Wednesday, February 26, 2025

RAIS DKT. SAMIA AZUNGUMZA NA WANANCHI WA PANGANI, AZINDUA MIRADI YA MAENDELEO MKOANI TANGA










PANGANI, TANGA – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Februari 26, 2025, amezungumza na wananchi wa Wilaya ya Pangani, mkoani Tanga, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi ndani ya mkoa huo. Hii ni siku ya nne tangu aanze ziara yake, ambayo inalenga kukagua, kuzindua na kuweka jiwe la msingi katika miradi mbalimbali ya maendeleo.

Katika hotuba yake kwa wananchi wa Pangani, Mheshimiwa Rais amesisitiza dhamira ya serikali yake ya kuwaletea wananchi maendeleo endelevu kwa kuboresha miundombinu, sekta ya elimu, afya, na uchumi kwa ujumla. Aidha, amewapongeza wananchi wa Pangani kwa juhudi zao katika kuchangia maendeleo ya mkoa wa Tanga, hasa katika sekta ya uvuvi, kilimo na utalii.

Akiwa Pangani, Rais Dkt. Samia amezindua miradi kadhaa muhimu inayolenga kuinua hali ya maisha ya wananchi, ikiwemo ujenzi wa barabara, maboresho ya huduma za maji safi na salama, pamoja na mradi wa uboreshaji wa sekta ya afya. Miradi hii ni sehemu ya juhudi za serikali katika kuhakikisha maendeleo yanawafikia wananchi wa maeneo yote nchini.

Ziara ya Rais Dkt. Samia katika mkoa wa Tanga inatarajiwa kuendelea katika siku zijazo, ambapo ataendelea kukagua miradi ya maendeleo, kuzungumza na wananchi, na kuweka mikakati ya kuimarisha ustawi wa jamii.

Tuesday, February 25, 2025

RAIS SAMIA AFUNGUA SHULE YA SEKONDARI YA WASICHANA TANGA

  



Kilindi, Tanga – 25 Februari, 2025

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameendelea na ziara yake ya kikazi mkoani Tanga kwa kufungua rasmi Shule ya Sekondari ya Wasichana Tanga, iliyopo Mabalanga, katika Kijiji cha Michungwani, Wilaya ya Kilindi.

Shule hii ni moja ya juhudi za Serikali katika kuimarisha elimu ya watoto wa kike, hasa katika maeneo ya vijijini, ikiwa ni sehemu ya dhamira ya Rais Samia ya kuhakikisha fursa za elimu zinapanuka kwa wasichana nchini.

Katika hotuba yake, Mhe. Rais amesisitiza umuhimu wa uwekezaji katika elimu kama njia ya kuwawezesha wasichana kupata maarifa na ujuzi utakaowaandaa kwa maisha bora ya baadaye. Amesema kuwa Serikali itaendelea kujenga na kuboresha miundombinu ya shule kwa kuhakikisha zinakuwa na mabweni, madarasa ya kisasa, maabara, maktaba na huduma nyingine muhimu zitakazowasaidia wanafunzi kusoma katika mazingira bora.

"Serikali ya Awamu ya Sita inaendelea kuwekeza kwenye sekta ya elimu ili kuhakikisha kila mtoto wa Kitanzania anapata haki yake ya msingi ya elimu, bila vikwazo vyovyote. Ujenzi wa shule hii ni hatua muhimu katika kuwawezesha wasichana kupata fursa sawa za elimu," alisema Rais Samia.

Aidha, alitoa rai kwa jamii kushirikiana na Serikali katika kuwahimiza watoto wa kike kuhudhuria shule, kutokomeza vitendo vya ndoa za utotoni, na kuwajengea mazingira salama ya kujifunza.

Kwa upande wake, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, amepongeza juhudi za Serikali katika kuendelea kupanua wigo wa elimu nchini, akisema kuwa shule hiyo mpya itasaidia kupunguza changamoto ya wanafunzi kusafiri umbali mrefu kufuata elimu.

