Monday, November 02, 2015

VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA WAKUTANA

Msajili wa vyama vya siasa nchini,Jaji Mstaafu ,Francis Mtungi akiarisha mkutano wa vyama vya siasa ulioandaliwa kwa ajili ya kumuaga Rais Dk.Jakaya Kikkwete leo jijini Dar es Salaam.

.Mchambuzi wa wa Masuala ya Siasa na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Dk.Benson Bana akizungumza na waandishi wa habari juu hali ya siasa nchini leo katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Aliyekuwa Mgombea Urais wa TLP,Maxmillian Lymo akifafanua jambo kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.

Makamu Mwenyekiti wa CCM, Phillip Mangula( Kushoto) akizungumza na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Labour Patry (TLP), Agustino Lyatonga Mrema  (kulia ) na katikati Mgombea Urais, Maxmillian Lymo  jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti  Taifa  wa chama cha  (AFD)  Said Soud Said akifafanua jambo kwa wandishi wa habari  leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Emmanuel Massaka wa Globu  ya Jamii

WAKAGUZI WATAKIWA KUZINGATIA WELEDI

Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT), Bw. Gerald Mwanilwa akizungumza na Mgeni rasmi wa mafunzo ya program ya TEAMMATE kwa ajili ya wakaguzi kutoka NAOT na Wizara ya Fedha, Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Bibi Wendy Massoy. Kushoto ni Bw. Slyvester Kibona, Mkaguzi Mkuu wa Nje wa Mkoa wa Morogoro. Mafunzo hayo yanafanyika mkoani Morogoro kuanzia tarehe 02 hadi 06 Novemba, 2015.
Mkurugenzi wa msaidizi (Mafunzo) Bibi Felister Tirutangwa akizungumza wakati wa mafunzo ya program ya TEAMMATE kwa ajili ya wakaguzi kutoka NAOT na Wizara ya Fedha. Mafunzo hayo yanafanyika mkoani Morogoro kuanzia tarehe 02 hadi 06 Novemba, 2015.
Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT) na Wizara ya Fedha wakifuatilia kwa umakini mafunzo  ya program ya TEAMMATE. Mafunzo hayo yanafanyika mkoani Morogoro kuanzia tarehe 02 hadi 06 Novemba, 2015.
Mgeni rasmi wa mafunzo ya program ya TEAMMATE kwa ajili ya wakaguzi kutoka NAOT na Wizara ya Fedha, Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Bibi Wendy Massoy akizungumza na wanahabari kuhusu mafunzo hayo.

Mgeni rasmi wa mafunzo ya program ya TEAMMATE kwa ajili ya wakaguzi kutoka NAOT na Wizara ya Fedha, Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Bibi Wendy Massoy akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wanaohudhuria mafunzo hayo.
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT), Bw. Gerald Mwanilwa akizungumza na wanahabari kuhusu mchango wa Serikali ya Awamu ya Nne katika kuhakikisha uhuru wa CAG unapatikana.


Na Mwandishi wetu, Morogoro
Watumishi wa umma nchini wenye fani ya ukaguzi, wametakiwa kutumia weledi katika utendaji kazi zao hali itakayoongeza ufanisi katika usimamizi wa rasilimali za umma.

Wito huo umetolewa na Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Bibi Wendy Massoy wakati akifungua mafunzo ya program ya TEAMMATE kwa ajili ya wakaguzi kutoka Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi na Wizara ya Fedha.

Bibi Massoy amesema, viwango vya ukaguzi Kimataifa vinahitaji mkaguzi kuhifadhi taarifa zake za ukaguzi vizuri ili kuwezesha mkaguzi mwengine kuweza kufikia hitimisho moja kulingana na kazi iliyofanywa na Mkaguzi mwengine.

“Programu ya TEAMMATE hutoa fursa kwa wakaguzi kwa kuwawezesha  kuhifadhi taarifa zake za ukaguzi vizuri hivyo kuwafanya kutii viwango vya ukaguzi Kimataifa vya ukaguzi,” alisema Bibi Massoy.

Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ameongeza kuwa mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo wakaguzi hao katika kazi yao ya ukaguzi.

“Nawasihi muweze kutumia fursa hii kujiendeleza na kutekeleza utaratibu wa kaguzi wa mwongozo kwa vile wengi wa hatua na taratibu wamekuwa umeboreshwa katika Teammate Programu.

Akizungumzia mchango wa Serikali ya Awamu ya Nne katika kuiboresha Ofisi ya CAG, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala, Bw. Gerald Mwanilwa alisema kwa kiasi kikubwa mafanikio ya Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi imechagizwa na uamuzi wa dhati wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuimarisha taasisi za utawala bora, maadili na udhibiti, ikiwemo NAOT.

Bw. Mwanilwa aliongeza kuwa Rais alifanya hivyo kwa kuboresha sheria, kuongeza uhuru wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, kuongeza uwazi wa taarifa za Ofisi hiyo kwa kupeleka Ripoti za CAG kwa mara ya kwanza Bungeni pamoja na kuboresha mazingira ya kazi.

