhusina na kampeni hiyo ya UZALENDO KWANZA mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani)  jijini Dar,kampeni hiyo inatarajia kuhamasishwa mikoa mbalimbali nchini .Pichani kushoto ni Msanii wa Filamu ni Misayo Ndumbagwe pamoja na Kemmy .
Baadhi ya Wasanii mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo wa uzinduzi wa kampeni hiyo ya UZALENDO KWANZA,itakayosambazwa nchi nzima kuhakikisha wananchi wanaelewa dhana nzima ya kuwa mzalendo na nchi yako.
Mkutano ukiendelea mapema leo wa uzinduzi wa kampeni ya UZALENDO KWANZA.
Msanii wa Filamu Wastara Juma akiwahimiza Watanzania kuwa WAZALENDO KWANZA katika mambo mbalimbali ikiwemo kuvithamini vya vyumbani,pia amewaomba Watanzania kuwaunga mkono Wasanii wao kwa kununu kazi zao zilizo halisi na halali ili kuhakikisha dhama nzima ya UZALENDO KWANZA inatimia.
Baadhi ya Wasanii wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri wakati wa uzinduzi wa kampeni ya UZALENDO KWANZA,itakayopita mikoa mbalimbali kuwahamasisha wananchi kuwa Wazalendo na nchi yao na pia kumuunga mkono Rais Dkt John Pombe Magufuli katika suala zima la kuhakikisha Tanzania inasonga mbele kimaendeleo.

SPIKA NDUGAI AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA UONGOZI LEO MJINI DODOMA

 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (katikati)akiongoza kikao cha kamati ya uongozi kilichofanyika leo katika ukumbi wa Spika Mjini Dodoma, ikiwa ni Maandalizi kabla ya kuanza Mkutano wa 8 wa Bunge la 11 unaoendelea leo tarehe 5 Septemba, 2017 Mjini Dodoma.
 Naibu Spika wa Bunge, Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson akizungumza jambo wakati wa kikao cha kamati ya uongozi kilichofanyika leo katika ukumbi wa Spika Mjini Dodoma, ikiwa ni Maandalizi kabla ya kuanza Mkutano wa 8 wa Bunge la 11 unaoendelea leo tarehe 5 Septemba, 2017 Mjini Dodoma. kushoto ni Katibu wa Bunge, Dkt. Thomas kashililah.
Wajumbe wa kamati ya uongozi wakiwa katika kikao cha pamoja kilichoongozwa  na Spika wa Bunge katika ukumbi wa Spika Mjini Dodoma, ikiwa ni Maandalizi kabla ya kuanza Mkutano wa 8 wa Bunge la 11 unaoendelea leo tarehe 5 Septemba, 2017 Mjini Dodoma.  kulia ni Mhe. Andrew Chenge, Mhe. Stanslaus Nyongo (katikati) na Mhe. Christine Ishengoma (kushoto).

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

Monday, September 04, 2017

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA ARDHI, MALIASILI NA UTALII YAUNGA MKONO KUFUTWA KWA KITONGOJI KILICHOANZISHWA KINYUME CHA SHERIA NDANI YA HIFADHI YA TAIFA YA SAADAN


 Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki (kushoto) akimkaribisha Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mhandisi atashasta Ndetiye kwa ajili ya kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Saadan hususan eneo lenye mgogoro wa ardhi baina ya kitongoji cha Uvinje na Hifadhi hiyo wakati wa ziara ya kamati hiyo wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani jana. Wananchi wa kitongoji hicho ambao wameweka makazi ndani ya hifadhi hiyo kinyume cha sheria wametakiwa kuondoka kwa hiari katika kipindi cha mwezi mmoja kupisha eneo la hifadhi kabda ya kuondolewa kwa nguvu ambapo watalipwa fidia.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mhandisi Atashasta Ndetiye (wa tatu kushoto) akizungumza na wananchi wa Kitongoji cha Uvinje wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani kuhusu mgogoro wa ardhi baina ya kitongoji hicho na Hifadhi ya Taifa ya Saadan wakati wa ziara ya kamati hiyo wilayani humo jana. Wananchi wa kitongoji hicho ambao wameweka makazi ndani ya hifadhi hiyo kinyume cha sheria wametakiwa kuondoka kwa hiari katika kipindi cha mwezi mmoja kupisha eneo la hifadhi kabda ya kuondolewa kwa nguvu ambapo watalipwa fidia.Wengine pichani ni Naibu Waziri,Wizara ya Maliasili, Mhandisi Ramo Makani(wa pili kulia) na  Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Majid Hemed Mwanga (kulia).
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani (wa tatu kushoto) akiongoza Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kutembelea eneo lenye mgogoro baina ya Kitongoji cha Uvinje na Hifadhi ya Taifa ya Saadan wakati wa ziara ya kamati hiyo kwenye eneo hilo wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani jana. Wananchi wa kitongoji hicho ambao wameweka makazi ndani ya hifadhi hiyo kinyume cha sheria wametakiwa kuondoka kwa hiari katika kipindi cha mwezi mmoja kupisha eneo la hifadhi kabda ya kuondolewa kwa nguvu ambapo watalipwa fidia. Wengine pichani ni Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhandisi Atashasta Ndetiye (wa nne kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Alhaj Majid Hemed Mwanga (wa pili kushoto).
Wajumbe wa kamati hiyo wakijadili baadhi ya mambo waliyoyaona katika eneo hilo lenye mgogoro.
 Mkurugenzi wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Mtango Mtahiko ambaye alimuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo  akiwasilisha taarifa ya Shirika hiyo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii ilipotembelea Hifadhi ya Taifa ya Saadan jana wilayani Bagamoyo.
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Alhaj Majid Hemed Mwanga (kushoto) akizungumza na wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kuhusu mgogoro baina ya kitongoji cha Uvinje na Hifadhi ya Taifa ya Saadan.
Wajumbe wa kamati wakikagua eneo hilo la mgogoro.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA),ambaye alikuwa Muhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Saadan Dkt. James Wakibara (kulia) akiteta jambo na Kaimu Mkurugenzi wa Biashara na Utalii wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Imani Nkuwi kandokando ya fukwe  za Hifadhi ya Taifa ya Saadan wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii wilayani Bagamoyo jana.
 Baadhi ya maofisa wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) wakitembelea fukwe za Hifadhi ya Taifa ya Saadan wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii wilayani Bagamoyo jana.
 Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Paschal Shelutete (kushoto) na Katibu wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Gerald Magiri wakitembelea fukwe za Hifadhi ya Taifa ya Saadan wakati wa ziara ya kamati hiyo kwenye hifadhi hiyo jana.
 Mwenyekiti wa kitongoji cha Uvinje, Hussein Akida akitoa maoni yake kuhusu mgogoro huo mbele ya kamati ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii jana. Kulia ni Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhandisi Atashasta Ndetiye.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuri (katikati), Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Dkt. James Wakibara (kulia) na Mkurugenzi wa Idara ya Mipango Wizara hiyo, Dkt. Iddi Mfunda wakisikiliza maoni ya wananchi wa kitongoji cha Uvinje katika mkutano wa hadhara wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii wilayani Bagamoyo jana.
 Baadhi ya wananchi wa kitongoji hicho wakitoa maoni yao mbele ya kamati.
 Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Moses Nnauye (kulia) akizungumza na wananchi wa Kitongoji cha Uvinje wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani kuhusu mgogoro wa ardhi baina ya kitongoji hicho na Hifadhi ya Taifa ya Saadan wakati wa ziara ya kamati hiyo wilayani humo jana. Wananchi hao ambao wameweka makazi ndani ya hifadhi hiyo wametakiwa kuondoka katika kipindi cha mwezi mmoja kupisha eneo la hifadhi ambapo watalipwa fidiaNyuma yake kulia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhandisi Atashasta Ndetiye.
 Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Moses Nnauye (kushoto) akizungumza na wananchi wa Kitongoji cha Uvinje wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani kuhusu mgogoro wa ardhi baina ya kitongoji hicho na Hifadhi ya Taifa ya Saadan wakati wa ziara ya kamati hiyo wilayani humo jana. Wananchi wa kitongoji hicho ambao wameweka makazi ndani ya hifadhi hiyo kinyume cha sheria wametakiwa kuondoka kwa hiari katika kipindi cha mwezi mmoja kupisha eneo la hifadhi kabda ya kuondolewa kwa nguvu ambapo watalipwa fidia.  Wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhandisi Atashasta Ndetiye.





Nyumba inayodaiwa kuwa ni ya muwekezaji anaeshikilia moja ya eneo katika hifadhi ya taifa ya Saadan kwa madai kuwa alipimiwa eneo hilo na Serikali. Taarifa zilitolewa ni kuwa eneo hilo lilipimwa kiholela bila ya kufuata taratibu za kisheria. Hata hivyo licha ya muwekezaji huyo kutoka nchini Botswana kukaa katika eneo hilo kwa zaidi ya miaka tisa ameonekana hajaendeleza eneo hilo kwa lengo lililokusidiwa.

NA HAMZA TEMBA - WMU.

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii imeunga mkono uamuzi uliofikiwa na kamati maalum iliyoundwa na Serikali ya Wilaya ya Bagamoyo kwa ajili ya kutafuta suluhu ya kumaliza mgogoro wa ardhi baina ya Hifadhi ya Taifa ya Saadan na wananchi wa kitongoji cha Uvinje walioanzisha makazi ya kudumu ndani ya hifadhi ya Taifa ya Saadan kinyume cha sheria.