Mmoja wa wanafunzi waliopata fursa ya kusoma katika shule hiyo ameonesha shukrani kwa Rais Samia na Serikali kwa kutoa nafasi kwa wasichana kupata elimu bora, akisema kuwa sasa wataweza kutimiza ndoto zao bila vikwazo.

Ufunguzi wa shule hii ni sehemu ya mwendelezo wa uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita katika sekta ya elimu, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa shule mpya, mabweni, kuongeza idadi ya walimu, na kuimarisha mitaala ili kuleta matokeo chanya kwa mustakabali wa taifa.

SERIKALI, SEKTA BINAFSI KUIMARISHA HUDUMA ZA FEDHA NCHINI








📌 Dkt. Biteko afungua tawi la Exim Benki Kahama

📌 Exim yachangia vifaa vya matibabu vya shilingi milioni 25 Hospitali ya Wilaya Kahama

Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati

Uzinduzi wa tawi la Exim Bank Kahama ni uthibitisho wa ukuaji wa sekta ya benki, ushirikiano wa sekta binafsi na Serikali na dhamira ya kukuza uchumi wa wananchi. Aidha, Serikali imekuwa ikihimiza taasisi za fedha kuipeperusha bendera ya Tanzania nje ya nchi kwa kufanya uwekezaji wa kimkakati.

Hayo yameelezwa leo Februari 25, 2025 Kahama mkoani Shinyanga na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko wakati akizindua tawi la Benki ya Exim.

“ Kahama ni kitovu kikubwa cha shughuli za kiuchumi, hasa sekta ya madini ambayo inachangia kwa kiasi kikubwa kwenye pato la Taifa. Zaidi ya madini, mji huu pia ni maarufu katika sekta ya kilimo na biashara. Ni wazi kuwa ufanisi wa sekta hizi unategemea upatikanaji wa huduma za kifedha imara na zinazokidhi mahitaji ya wajasiriamali na wafanyabiashara,” amesema Dkt. Biteko.

Ameendelea “Hivyo, kwa kufungua tawi hili, Exim Benki inatoa fursa ya kipekee kwa wakazi wa Kahama kupata huduma za kifedha zinazoendana na shughuli zao za kiuchumi. Na kunaleta manufaa makubwa kwa jamii ya hapa Kahama, kwa wateja wengine wa benki na benki yenyewe kwa ujumla,”

Dkt. Biteko ametaja manufaa hayo kuwa ni kuongezeka kwa fursa za uchumi kwa kuongeza ajira, kuongeza mapato ya benki na hivyo kutumia sehemu ya faida yake kuchangia maendeleo ya jamii ikiwemo kusaidia makundi maalum kadhaa yenye uhitaji yaani (Corporate Social Responsibility - CSR)

Aidha, manufaa mengine ni kuongezeka kwa mapato ya kodi Serikalini na kuongezeka kwa ushindani wa huduma za kibenki.

Pia, Dkt. Biteko ameipongeza benki hiyo kwa hatua kubwa na kwa jitihada zake za kuleta huduma za kifedha karibu zaidi na wananchi pamoja na kuiwakilisha Tanzania  katika nchi za Comoros, Uganda, Djibouti, pamoja na Ethiopia.

Katika hatua nyingine, Dkt. Biteko ameipongeza Benki ya Exim kwa kuisaidia jamii kupitia Exim Cares “ Nimefurahi kusikia kuwa kabla ya kuzindua wa tawi hili tayari mmechangia vifaa vya matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama vyenye gharama ya zaidi ya shilingi milioni 25. Mchango huo wa vifaa vya matibabu utasaidia kuboresha huduma za afya kwa wananchi wa Kahama. Hatua kama hizi zinaonesha mshikamano wa sekta binafsi na Serikali katika kuboresha ustawi wa wananchi.”
 