“Kwa mara ya kwanza Rais Jakaya Mrisho Kikwete aliitisha vikao mbalimbali, kwa nyakati tofauti na Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya na Mamlaka za Serikali za Mitaa kusisitiza umuhimu wa kuzipitia na kuzifanyia kazi taarifa zinazotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali. Hii imeleta mwamko mpya katika kuona umuhimu wa ripoti hizi na kutumika katika kufanya maamuzi mbalimbali serikalini,” alisema.

Bw. Mwanilwa aliongeza Katika Uongozi wa Awamu ya Nne NAOT ilishuhudia uanzishwaji wa Sheria ya Ukaguzi wa Umma, ambapo serikali ilitunga Sheria ya Ukaguzi wa Umma ya Mwaka 2008 pamoja na kanuni zake za mwaka 2009. Sheria hii iliongeza wigo na uhuru wa Ofisi hii katika kutekeleza majukumu yake Kikatiba.

Kuhusu Bajeti ya uendeshaji wa NAOT, Bw. Mwanilwa aliongeza: “Rais Kikwete aliongeza Bajeti ya Ofisi ya Ukaguzi ambapo Serikali iliboresha utaratibu na mchakato mzima wa kupitisha bajeti ya Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali uliowezesha bajeti ya Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi kuongezeka kwa asilimia 306% katika kipindi cha miaka mitano, kuanzia mwaka wa fedha wa 2008/9 hadi 2013/14.”

Jumla ya wakaguzi 65 kutoka Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi na kutoka 25 Wizara ya Fedha wanahudhuria mafunzo hayo ya siku tano yanayofanyika mkoani Morogoro.

AYSHAROSE AWASHUKURU WALIOMPIGIA KURA MAGUFULI

sin1
Na mwandishi wetu
MBUNGE mteule wa Viti Maalumu Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe, amesema ushindi wa kishindo wa Dk. John Magufuli, ni ishara kuwa watanzania wanataka mabadiliko ya maendeleo na si bora mabadiliko.
Amesema ana imani kubwa watanzania hawatajutia uamuzi wala kura zao walizompigia Dk. Magufuli kwa kuwa, yote aliyoahidi yanakwenda kufanyiwa kazi na hatimaye Tanzania kuwa ya tofauti katika muda mfupi ujao.
Aidha, amesema uchaguzi umemalizika kwa amani na watanzania wamefanya uamuzi sahihi hivyo, kilichobaki ni wote kuungana na kufanya kazi kwa bidii ili kuleta mabadiliko yanayokusidiwa.
Aliyasema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kutoa shukrani zake kwa Watanzania na wananchi wa Singida kwa kumchagua Dk. Magufuli na wagombea ubunge na udiwani wa CCM.
Alisema wananchi wa Singida wameonyesha mshikamano mkubwa na ukomavu wa kisiasa kwa kujitokeza kwa wingi kwenye mikutano ya hadhara kusikiliza sera na baadaye kufanya uamujzi sahihi wa kuwachagua kwa kishindo wagombea wa CCM.
“Niko hapa kuwashukuru Watanzania wote kwa kufanya uamuzi sahihi wa kumchagua mgombea urais wetu, Dk. John Magufuli kwa kishindo na hatimaye kutangazwa kuwa mshindi.
“Uamuzi waliofanya umetokana na CCM kusimamisha mtu makini, mwadilifu na mwenye dhamira ya dhati ya kutuletea maendeleo ya haraka na ya kweli. Kazi kubwa iliyopo mbele yetu ni kuungana na kufanya kazi kwa bidii kutimiza ndoto za watanzania. Falsafa yetu ya HapaKaziTu ndiyo inakwenda kutekelezwa sasa,” alisema Aysharose.
Mbunge huyo mteule, ambaye amejizolea sifa na umaarufu mkubwa kutokana na kupambana kikamilifu katika kusaka ushindi wa wagombea wa CCM katika ngazi ya utais, ubunge na madiwani, alisema amejipanga kuhakikisha anatatua changamoto zinazowakabili wanawake na vijana.
Alisema wakati wa kampeni, alizunguka katika maeneo mbalimbali mkoani Singida na huko alikutana na kero mbalimbali ambazo tayari ameanza kuzifanyia kazi kabla ya kuwapishwa kuwa mbunge.
Aysharose alisema changamoto ya huduma za afya na uwezeshaji kiuchumi kwa akinamama na vijana ndiyo kitakuwa kipaumbele chake cha kwanza mara baada ya kuapishwa.
“Nimeona changamoto nyingi, lakini kwa kuanzia nitaweka nguvu katika huduma za afya na uwezeshaji kiuchumi kwa wanawake ili kuwawezesha kukua kiuchumi. Natambua kuwa ukimuwezesha mwanamke basi umewezesha familia nzima kusonga mbele kimaendeleo na hili, nitalipa msukumo wa aina yake,” alisema.