Kamati hiyo iliyoundwa na wajumbe watatu ambao ni Serikali ya Wilaya ya Bagamoyo, Uongozi wa Kitongoji cha Uvinje na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania(TANAPA) kupitia Hifadhi ya Taifa ya Saadan ilifikia maazimio kuwa wananchi wa kitongoji hicho walioanzisha makazi ndani hifadhi hiyo waondolewe kwa utaratibu wa kulipwa fidia ili kumaliza mgogoro huo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Wilayani Bagamoyo, Mwenyekii wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii, Mhandisi Atashasta Ndetiye alisema baada ya kutembelea eneo hilo wamejiridhisha kuwa Kitongoji hicho cha Uvinje kimeanzishwa ndani ya eneo la hifadhi ambapo ni kinyume cha sheria. 

"Kiuhalisia tumeona kuna kitongoji ndani ya hifadhi ya Taifa ya Saadan, tumewasikiliza wananchi, tumesikiliza upande wa Serikali, kwa mujibu wa taratibu na sheria wale wananchi wanapaswa watoe ushirikiano, tunaamini kuna taratibu za Kiserikali zinafanywa kuhakikisha wale wananchi wanalipwa ili waondoke kwa usalama" alisema Ndetiye.

Aliongeza, "tumeona jinsi ambavyo baadhi ya wananchi hawako tayari kulipwa, lakini nadhani wakieleweshwa vizuri wataelewa kuwa ile ni hifadhi ya Taifa, na kama ni hifadhi ya Taifa basi inahusu maslahi ya Taifa, hivyo kila mwananchi anatakiwa atoe ushirikiano ili angalao Serikali ifanye uwekezaji wa kueleweka"

Ndetiye alisema kamati hiyo imeshaweka maazimio kwa ajili ya kushauri Bunge ili liazimie ni nini kifanywe na Serikali kumaliza mgogoro huo. Alisema, "Kwa udharura wake na kutokana na maelezo ya mkuu wa Wilaya, kwa ujumla kamati inakubaliana nayo kwasababu ameeleza vitu ambavyo tumeona vina tija zaidi kwa watanzania na tunaenda kulishauri Bunge na Serikali haraka iwezekanavyo ili hatua ziweze kuchukuliwa kumaliza mgogoro huo".

Awali akielezea kuhusu mgogoro huo Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Majid Hemed Mwanga alisema baada ya maazimio ya kamati iliyoundwa na Serikali ya wilaya kumaliza mgogoro huo baadhi ya wananchi walikubali maazimio yaliyowekwa ya kulipwa fidia huku wengine wakikaidi kuondoka akiwemo muwekezaji aliyeshikilia sehemu ya eneo hilo kwa zaidi ya miaka tisa bila kuwekeza mradi uliokusudiwa ambapo wamepewa kipindi cha mwezi mmoja waondoke kwa hiari kabla ya nguvu kutumika kuwaondoa.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Uvinje,  Hussein Akida alisema kitongoji hicho kilianzishwa ndani ya kijiji cha Saadan katika Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani zaidi ya miaka 100 iliyopita huku kikiwa na ukubwa hekta 3,000 na mpaka sasa Kitongoji hicho kina wakazi wasiopungua 72. Aliiomba Serikali kutambua mipaka ya kitongoji hicho pamoja na kuwasogezea wananchi  huduma za kijamii.

Baadhi ya wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii walitilia mashaka uwiano wa kimahesabu wa taarifa hiyo na uhalisia ambapo walihoji iweje kitongoji chenye miaka mingi kiasi hicho kiwe bado hakijapewa hati ya kuwa kijiji kamili pamoja na idadi ndogo ya wananchi wasiongezeka ndani ya muda mrefu wa miaka zaidi ya 100 toka kuanzishwa kwa Kitongoji hicho.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani alisema, mgogoro huo uko wazi na unapaswa kumalizika mara moja kwa kuwa Serikali ya Wilaya kupitia kamati iliyoundwa imeshafikia maazimio ya kuwaondoa wananchi walioanzisha makazi ndani ya eneo la hifadhi kinyume cha Sheria. Alitoa wito kwa wananchi kutii sheria za hifadhi na kuheshimu mipaka iliyowekwa kuepusha migogoro isiyo ya lazima baina ya Serikali na wananchi.

WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU AMPONGEZA NDEJEMBI, AMSIFIA KWA UADILIFU NA UCHAPAKAZI

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba , amempongeza Mhe. Deogratius John Ndejembi kwa kuaminiwa ...