Sunday, July 05, 2009

Matokeo Biharamulo

MATOKEO ya awali ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Biharamulo Magharibi yameonyesha Chama cha Chadema kikikaba koo chama cha CCM kwa kura chache ambazo hata hivyo zinaweza kufikiwa na CCM.

Mpaka sasa asilimia 84 ya kura zimeshahesabiwa na matokeo yanaonyesha kuwa Chadema kimezoa asilimia 51.2 ya kura zote huku CCM kikipata asilimia 48.8 ya kura na TLP kimiambulia asilimia 0.65. Matokeo haya ni ya awali na hayajathibitishwa na tume ya uchaguzi.

Matokeo kamili yatatolewa kesho hivi sasa wanakusanya masanduku ya kura na matokeo kutoka bush na vyama vimekubaliana matokeo kesho. Tofauti na uchaguzi uliopita, matokeo ya uchaguzi wa Jimbo la Biharamulo yamekuwa ni ya kushangaza, kwani katika maeneo ya vijijini ambako ndiko kunakotarajiwa kuwa ngome ya chama tawala cha CCM baadhi ya kata zinaonyesha kuwa na kura nyingi za mgombea wa Chadema.

Lakini pia maeneo ya mijini ambayo yanaonekana kuwa ni ngome kubwa ya vyama vya upinzani, lakini kwa Biharamulo CCM ilionekana kuchuana vikali katika vituo na kata mbalimbali huku vituo vingine vyama hivyo vikilingana kwa kura. Matokeo kamili tutawaletea kesho.

dawa za kukuza matako, matiti



Pichani Meneja wa mawasiliano wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Gaudencia Simwanza akionyesha mojawapo ya dawa za kuongeza matako na matiti kwenye viwanja vya maonyesho vya Mwalimu Nyerere (DITF), dawa hizo zimeelezwa kuwa na athari zinazosababisha kansa.

Wakati huo huo TFDA imewatahadharisha wanawake wanaotumia vipodozi vya kuongeza makalio na matiti kwamba wanaweza kupata madhara ya figo, ubongo na kansa ya ngozi.

Mkaguzi wa dawa vipodozi na vifaa vya tiba wa TFDA Kissa Mwamwita alisema kumekuwa na wimbi kubwa la wanawake wanaotumia vipodozi hivyo ambavyo havijasajiliwa na mamlaka hiyo.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii, Mwamwita alisema vipodozi hivyo vimekuwa vikiingizwa nchini na kuuzwa kwa kificho huku ikidaiwa kuwa wateja wake wakubwa ni wanafunzi wa sekondari na wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu.

Mwamwita aliwataka wanawake wanaotumia vipodozi kuwa makini wakati wanaponunua vipodozi kwa kuangalia kama vimesajiliwa kwani vipo vipodozi vinavyouzwa kwa kificho.

“Matumizi ya vipodozi hivyo vinavyoongeza ukubwa wa makalio na matiti ni hatari kwa afya na pia yanawaweka katika hatari ya kupata magonjwa ya saratani,” alisema Mwamwita.

Alisema watumiaji wa vipodozi wanatakiwa kuwa makini wanapotaka kununua bidhaa hizo ili kuepuka kununua vipodozi vyenye viambata vya sumu.

Hata hivyo TFDA imetoa tahadhari kwa wananchi wanaoendelea kutumia vipodozi vyenye viambata vya sumu zikiwemo ‘losheni’ kuacha kutumia kwa kuwa kiafya vina madhara makubwa.

Mwamwita alitaja baadhi ya vipodozi vyenye viambata kuwa ni Chloqinone,Chloroform na Mercury Compound.

Foleni Ndefu


Baadhi ya wakazi wa mjini Biharamulo wakiwa katika foleni ya kwenda kupiga kura ya kumchagua mbuge wa Jimbo la Biharamulo Mgharibi kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika katika kituo cha Shule ya Msingi Umoja Mjini Biharamulo Mkoani Kagera jana wa kutafuta mirithi wa kiti hicho kilichoachwa wazi na Marehemu, Phares Kabyeu. Picha na Salhim Shao

Uchaguzi Biharamulo





Wananchi katika Jimbo la Biharamulo Magharibi mkoani Kagera leo wanapiga kura kumchagua mbunge wao baada ya kampeni za uchaguzi huo kukamilika jana huku ushindani ukitarajiwa kuwa mkali kati ya vyama vya Chadema na CCM.

Leo wanapiga kura kumchagua mbunge wao baada ya kampeni za uchaguzi huo kukamilika jana huku ushindani ukitarajiwa kuwa mkali kati ya vyama vya Chadema na CCM.

Katika uchaguzi huo, ambao kampeni zake zilitawaliwa na vurugu, kila chama kilifanya kampeni ya nguvu kutupa kete yake ya mwisho kujinadi kwa wapigakura.

CCM ilihitimisha kampeni zake Biharamulo mjini katika Uwanja wa Sokoni, huku Chadema ikihitimisha kampeni zake katika uwanja wa mpira mjini hapa.

Wanaochuana ni Dk Anthony Gervas Mbassa wa Chadema, Oscar Rwegasira Mukassa wa CCM na Mpeka Buhangaza wa TLP.

Katika uchaguzi huo vituo 238 vimetengwa kwa ajili ya kupigia kura na waliojiandikisha kupiga kura ni watu 87,189.


Lwakatare naye yumo Chadema.

Serena bingwa wimbledon 2009




Serena williams amejinyakulia ushindi wa kombe la Wimbledon mwaka huu. Serena alikuwa akichuana na dada yake Venus Williams na bingwa mtetezi wa kombe hilo amemtoa dadayake kwa seti mfululizo 7-6, na 6-2. hii inafanya jumla ya Grand slams 11ambazo Serena amesha shinda hadi hivi sasa. Venus ana Gland slams 7. Hongereni sasa Venus na Serena.

Thursday, July 02, 2009

Wake za Viongozi Ndani ya Libya



Mke wa Rais, mama Salma Kikwete (katikati) akiwa na wake wa viongozi katika mkutano wa 13 wa Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika(AU)huko Sirte, Libya. Picha na Freddy Maro/ Ikulu.

Wednesday, July 01, 2009

Umeme Zenji nomaaa



Watoto Said na Mwanakhamis Vuai wakijisomea nyumnbani kwao Umpendae jijini Zanzibar juzi usiku huku akitumia mshumaa kutokana na matatizo ya umeme yaliyokumba mji wa Zanzibar.pembeni yake ni Mamayake Kijakazi Mohamed Hassan. (Picha na Mpoki Bukuku)

RAIS SAMIA AKUTANA NA WAZEE WA MIKOA YOTE NCHINI, AFUNGUA UKURASA MPYA WA MAZUNGUMZO YA KITAIFA

  Dodoma, Agosti 27, 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amekutana na wazee wa Mkoa wa Dodoma pam...