Benki
ya NMB imetoa msaada wa vifaa tiba kwa hospitali ya Jeshi la wananchi
Kanda ya Arusha iliyoko Monduli Mkoani Arusha vyenye thamani ya Sh 3.1
milioni.
Vifaa hivyo ni pamoja na stendi za dripu, vitanda pamoja
na magodoro kwa ajili ya kusaidia wananchi mbalimbali wanaofika katika
hospitali hiyo kupata huduma bora kwa urahisi zaidi.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini,
Baraka Ladislaus amesema kuwa taasisi hiyo imetenga zaidi ya Sh 5.4
milioni kwa mwaka 2024 kwa ajili ya kuchangia huduma mbalimbali nchini
katika sekta ya Elimu, Afya, mazingira na majanga.
“Leo tumekuja
kutoa vifaa hivi ajili ya kurahisisha huduma kufanyika katika hospitali
hii tukitambua umuhimu wa afya bora kama moja ya kipaumbele chetu kwa
maendeleo ya Taifa lolote duniani” amesema Baraka.
Amesema
Serikali imekuwa ikifanya kwa nafasi kubwa katika kuhakikisha huduma za
afya zinapatikana kwa wakati na kwa ukaribu hivyo wao kama wadau wa
maendeleo wana jukumu la kusaidia kuhakikisha mazingira na miundo mbinu
yote ya afya yanapatikana.
“Leo tunagawa vifaa hivi kama sehemu
ya kutoa shukrani kwa wananchi wanaotuunga mkono kwa kufanya kazi na
kufungua akauti zao kupitia benki yetu ambapo tumetenga asimilia moja ya
faida kuhakikisha inawarudia wananchi katika huduma mbalimbali”
Amesema
katika kuzidi kusogeza huduma kwa wateja, wamefanikiwa kufungua matawi
zaidi ya 234 na kusambaza mashine zaidi ya 700 lakini pia wana mawakala
zaidi ya 44,000 nchi nzima ili kutekeleza kauli ya ‘NMB Karibu
yako’”Amesema.
“Pia tumeendelea kutoa masuluhisho mbalimbali ya
kifedha ikiwemo mikopo ya makundi mbalimbali lakini pia kubuni na
kuzindua huduma mbalimbali za kidigitali kusaidia kurahisisha huduma kwa
wateja, hivyo tunawakaribisha pia wateja kutoka hapa jeshini kuja
kufungua akaunti zenu na kuwa sehemu ya mafanikio haya ya huduma kwa
jamii” alisema Baraka.
Akipokea
vifaa hivyo, Kamanda wa kikosi, hospitali ya Jeshi Kanda ya Arusha,
Luteni Kanali Jichola Jilya Masanja ameshukuru kwa msaada huo kutoka NMB
na kusema hayo ni matokeo ya ushirikiano kati ya jeshi na taasisi hiyo
ya kifedha.
“Kutupatia vitanda, magodoro, na stendi za dripu
zitasaidia watanzania wote wanaohudumiwa hapa kupanua wigo wa huduma na
sisi kama wadau tunaahidi kutunza vifaa hivi kwa manufaa ya wengi zaidi
na tuaomba mashirikiano yaendelee sio Arusha tu na maeneo mengine
wafaidike” amesema Mkuu huyo.
No comments:
Post a Comment