Pia, amesema kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na sekta binafsi katika kuimarisha huduma za kifedha na kuhakikisha kuwa zinapatikana kwa urahisi na kwa ufanisi kwa kila Mtanzania.

Vilevile, Dkt. Biteko ametoa wito kwa Benki hiyo kuwashika mkono na kuwakuza vyema wananchi wa kawaida na wa hali ya chini ambao wao watakuwa ni wateja muhimu. Aidha, uchumi wa wananchi hao wa kawaida hukuwa kwa kasi kutokana na shughuli zao za kiuchumi na hivyo kuisaidia pia benki kukua.

Benki hiyo ya Exim inatarajiwa kuwasaidia wananchi wa Kahama wanaohitaji huduma za kibenki ili kukua kiuchumi kwa kutoa huduma mbalimbali kama vile fursa za kufungua akaunti, kupata mikopo, na kufanikisha malipo mbalimbali kwa njia salama na rahisi zaidi.

“ Niwatoe wasiwasi Benki ya Exim  kuwa Kahama inafedha na inaendelea kukuwa kwa sababu ya uwepo wa bandari kavu na katika sekta ya madini mfano Kabanga nikeli na bidii ya watu wa hapa ya kufanya kazi. Hapa ni soko kubwa na muone fahari watu wa Kahama wanatajirika kupitia benki yenu,” amemalizia Dkt. Biteko.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha amesema kuwa ufunguzi wa tawi la benki hiyo ni kielelezo kuwa shughuli za uchumi ni nyingi na zitaendelea kuimarishwa.

Ameongeza kuwa Mkoa huo una matawi ya benki 11 ambayo yote pia yapo Kahama hivyo  ni kiashiria kuwa Kahama ipo kibiashara na kuwa Mkoa huo uko tayari kushirikiana na benki hiyo.

Naye, Kamishna wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha kutoka Wizara ya Fedha, Dkt. Charles Mwamwaja amesema kuwa Serikali imeendelea kuweka mazingira mazuri ya kifedha na kuwa dira iliyopo imekuwa ikiwaongoza na ni mpango mkuu wa sekta ya fedha ulioandaliwa na Serikali umeweka mazingira wezeshi na moja ya manufaa yake ni kufunguliwa kwa tawi hilo la benki.

Akitaja idadi ya benki zilizopo nchini amesema kwa sasa kuna benki 44, matawi zaidi ya 1000 na wakala wa huduma za kibenki zaidi ya 100,000 na hivyo ukuaji wa benki umeongezeka.

“ Wizara tunaipongeza kwa dhati Benki ya Exim kwa kufungua tawi Kahama na kusogeza huduma hizi karibu na wananchi,” amesema Dkt. Mwamaja.

Pamoja na hayo, amesema kuwa kumekuwepo na changamoto ya watoa huduma wasio waaminifu na mikopo chechefu, hivyo Wizara kupitia Benki Kuu imeendelea  kukabiliana na changamoto hizo kwa kutoa elimu ya masuala ya fedha mijini na vijijini ili wananchi waelewe na kutumia fursa za fedha zilizopo.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim, Jaffari Matundu amesema kuwa uzinduzi huo unathibitisha dhamira ya benki hiyo ya kuleta suluhu ya masuala ya fedha na uwekezaji ambapo mwaka 1997 walizindua tawi la kwanza jijini Dar es salaam na kwa sasa taasisi hiyo ina wigo mpana wa kutoa huduma zake.

“ Benki yetu imekuwa ikishirikiana mwa karibu na watu wa Kahama kwa shughuli mbalimbali ambapo tumewajulisha wakazi kuhusu huduma zetu na kuwa mshirika wa kudumu wa fedha,” amesema Bw. Matundu.

Aidha, amesema benki hiyo si tu imesaidia katika sekta ya afya bali hata elimu, ubunifu na kuwezesha wajasiriamali wanawake.
 
