Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika
Mashariki, Mhe. Dennis Londo akikaribishwa na Naibu Waziri wa Mambo ya
Nje wa shirikisho la Urusi, Mhe. Bogdanov Mikhail Leonidovich
alipowasili kwa mazungumzo yaliyofanyika pembezoni mwa Mkutano wa Kwanza
wa Mawaziri wa Mambo ya Nje kutoka nchi za Afrika na Shirikisho la
Urusi unaofanyika tarehe 9 hadi 10 Novemba, 2024 mjini Sochi, Urusi
Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki, Mhe. Dennis Londo
amezinadi fursa za mbalimbali za kiuchumi ikiwemo uwekezaji, biashara na
utalii nchini Urusi wakati alipokutana kwa mazungumzo na Naibu Waziri
wa Mambo ya Nje wa shirikisho la Urusi, Mhe. Bogdanov Mikhail
Leonidovich.
Mazungumzo ya viongozi hao yamefanyika tarehe 10
Novemba, 2024 pembezoni mwa Mkutano wa Kwanza wa Mawaziri wa Mambo ya
Nje kutoka nchi za Afrika na Shirikisho la Urusi unaofanyika tarehe 9
hadi 10 Novemba, 2024 mjini Sochi, Urusi
Pamoja na mauala
mengine, wamejadili kuhusu Ushirikiano wa kihistoria uliopo kati ya
Tanzania na Urusi tangu enzi za Baba wa Taifa Hayati, Mwl. Julius
Kambarage Nyerere na kuhaidi kuendelea kuimarisha Ushirikiano huo kati
ya nchi hizi mbili.
Aidha, kwa upande wake Mhe. Londo
ameihakikishai Serikali ya Urusi kuwa Tanzania ina nia ya dhati ya
kuhakikisha ushirikiano katika sekta za Utalii, Uwekezaji, Biashara,
Kilimo, Afya, Viwanda una imarika na kukua kwa maendeleo endelevu ya
watu wake na mataifa hayo kwa ujumla.
Vilevile, Mhe. Naibu
Waziri Londo ameeleza kuhusu uwepo wa mazingira rafiki ya uwekezaji,
fursa mbalimbali za uwekezaji zinazopatikana nchini na maeneo ya
kimkakati ambayo Urusi inaweza kushirikiana na Tanzania ili kuleta tija
katika ushirikiano wake. Kadhalika, ametoa rai kwa wawekezaji na
wafanyabiashara kutoka Urusi kuchangamkia fursa nyingi za uwekezaji na
masoko zinazopatikana nchini.
Naye, Mhe. Leonidovich ameishukuru
Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kukuza ushirikiano na Urusi na
kuahidi kuwa Urusi imejizatiti kuhakikisha ushirikiano wake na Tanzania
unakuwa wenye manufaa makubwa kiuchumi na kidiplomasi kwa pande zote.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA
Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...
-
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu na timu ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwa katika ...
-
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2014 EXAMINATION RESULTS ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA ...
-
Adam Malima James Wanyancha Hamis Kagasheki RAIS Jakaya Kikwete ameteua Baraza la Mawaziri, huku likiwa na sura na damu mchanganyiko. Bar...
No comments:
Post a Comment