Saturday, February 01, 2025

Rais Samia Akabidhi Mobile Clinic kwa Sikonge na Uyui






Dodoma, 1 Februari 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo amemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Paul Matiku Chacha, mfano wa ufunguo wa magari maalum ya huduma ya afya inayotembea (Mobile Clinic) kwa ajili ya Wilaya za Sikonge na Uyui.

Magari hayo yametolewa na Jakaya Kikwete Foundation kwa ufadhili wa Kampuni ya SC Johnson Family ya Marekani, ikiwa ni juhudi za kuboresha upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi wa maeneo husika. Hafla hiyo imefanyika Ikulu Chamwino, mkoani Dodoma.

No comments:

PPAA yatoa rai wazabuni kutumia moduli kuwasilisha rufaa

  Na Mwandishi wetu, Dar Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) imetoa rai kwa wazabuni kutumia Moduli ya kupokea na kushughulikia malal...