“ Tutaongeza ushiriki wa kifedha kutoka kwa wafanyabiashara na wananchi wanaotafuta suluhu ya kifedha kwa ajili ya kuongeza ufanisi katika shughuli zao,” amebainisha Bw. Matundu.

Saturday, February 22, 2025

RAIS SAMIA ASHIRIKI NA KUTUNUKU TUZO ZA WASANII WA KOMEDI TANZANIA 2025

 










Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameshiriki kama mgeni rasmi katika hafla ya utoaji wa Tuzo za Wasanii wa Komedi Tanzania (Tanzania Comedy Awards) iliyofanyika leo, tarehe 22 Februari 2025, katika ukumbi wa The Super Dome, Masaki, jijini Dar es Salaam.

Hafla hii imewaleta pamoja wasanii mbalimbali wa vichekesho, wadau wa sanaa, na wageni mashuhuri, ikiwa ni sehemu ya kutambua na kuthamini mchango wa wasanii wa komedi katika kukuza sanaa na burudani nchini.

Katika hotuba yake, Rais Samia amepongeza juhudi za wasanii wa komedi kwa kuleta furaha na kuelimisha jamii kupitia sanaa yao. Ameeleza kuwa serikali itaendelea kuwaunga mkono wasanii kwa kuboresha mazingira ya kazi na kuhakikisha sanaa inachangia katika maendeleo ya taifa.

Aidha, Rais Samia amewataka wasanii kutumia vipaji vyao kuhamasisha amani, umoja, na mshikamano miongoni mwa Watanzania, hasa kuelekea uchaguzi mkuu ujao. Amesisitiza umuhimu wa sanaa katika kuleta mabadiliko chanya na kujenga jamii yenye maadili mema.

Tuzo za Wasanii wa Komedi Tanzania ni tukio la kila mwaka linalolenga kutambua na kusherehekea mafanikio ya wasanii wa vichekesho nchini. Hafla ya mwaka huu imekuwa ya kipekee kutokana na uwepo wa Rais Samia kama mgeni rasmi, hatua inayoonyesha dhamira ya serikali katika kuendeleza na kuthamini sekta ya sanaa na burudani.

Kwa kushiriki kwake, Rais Samia ameonyesha mfano wa kuigwa katika kuthamini na kuunga mkono juhudi za wasanii wa ndani, na kutoa wito kwa wadau wengine kujitokeza kusaidia kukuza vipaji na sekta ya sanaa kwa ujumla.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ashiriki kwenye hafla ya utoaji tuzo za Wasanii wa Komedi Tanzania (Tanzania Comedy Awards) katika ukumbi wa The Super Dome, Masaki Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 22 Februari, 2023.

*WATAFITI WA MIMEA VAMIZI WATUA SERENGETI










Na Sixmund Begashe - Serengeti 

Ziara ya kikazi ya watafiti wa mimea vamizi kutoka Jamhuri ya Cuba walioungana na wataalam wa ikolojia kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii katika Hifadhi ya Taifa Serengeti inatarajiwa kuwa neema kubwa kwa Wanyamapori kwenye Hifadhi hiyo, kwa kuongeza maeneo ya malisho kwa wanyama hao ambayo kwa sasa yameanza kuathiriwa na mimea vamizi.

Akizungumza na watafiti hao katika Hifadhi hiyo ya kipekee duniani, Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Serengeti, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi Stephano Msumi ameushukuru na  kuupongeza uongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii kwa hatua hiyo muhimu ya kuwakutanisha watafiti wa Wizara hiyo na kutoka nchi Cuba kutembelea Hifadhi ya Serengeti ili kujionea changamoto hiyo kwa lengo la kutafuta ufumbuzi wakudumu.

Aidha, amesema kuwa Hifadhi hiyo ni moja ya Hifadhi za Taifa zinazochangia kwa kiasi kikubwa katika pato la taifa kupitia utalii hususani wa Wanyamapori hivyo jitihada zinazofanywa na Serikali katika kuhakikisha Wanyamapori wanapata malisho ya kutosha ni za  kuungwa mkono. 

