Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (kulia) na Balozi wa Oman nchini Tanzania, Mhe. Saud Al-Shidhani, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukutana na kufanya mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam, kuhusu kuendeleza ushirikiano baina ya nchi hizo mbili katika Nyanja mbalimbali za maendeleo ikiwemo, katika Sekta ya Nishati na Madini, kutengeneza mazingira bora ya uwekezaji baina ya nchi hizo, Ushirikiano wa mafunzo katika masuala ya Kodi pamoja na kuondoa Utozaji kodi mara mbili kwa wawekezaji na wafanyabiashara watakaofanya shughuli zao kati ya nchi hizo mbili.
Na Joseph Mahumi, WF, Dar es Salaam
Tanzania
na Oman zimekubaliana kuendeleza ushirikiano katika nyanja mbalimbali
za maendeleo ikiwemo Sekta ya Nishati na Madini, kutengeneza mazingira
bora ya uwekezaji, kubadilishana uzoefu na mafunzo katika masuala ya
kodi pamoja na kuondoa utozaji kodi mara mbili kwa wawekezaji na
wafanyabiashara watakaofanya shughuli zao kati ya nchi hizo mbili.
Hayo
yamesemwa wakati wa kikao cha Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck
Nchemba (Mb) alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Oman nchini
Tanzania, Mhe. Saud Al-Shidhani, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha
Jijini Dar es Salaam.
Mhe.
Dkt. Nchemba, alisema kuwa ajenda kubwa ya Serikali ya Awamu ya Sita
chini ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ni kuhakikisha
inawezesha sekta binafsi kuwa na nguvu, sambamba na uboreshaji wa
mazingira ya biashara na uwekezaji, hivyo ushirikiano kati ya nchi hizo
utaendelea kunufaisha sekta binafsi na wawekezaji kwa kiasi kikubwa.
“Serikali
zetu mbili zimeanzisha Tume ya Kudumu ya Pamoja inayosimamia maeneo ya
ushirikiano kati ya nchi zetu mbili, ikiwemo biashara na uwekezaji,
hivyo natarajia kutakuwa na fursa ya kupanua zaidi ushirikiano wetu wa
maendeleo kwa manufaa ya watu wetu” alisema Dkt. Nchemba
Alikubali
maombi ya Balozi wa Oman ambaye alisisitiza umuhimu wan chi yake
kujifunza zaidi kuhusu mifumo ya kodi kutoka Tanzania kwa kuwa Mamlaka
ya Mapato Tanzania ina uzoefu mkubwa katika aneo hilo na kwamba nchi
yake imeanza kutoza kodi hivi karibuni.
“Tunatazamia
Ushirikiano wa mafunzo hasa kwenye masuala ya kodi, na sehemu ambazo
nchi zetu hizi mbili zina utaalamu mahsusi, lengo ni kujengeana uwezo
pamoja ili tuweze kunufaika zaidi” alisema Dkt. Nchemba.
Naye
Balozi wa Oman nchini Tanzania, Mhe. Saud Al-Shidhani, ameipongeza
Tanzania kwa kupiga hatua katika masuala ya kodi na ameona fursa ya
kubadilishana uwezo katika masuala ya kodi ikiwa ni moja ya ajenda kubwa
ya ushirikiano kati ya nchi hizo.
Mhe.
Balozi Al-Shidhani, alisema kuwa biashara kati ya nchi hizi mbili
umeongezeka kwa kiasi kikubwa na kuna tija kubwa ya kuondoa utozaji kodi
mara mbili kwa wawekezaji na wafanyabiashara wanaofanya shughuli zao
kati ya nchi hizo mbili.
“Tunapenda
kusema kuwa Oman tunataka kujifunza namna ya kushughulikia masuala ya
ukusanyaji wa mapato kwa Kuwa Tanzania tayari imepiga hatua katika
masuala hayo na sisi tumeanza miaka ya karibuni, kwa hiyo tuna mengi ya
kujifunza” alisema balozi huyo.
Kikao
hicho kilihudhuriwa na Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje Bw.
Melckzedeck Mbise, Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Sheria Wizara ya
Fedha, Bi. Mwantumu Sultan na Maafisa wengine waandamizi wa Serikali.
