Monday, November 11, 2024

Vodacom Tanzania, Soko la Hisa la Dar es Salaam kuwawezesha Watanzania kiuchumi, wazindua DSE Mini App ndani ya M-Pesa Super App

 Vodacom Tanzania Plc imetangaza rasmi kuingia katika ushirikiano wa kidijitali na Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), kwa kuzindua programu ya DSE Mini App kupitia M-Pesa Super App ya Vodacom.


Ushirikiano huu wa kimapinduzi unalenga kuleta mabadiliko katika upatikanaji wa masoko ya mitaji nchini Tanzania kwa kuwawezesha wawekezaji kununua, kuuza, na kusimamia uwekezaji wao katika his ana dhamana nyinginezo moja kwa moja kupitia simu zao za mkononi.

Programu hii ya DSE Mini App inatoa njia ya kibunifu inayowawezesha Watanzania kushiriki kwenye masoko ya kifedha, ikiwa ni sehemu ya kukuza ushirikishwaji wa kifedha na kuwawezesha wananchi kiuchumi.

DSE Mini App, iliyounganishwa kwenye M-Pesa Super App, inawawezesha watumiaji kufungua akaunti za uwekezaji, kununua na kuuza hisa na dhamana nyingine moja kwa moja kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam, kupata taarifa kwa haraka kuhusu mwenendo wa soko, na kupokea huduma za ushauri kutoka kwa madalali.

Programu hii pia inaonesha hali halisi na uwezo wa mwekezaji kwenye orodha yake ya uwekezaji na msaada wa huduma kwa wateja kutoka Vodacom kwa saa 24. Ushirikiano huu kati ya Vodacom Tanzania na Soko la Hisa la Dar es Salaam unaonesha jinsi teknolojia inavyoweza kuziba mapengo, na kufanya masoko ya kifedha kuwa shirikishi zaidi, yenye uwazi na yanayofikiwa na Watanzania wote."

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi wa M-Pesa Vodacom Tanzania, Epimack Mbeteni, alisema, "kwa kuunganishwa na DSE Mini App kwenye M-Pesa Super App, tunafanya masoko ya mitaji kuwa rahisi kufikiwa na Watanzania wote. Ushirikiano huu unaendana na lengo letu la kupanua ushirikishwaji wa kifedha kwa kutoa huduma za kidigitali zenye ubunifu zinazowawezesha wateja kuwekeza kwa urahisi na kukuza uchumi wao."

Programu ya DSE Mini App inawapa wawekezaji fursa muhimu kama vile uwezo wa kufungua akaunti za uwekezaji, kununua na kuuza his ana dhamana nyingine, kupata taarifa kuhusu kampuni zilizoorodheshwa, na kupata taarifa kwa haraka kuhusu mwenendo wa soko. Ushirikiano huu unatoa nafasi ya moja kwa moja kwa Watanzania kushiriki kwa urahisi na salama katika shughuli za masoko ya mitaji.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Soko la Hisa la Dar es salaam Peter Nalitolela, alisema, “Ushirikiano huu kati ya Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) na Vodacom M-Pesa ni uthibitisho wa nia ya dhati toka taasisi zote mbili ya kukuza ujumuishwaji wa wananchi katika huduma za kifedha.

DSE inategemea kutumia App ndogo ya DSE iliyopo katika M-Pesa kufikia uma wa Watanzania na kuwapa njia ya rahisi ya Watanzania wote kununua na kuuza his ana dhamana nyingine kwa urahisi popote pale walipo; hata majumbani mwao. Hii itawawezesha kukuza uwekezaji wao kwa manufaa yao binafsi nay a wale wawapendao”.

Ushirikiano kati ya Vodacom na DSE haujalenga tu kutoa ufikiwaji wa masoko ya mitaji ya Tanzania bali pia kuongeza uelewa na ushiriki kwenye soko la hisa. Programu ya DSE Mini App inarahisisha mchakato wa uwekezaji na inawapa watumiaji zana wanazohitaji ili kufanya maamuzi sahihi ya uwekezaji.
Mkurugenzi wa M-Pesa kutoka Vodacom Plc, Epimack Mbeteni (wa nne kutoka kushoto) akimpa mkono Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Peter Nalitolela baada ya kuingia katika ushirikiano wa kidijitali kwa kuzindua programu ya DSE Mini App katika M-Pesa Super App hivi karibuni jijini Dar es Salaam. DSE Mini App hii inawapa fursa wawekezaji kufungua akaunti za uwekezaji, kuuza na kununua hisa kwa njia rahisi na salama kupitia simu za mkononi.






 

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...