NYALANDU APONGEZA ASKARI KWA KUMNASA JANGILI SUGU

sin2
Na mwandishi wetu
JITIHADA za serikali kwenye mapambano dhidi ya ujangili zinaendelea kuzaa matunda baada ya Kikosi cha Kupambana na Ujangili kumkamata mtuhumiwa mkuu wa ujangili anayejulikana kama Shetani.
Kukamatwa kwa jangili huyo kumetokana na jitihada za usiku na mchana zilizofanywa kwa ushirikiano wa Wizara ya Maliasili na Utalii na wadau wengine hususan askari wa wanyamapori kwa kipindi cha mwaka mmoja kwenye maeneo mbalimbali ya uhifadhi nchini.
Akizungumza na UHURU wakati akielekea jijini London, Uingereza kwa safari ya siku mbili ya kikazi, Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, alisema kazi iliyofanyika ni kubwa na inastahili pongezi.
Alisema majangili wamekuwa wakiisumbua serikali kwa kipindi kirefu lakini kutokana na jitihada za serikali na wadau wengine zikiwemo nchi wahisani wa maendeleo na jumuia za kimataifa hali inaendelea kuwa nzuri.
Alisema Shetani anakuwa wa pili kukamatwa baada ya Queen of Victory aliyekamatwa na serikali kipindi cha nyuma akiendelea na jitihada za kufanya uhalifu wa kuua na kuiba viungo vya wanyamapori wa Tanzania.
Waziri Nyalandu alisema serikali itaendelea na mapambano ya kuwasaka na kuwachukulia hatua za kisheria vigogo wa ujangili na wanaowasaidia kufanikisha uhalifu huo hapa nchini.
Alisema akiwa jijini London atahudhuria mkutano wa Mawaziri wa Utalii kutoka nchi mbalimbali zikiwemo za Afrika Mashariki, ambao watazungumza mambo mbalimbali yanayohusu namna za kuendeleza sekta ya Utalii katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Alisema pia mkutano huo utahudhuriwa na Mwanahabari maarufu wa Shirika la Habari la CNN, Richard Quest atakayefanya mahojiano maalumu kuhusu masuala ya Utalii na Maliasili.
Kuhusu hali ya siasa nchini, Nyalandu alisema uchaguzi umeisha na  kwamba viongozi walioshinda wanapaswa kufahamu kuwa si wao walioshinda bali ni watanzania kwa ujumla hivyo wawe wamoja kuijenga Tanzania.

KAMA ULIKOSA KIPINDI CHA MKASI CHA SALAMA JABIR NA MO DEWJI TAZAMA HAPA

IMG-20151030-WA0039
 : Kipindi extended na  bonyeza play hapa chini

RAIS KIKWETE AMTEUA RAMADHAN KASWA KUWA KATIBU TAWALA WA MKOA LINDI

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua  Ndugu Ramadhan Kaswa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi kuanzia Oktoba  30, mwaka huu, 2015.

          Kabla ya uteuzi wake, Ndugu Kaswa alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa Msaidizi,  Mkoa wa Tanga.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
2 Novemba, 2015

PUMZIKA WA AMANI MAREHEMU ANNETH CHRISTIAN KAJURA

Mume wa marehemu akitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa mke wake Anneth Christian mwishoni mwa wiki iliyopita nyumbani kwa marehemu Mbezi Beach - SalaSala Jijini Dar es Salaam na baadae maziko yalifanyika Makaburi ya Kondo - Bahari Beach.
 Mmoja ya wanandugu akitoa heshima ya mwisho.
 Mume wa marehemu Anneth Christian akiweka mchanga katika kaburi la mke wake katika Makaburi ya Kondo - Bahari Beach.
 Mama wa marehemu akitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa mwanae Anneth Christian mwishoni mwa wiki iliyopita nyumbani kwa marehemu Mbezi Beach - SalaSala Jijini Dar es Salaam na baadae maziko yalifanyika Makaburi ya Kondo - Bahari Beach.
 Mume wa marehemu akiweka shahada la ua katika kaburi la mke wake katika Makaburi ya Kondo - Bahari Beach.
 Mtoto wa marehemu akiweka mchanga katika kaburi la mama yake.
 Mama wa marehem akiweka mchanga katika kaburi la mwanae.
 Wanafamilia wakiweka maua katika kaburi la Anneth Christian.
Mwili wa Marehemu Anneth Christian ukiingizwa nyumbani kwake Mbezi Beach - SalaSala Jijini Dar es Salaam na baadae maziko yalifanyika Makaburi ya Kondo - Bahari Beach.
 Waombolezaji.

WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU AMPONGEZA NDEJEMBI, AMSIFIA KWA UADILIFU NA UCHAPAKAZI

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba , amempongeza Mhe. Deogratius John Ndejembi kwa kuaminiwa ...