Ameongeza kuwa, zipo juhudi zinazofanywa na wataalam kutoka katika Hifadhi hiyo za kupambana na mimea vamizi lakini bado hazijazaa matunda yaliyotarajiwa, hivyo uwepo wa watafiti hao kutoka Cuba na kuungana na watafiti wa Wizara hiyo ni hatua muhimu katika kufikia malengo ya kuhakikisha malisho na usalama wa ikolojia ya Hifadhi hiyo ni endelevu.

Naye mtaalam mtambuzi wa mimea asili kutoka nchini Cuba, Dkt. Ramona Oviedo Prieto ametoa ushauri kwa wataalam wa ikolojia  wa Hifadhi ya Taifa Serengeti kuchukua hatua za haraka za kulinda kingo za Mto Mara uliopo ndani ya Hifadhi hiyo kwa kurejeresha mimea ya asili iliyokuwepo pembezoni mwa Mto huo.

Wakiwa kwenye Hifadhi ya Taifa Serengeti, timu hiyo ya watafiti walitembelea maeneo ya Seronera, Ikoma, Mto Mara na Machochwe na kushuhudia  mimea vamizi aina ya gugu karoti ( Parthenium hysterophorus) Chromolaena odorata na Opuntia ambayo ndio imeanza kusambaa kwenye maeneo hayo.

Friday, February 21, 2025

WAZIRI NDEJEMBI AAGIZA KUSIMAMISHWA KAZI KWA MKUU WA IDARA YA ARDHI HANDENI KWA KUCHOCHEA MIGOGORO YA ARDHI





Handeni, Tanga
– Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Deogratius Ndejembi, ameagiza kusimamishwa kazi kwa Mkuu wa Idara ya Ardhi wa Halmashauri ya Mji wa Handeni kwa madai ya kuhusika na kuzorotesha utatuzi wa migogoro ya ardhi katika eneo hilo.

Agizo hilo limetolewa Januari 20, 2025, wakati Waziri Ndejembi alipofanya ziara ya kikazi katika Wilaya ya Handeni, Mkoa wa Tanga. Akiwa katika eneo la Kwanjugo Kitalu A, ambapo wananchi wamekuwa wakilalamikia mashamba yao kuchukuliwa bila fidia kwa muda mrefu, Waziri Ndejembi aliweka wazi msimamo wa serikali kuhusu migogoro ya ardhi na uwajibikaji wa watendaji wa umma.

"Eneo hili lina historia yake. Palikuwa na umiliki wa wananchi wa asili, na sasa haiwezekani watu hawa kuonewa. Migogoro yote hii inatokana na kushindwa kuwasikiliza wananchi wetu. Ninamuelekeza Katibu Mkuu wa Wizara kumsimamisha kazi mara moja Mkuu wa Idara ya Ardhi wa Halmashauri na haraka sana aletwe mtu mwingine atakayeweza kutatua changamoto hizi za ardhi Handeni," amesema Waziri Ndejembi.

Timu ya Uchunguzi Kuundwa

Mbali na hatua hiyo, Waziri Ndejembi ameagiza kuundwa kwa timu maalum ya uchunguzi itakayokuwa chini ya Kamishna wa Ardhi. Timu hiyo inatarajiwa kuwasili Handeni ndani ya wiki moja ili kufanya tathmini ya kina kuhusu umiliki wa viwanja vya sasa na kubaini iwapo kuna watumishi wa ardhi waliojihusisha na unyakuzi wa ardhi ya wananchi.

"Lazima tuhakikishe haki inatendeka. Tunataka kujua wamiliki wa sasa wa viwanja ni akina nani, na kama kuna watumishi wa ardhi waliojihusisha na vitendo vya unyang’anyi wa ardhi, wachukuliwe hatua kali. Hatutaruhusu wananchi kunyanyaswa na watumishi wa umma," ameongeza Waziri.