Waziri
wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (kulia) na
Balozi wa Oman nchini Tanzania, Mhe. Saud Al-Shidhani, wakiwa katika
picha ya pamoja baada ya kukutana na kufanya mazungumzo katika Ofisi
Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam, kuhusu kuendeleza
ushirikiano baina ya nchi hizo mbili katika Nyanja mbalimbali za
maendeleo ikiwemo, katika Sekta ya Nishati na Madini, kutengeneza
mazingira bora ya uwekezaji baina ya nchi hizo, Ushirikiano wa mafunzo
katika masuala ya Kodi pamoja na kuondoa Utozaji kodi mara mbili kwa
wawekezaji na wafanyabiashara watakaofanya shughuli zao kati ya nchi
hizo mbili.
Waziri
wa Fedha, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (Katikati) akiongoza
kikao chake na Balozi wa Oman nchini Tanzania, Mhe. Saud Al-Shidhani,
wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na balozi huyo katik Ofisi
Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam, kuhusu kuendeleza
ushirikiano baina ya nchi hizo mbili katika Nyanja mbalimbali za
maendeleo ikiwemo, katika Sekta ya Nishati na Madini, kutengeneza
mazingira bora ya uwekezaji baina ya nchi hizo, Ushirikiano wa mafunzo
katika masuala ya Kodi pamoja na kuondoa Utozaji kodi mara mbili kwa
wawekezaji na wafanyabiashara watakaofanya shughuli zao kati ya nchi
hizo mbili. Wengine katika picha ni Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za
Nje Bw. Melckzedeck Mbise (wa pili kushoto), Mkurugenzi Msaidizi wa
Huduma za Sheria Wizara ya Fedha, Bi. Mwantumu I. Sultan ( wa kwanza
kushoto) na Maafisa wengine waandamizi wa Serikali.
Waziri
wa Fedha, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) akizungumza jambo
wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Oman nchini
Tanzania, Mhe. Saud Al-Shidhani (hayupo pichani), katika Ofisi Ndogo za
Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam, kuhusu kuendeleza ushirikiano
baina ya nchi hizo mbili katika Nyanja mbalimbali za maendeleo ikiwemo,
katika Sekta ya Nishati na Madini, kutengeneza mazingira bora ya
uwekezaji baina ya nchi hizo, Ushirikiano wa mafunzo katika masuala ya
Kodi pamoja na kuondoa Utozaji kodi mara mbili kwa wawekezaji na
wafanyabiashara watakaofanya shughuli zao kati ya nchi hizo mbili.
Balozi
wa Oman nchini Tanzania, Mhe. Saud Al-Shidhani, akizungumza jambo
wakati wa kikao na Waziri wa Fedha, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu
(Mb) (hayupo pichani), wakati walipokutana na kufanya mazungumzo katika
Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam, kuhusu kuendeleza
ushirikiano baina ya nchi hizo mbili katika Nyanja mbalimbali za
maendeleo ikiwemo, katika Sekta ya Nishati na Madini, kutengeneza
mazingira bora ya uwekezaji baina ya nchi hizo, Ushirikiano wa mafunzo
katika masuala ya Kodi pamoja na kuondoa Utozaji kodi mara mbili kwa
wawekezaji na wafanyabiashara watakaofanya shughuli zao kati ya nchi
hizo mbili.
Waziri
wa Fedha, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (kulia), akipokea
zawadi ya Kitabu chenye historia ya Oman, kutoka kwa Balozi wa Oman
nchini Tanzania, Mhe. Mhe. Saud Al-Shidhani, mara baada ya kumalizika
kwa mazungumzo yao, yaliyofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha
Jijini Dar es Salaam, ambapo wamejadiliana kuhusu kuendeleza ushirikiano
baina ya nchi hizo mbili katika Nyanja mbalimbali za maendeleo ikiwemo,
katika Sekta ya Nishati na Madini, kutengeneza mazingira bora ya
uwekezaji baina ya nchi hizo, Ushirikiano wa mafunzo katika masuala ya
Kodi pamoja na kuondoa Utozaji kodi mara mbili kwa wawekezaji na
wafanyabiashara watakaofanya shughuli zao kati ya nchi hizo mbili
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dar es Salaam)
Comments