NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV
KITUO
cha Ubia Kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC) kimeendesha
Mafunzo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa (TAMISEMI)
Mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo kuhusu majukumu
ya PPPC yamefanyika leo Novemba 11, 2024 katika ukumbi wa JNICC Jijini
Dar es Salaam.
Katika mambo ambayo yamejadiliwa ni pamoja umuhimu
wa kutumia PPP katika utekelezaji wa Mipango ya Taifa ya Maendeleo ya
nchi, muundo wa kisheria na Kitaasisi katika utekelezaji wa program ya
PPP Tanzania.
Mambo mengine ambayo yamejadiliwa ni pamoja na
dhana ya PPP na Orodha ya Miradi ya PPP iliyoandaliwa chini ya Mamlaka
za Serikali za Mitaa.
No comments:
Post a Comment