Hatua Hii Inalenga Kurejesha Haki kwa Wananchi

Serikali kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha haki za wananchi katika masuala ya ardhi zinalindwa. Waziri Ndejembi amesisitiza kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi ya watendaji wote wa sekta ya ardhi wanaohusika na vitendo vya dhuluma na rushwa katika upangaji, ugawaji, na umiliki wa ardhi.

Ziara hii ni sehemu ya juhudi za serikali za kushughulikia migogoro ya ardhi nchini na kuhakikisha usimamizi bora wa rasilimali za ardhi kwa maendeleo ya taifa na ustawi wa wananchi.

Wednesday, February 19, 2025

🤝🌍 TANZANIA NA KOREA KUIMARISHA USHIRIKIANO KATIKA UCHUMI, TEKNOLOJIA NA AJIRA

 







Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango, leo Februari 19, 2025, amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Tanzania, Mhe. Eunju Ahn katika Ikulu ya Chamwino, Dodoma.

Katika mazungumzo hayo, Tanzania imeonesha dhamira ya kuimarisha uhusiano wake na Korea ambao umeendelea kuleta maendeleo katika sekta mbalimbali kama Elimu, Miundombinu, TEHAMA, Afya, Kilimo, Viwanda na Nishati tangu kuanzishwa kwake mwaka 1992.

🔹 Madini ya Kimkakati na Uchumi wa Kijani

Makamu wa Rais amepongeza ushirikiano kati ya Tanzania na Korea katika sekta ya madini ya kimkakati, akisisitiza kuwa rasilimali hizo zitaleta maendeleo makubwa kwa Tanzania hasa katika uchumi wa teknolojia za kijani 🌱⚡.

🔹 Kukuza Biashara na Uwekezaji

Mhe. Dkt. Mpango ameisihi Korea kuongeza kiwango cha biashara baina ya nchi hizo mbili na kuwahamasisha wawekezaji wa Korea kuja Tanzania ili kujionea fursa za uwekezaji katika sekta kama viwanda, ambapo kuongeza thamani kwa malighafi ndani ya nchi kutaongeza ajira na kuhamasisha uhamishaji wa teknolojia 🏭📈.

🔹 Ajira kwa Watanzania nchini Korea

Makamu wa Rais pia ameweka wazi dhamira ya Tanzania kushirikiana na Korea katika kubadilishana wafanyakazi, akisisitiza umuhimu wa Tanzania kujiunga na Mfumo wa Vibali vya Ajira (EPS). Mfumo huu utatoa fursa kwa Watanzania kufanya kazi Korea katika ujenzi wa meli 🚢, sekta ya viwanda 🏭, na kilimo cha kisasa 🌾.

🔹 Kuendeleza Elimu na Utaalamu wa Afya

Makamu wa Rais amesisitiza kuwa Tanzania ipo tayari kushirikiana na Korea katika mafunzo ya ubingwa kwa wataalamu wa afya, pamoja na kubadilishana utamaduni, michezo na lugha ya Kiswahili 📚🏅.

Kwa upande wake, Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Tanzania, Mhe. Eunju Ahn, ameahidi kuhakikisha makubaliano yote yanayolenga madini ya kimkakati na maendeleo ya uchumi wa buluu yanatekelezwa kwa haraka.

🇹🇿🤝🇰🇷 Uhusiano huu ni chachu ya maendeleo ya Tanzania!

Unazungumziaje hatua hii? Tag marafiki zako tujadili! 👇🏽

#TanzaniaKorea #UshirikianoWaMaendeleo #MadiniYaKimkakati #AjiraKwaWatanzania #UchumiWaKijani

MAKAMU WA RAIS DKT. PHILIP MPANGO AWATAKA WATANZANIA KUKEMEA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akihutubia wakati wa Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Wanawak...